Prof Kitila: Serikali Imepokea Ushauri wa Kujenga Daraja kati ya Dar-Zanzibar

Prof Kitila: Serikali Imepokea Ushauri wa Kujenga Daraja kati ya Dar-Zanzibar

Kwa nini asiwekeze kama atapata faida? Swala sio urefu Bali faida ya kibiashara
Tanzania hatuaminiki kwenye uwekezaji wa aina hiyo. Na sababu za kutokuaminika ziko wazi kutokana na utawala wa Nyerere, na Magufuli alivyoingia madarakani akaondoa kabisa hata ile imani ndogo wanaliyoweza kuwa nayo wawekezaji wa miradi mikubwa ya hivyo.
 
Bro mahitaji yanapimwa hivyo kweli? Ni sawa na kusema useme Kuna mahitaji ya kujenga Daraja kutoka musoma kwenda bukoba sababu watu wa musoma hutumia gharama kubwa kuvuka

Ndani ya miaka 20 au 30 mwekezaji atakua karudisha pesa yake? Mradi wa zaidi ya trillion 100 unarudisha pesa kwa miaka 20 hadi 30? Kwa pesa za wanaovuka? Sidhani unamaanisha

Pia huyo mwekezaji wa kuweka pesa kujenga Daraja kwa gharama hizo yupo wapi dunia hii?? Naomba kumjua
Mradi tu wa bandari kwa trillion 20 jasho lilimtoka miaka zaidi ya 10 ni mvutano. Ije kuwa daraja
Nakubaliana na wewe, hata hivyo kujua gharama halisi za Mradi vyema ikafanyika feasibility study kuweza kujua kama huo Mradi utatekelezeka ama uishie kwenye Makaratasi
 
Hivi Kwa hali ya Uchumi wetu tutaweza kweli hizo gharama za Ujenzi?

Labda kama tutajenga Kwa njia ya PPP then tukawa tunatumia Kwa kulipia kama ilivyo daraja la Mwalimu Nyerere - Kigamboni

Ni wazo zuri kulitekeleza kama Kuna hiyo nafasi
Kupanga ni kuchagua🤣🤣🤣🤣🤣📌
 
Nakubaliana na wewe, hata hivyo kujua gharama halisi za Mradi vyema ikafanyika feasibility study kuweza kujua kama huo Mradi utatekelezeka ama uishie kwenye Makaratasi
Gharama zinazokaribia wala sio shida kujua sababu yapo ya hivyo yamejengwa huko kwa wenzetu
Issue hakuna wa kuweka hiyo pesa kwenye Daraja ndio maana nilikutolea hata mfano wa bandari ya bagamoyo ambao mradi ulikua wa trillion 20 lakini wamevutana miaka 10 na hakuna kilichoendelea
 
Nakubaliana na wewe Mkuu, nafikiri Kuna haja tathmini ya kina ikafanyika ili hata kama tutajenga Kwa PPP basi tujue pros and cons zake kama Taifa
 
Tanzania hatuaminiki kwenye uwekezaji wa aina hiyo. Na sababu za kutokuaminika ziko wazi kutokana na utawala wa Nyerere, na Magufuli alivyoingia madarakani akaondoa kabisa hata ile imani ndogo wanaliyoweza kuwa nayo wawekezaji wa miradi mikubwa ya hivyo.
Unataka kutuongopea sasa, mwekezaji hata serikali iwe unstable kiasi gani akiona fursa anakimbilia fasta. Ndio maana pamoja na machafuko yote sehemu zenye madini congo n.k lakini bado wawekezaji wanaenda

Hata Somalia ambayo ni failed state bado wawekezaji wanaenda.

Issue ni ukubwa wa gharama kulinganisha na mradi. Ndio maana kule lindi kwenye LNG wapo tayari kuweka hiyo trillion 100 sababu wanajua inarudi. Hayo ya sijui atakuja raisi gani ni propaganda tu
 
Kwanini tunnel la chini lisijengwe Bagamoyo mpaka ZnZ? Au daraja maana ni karibu na kufanya bagamoyo liwe jiji kubwa kuliko kila msongamano mnapelea Dar
 
nani anagharamia? mambo mengine mwachieni bhakressa
 
Nakubaliana na wewe Mkuu, nafikiri Kuna haja tathmini ya kina ikafanyika ili hata kama tutajenga Kwa PPP basi tujue pros and cons zake kama Taifa
Mkuu kujengwa daraja la hivyo kwa nchi ya ulimwengu wa tatu ni ndoto. Sababu kubwa ni gharama na pia jiographia ya hayo maeneo mawili kuweka Daraja ni ngumu mno sababu ya mkondo wa bahari uliopo
 
Kwasabab ni wazo litapokelew na kujadiliwa ikiwa Kam miswaada mingine ban ndugu.haitawa official hiyo presha za nin
 
Kwanini tunnel la chini lisijengwe Bagamoyo mpaka ZnZ? Au daraja maana ni karibu na kufanya bagamoyo liwe jiji kubwa kuliko kila msongamano mnapelea Dar
Hiyo fedha iingizwe kwenye Maji safi na salama kwa wote kwanza hapo ni bora aletwe mwekezaji wa Ferry kubwa zenye kubeba hadi Malori.
 
Prof acha uchawa, kama kuna hela wajenge SGR kwenda South Africa tuongeze biashara. Na kama litajengwa daraja hili litaitwa Daraja la Muungano, au Union Bridge
 
Back
Top Bottom