Prof. Lettice: Kama mmeshindwa kuziba Mabomba tupeni sekta binafsi

never-ending battle

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2024
Posts
277
Reaction score
183
Profesa ataka sekta binafsi iokoe mamlaka za maji nchini

Kongamano la Kitaifa kuhusu Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) katika Sekta ya Maji lililofanyika Mei 9, 2026 jijini Dar es Salaam limeibua mjadala kuhusu changamoto za ufanisi, ucheleweshaji wa huduma na mianya ya rushwa katika mamlaka za maji nchini ikiwemo DAWASA.

Akiwasilisha mada kwa hisia na uzoefu wake binafsi, Lettice Rutashobya, ambaye aliwahi kuhudumu katika Bodi ya DAWASCO kwa kipindi cha miaka sita, alisema bado kuna changamoto kubwa katika usimamizi wa huduma za maji licha ya uwepo wa taasisi na wataalamu wa kutosha.

Profesa Rutashobya alieleza kusikitishwa na kasi ndogo ya kushughulikia hitilafu za miundombinu, hususan mabomba yanayovuja na kuchelewa kwa huduma za matengenezo, hali inayochangia upotevu mkubwa wa maji na usumbufu kwa wananchi.

“Kama wahandisi hawatoshi, na inachukua mwaka mmoja au hata miwili kurekebisha bomba linalovuja, basi kuna haja ya kujiuliza kwa nini tusitumie mfumo tofauti na kuipa nafasi sekta binafsi kusaidia,” alisema Profesa Rutashobya.

Mbali na changamoto za kiufundi, Profesa huyo pia alifichua kuwepo kwa vitendo vya ukosefu wa uadilifu vinavyofanywa na baadhi ya watendaji wa chini, ambapo wananchi hudaiwa fedha zisizo rasmi kwa madai ya kununua vifaa vya kuunganishiwa huduma za maji.

Profesa Rutashobya aliiomba Serikali kuharakisha utekelezaji wa mfumo wa PPP katika sekta ya maji ili kuvutia uwekezaji, kuongeza uwajibikaji na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Kwa mujibu wake, ushiriki wa sekta binafsi unaweza kusaidia kuongeza kasi ya matengenezo ya miundombinu, matumizi ya teknolojia za kisasa pamoja na kuimarisha usimamizi wa rasilimali za maji nchini.

​
Chanzo: The Newsroom tz
 
Naona PPP imevamiwa na maprofesa

IMG-20260512-WA0066.jpg
 
Sawa sawa
 
Point msomi
 
WASOMI
 
Back
Top Bottom