Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba akiwa Bukoba Vijijini: Nitasimamia elimu bora na matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano

Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba akiwa Bukoba Vijijini: Nitasimamia elimu bora na matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano

Lissu hajawahi kukusanya watu, watu ndo wanakusanyika kwa ajili yake. Kuna anayekusanya watu kwa malori unamjua vizuri usijitoe ufahamu.
... jibu bora kabisa la zama zetu hizi!
 
View attachment 1580737View attachment 1580738NITASIMAMIA ELIMU BORA NA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO "PROF.LIPUMBA"

BUKOBA VIJIJINI


Serikali ya umoja wa kitaifa chini ya CUF itahakikisha kuwa watoto wote wa Tanzania wanakuwa na haki ya kupata elimu bora ya msingi, elimu ya sekondari na elimu ya juu. Kila raia atahimizwa kujiendeleza kielimu hasa kwa kutumia vizuri teknolojia ya habari na mawasiliano.

Serikali ya umoja wa kitaifa itakayoundwa na CUF itatoa kipaumbele maalum katika kuwaendeleza kielimu wasichana na kujenga misingi imara ya kuendeleza elimu za hisabati, sayansi na teknolojia.

Serikali ya umoja wa kitaifa chini ya CUF itahakikisha kwamba ifikapo 2025 asilimia 50 ya Shule za Umma nchini zinakuwa na Uwezo wa Kufundisha wanafunzi wake kwa njia ya TEHAMA na asilimia 100 ifikapo 2028.

Hili litawezesha wanafunzi wengi kuendelea na masomo hata pale shule zitakapofungwa kwa dharura kama tulivyojifunza kupitia janga la CORONA.
Hahahaaa, kwisha habari yake propumba. Afadhali yule bwana ubwabwa.
 
Back
Top Bottom