Mgombea Urais wa CUF, Prof Lipumba amemshukia vikali Tundu Lissu kwa kumuita mnafiki asiyejua chochote kuhusu Sera, Amani, Maendeleo na Demokrasia ya Nchi yetu.
Prof. Lipumba amehoji sababu za Lissu kumuwekea pingamizi kwenye tume ya uchaguzi eti kisa tu amefuata maelekezo ya tume ya uchaguzi!! Lipumba amehoji asipofuata maelekezo ya tume ya uchaguzi afuate maelekezo ya nani?? Pia amehoji wagombea wote wa urais mwaka huu wamefuata maelekezo ya tume ya uchaguzi akiwemo Membe, iweje awawekee pingamizi wagombea wawili tu?
Hali hiyo imemsikitisha sana Lipumba na kuwaasa watanzania kutokumchagua Lissu kwani ameonyesha udikteta wa kuminya demokrasia mapema sana.
View attachment 1550344