Ngalikihinja
JF-Expert Member
- Sep 1, 2009
- 33,643
- 36,090
Nimejaribu luwaza maneno yale na luyalinganisha na uaomi wake wa uchumi, NAHISI KAMA HAVINA UHUSIANO
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Professor anayeamini mwanachana ni mwaminifu kuliko benki!!Mwenyekiti wa Cuf Prof Lipumba amesema sh 300m za ruzuku walizihamishia kwenye akaunti binafsi ya mwanachama mwaminifu Omari Muhina ili kuzilinda zisiibiwe pale benki.
Prof Lipumba amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari leo.
Source ITV habari
Hivi sakaya yupo hai/mzima?Yaani huyu na Sakaya wameipiga sana cuf
In God we Trust
Ahaa sasa nimemuelewa Prof. walipewa 380, hizo 80 zikanunulia magari, wakaamua kuhamisha mia tatu ili zisiibiwe.
Kama mwenyekiti wako alivyokua anasambaza korona kwa raia wasiokuwa na hatia.Ni zaidi ya mpigaji kama maccm wenzake
In God we Trust
Wanasiasa au vyama vyao na watawala au viongozi wa vyama tawala ni makundi yanayogombea na yale yanayoishi kwa jasho la walalahoi.Najiuliza wazo la Vyama vya siasa kupewa fedha za "ruzuku" mwanzilishi wake duniani alikuwa nani?
Maelezo mazuri, siasa ni mradi mzuri sana nchini Tanzania.
P
Halafu alisema walipewa kibali na msajili wa nyama vya siasa. Hii kusema kweli ni matumizi mabaya ya fedha za walipa kodiHahahaaaa........mwanachama mwaminifu Takukuru inamuhusu!
Sijui kwanini nilisoma mambo magumuuu na hela naipata kwa ugumuuu! Sifa za kijinga zimeniponza![emoji1787][emoji1787] Ningejifanyia zangu Siasa ningetoboa kiulainiiii kama Mh Madreva na wa aina yake!Maelezo mazuri, siasa ni mradi mzuri sana nchini Tanzania.
P
Mwenyekiti wa Cuf Prof Lipumba amesema sh 300m za ruzuku walizihamishia kwenye akaunti binafsi ya mwanachama mwaminifu Omari Muhina ili kuzilinda zisiibiwe pale benki.
Prof Lipumba amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari leo.
Source ITV habari
Kaka maelezo yanamashiko .ila mashaka yapoMaelezo mazuri, siasa ni mradi mzuri sana nchini Tanzania.
P
lipumba ni mwiziTarehe 26 March 2020, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere aliwasilisha ripoti ya ukaguzi wake ya 2018/19 kwa Rais John Magufuli katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dodoma.Pamoja na Mambo mengine CAG Charles Kichere alisema:
"Mheshimiwa Rais, nilibaini Chama cha Wananchi CUF kilipokea ruzuku toka Serikalini ya Kiasi cha Shilingi milioni 369.38 Lakini Chama hicho kilihamisha kiasi cha shilingi milioni 300 kutoka akaunti ya Chama kwenda akaunti binafsi ya mwanachama na kiasi cha shilingi milioni 69 kilitolewa kama fedha taslimu.
Hata hivyo nyaraka za matumizi ya fedha hizo hazikuwasilishwa kwangu kwa ajili ya ukaguzi."
Kauli hii ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imeleta mtafaruku na sintofahamu kubwa kuhusu usimamizi wa fedha za Chama cha CUF.Ni vema tukaweka sawa kumbukumbu zetu kwamba tukio hili lilitokea Januari 2017. Wakati huo Chama chetu kilikuwa katika mgogoro wa uongozi na akaunti za Chama katika Benki ya NMB zilikuwa na tishio la kuzuwiwa.
Naomba nikumbushe kuwa tarehe 2 Desemba 2016,Tume ya Taifa ya Uchauzi ilitangaza uchaguzi mdogo wa Udiwani katika kata 22 za Tanzania Bara.Nikumbushe kuwa baadaye Time ilifanya masahihisho na kueleza kuwa ni kata 20 ndizo zitakazohusika na uchaguzi mdogo.Pia CUF iliamua kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Dimani,Zanzibar.
Hatimaye Chama kilisimamisha wagombea 14 kati ya kata 20 zilizotangazwa kurejesha uchaguzi.Upande wa Zanzibar CUF iliweka Mgombea Ubungo Jimbo la Diwani
Naomba nikumbushe kuwa wakati uchaguzi mdogo unatangazwa,Chama kilikuwa hakipewi ruzuku ya serikali.Kwa sababu tulitaka kushiriki uchaguzi na hatukuwa na fedha,mnamo tarehe 28 Desemba 2016 nilimuandikia Msajili wa vyama vya Siasa kuiomba Ofisi yake ikipatie Chama chetu fedha zitokanazo na ruzuku ya kila mwezi ya chama toka Serikalini ili kiweze kishiriki kikamilifu katika chaguzi ndogo zilizotangazwa kurejewa hapa nchini na kutekeleza Mpango Mkakati wa Ujenzi wa Chama chetu.
Msajili wa Vyama vya Siasa aliridhia Chama kipate sehemu ya ruzuku ili kishiriki katika uchaguzi na kutekeleza shughuli za Chama.Fedha hizo ziliwekwa kwenye akaunti ya Chama ya Benki ya NMB,tawi la Temeke.
Katika kipindi kulikuwa na tishio la aliyekuwa Katibu Mkuu kuzuia akaunti zetu zote za Chama upande wa Tanzania Bara zisifanye kazi.Katika hali hiyo Kamati ya Utendaji iliamua shilingi 300 tulizoomba kwa ajili ya kugharamia uchaguzi zihamishwe akaunti ya Benki.Mwanachama huyo ni Masoud Mhina Omari,aliyekuwa Naibu Katibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na sasa Naibu Mkurugenzi wa Mafunzo,Itifaki na Udhibiti.
Shilingi milioni 69 zilitolewa kama fedha taslimu kuanzia kugharamia shughuli za kampeni za uchaguzi zikiwemo ziara za viongozi kwenda kwenye kata zenye uchaguzi mdogo.
Fedha zote zilizowekwa kwenye akaunti ya Masoud Mhina Omari zilitumiwa na Chama katika masuala ya Uchaguzi na uendeshaji wa shughuli za chama.Wakaguzi wa CAG waliokuja kutukagua walipewa maelezo haya na nyaraka za matumizi ya Chama ya Mwaka2016/17.
Chama kinamshukuru Masoud Mhina Omari kwa Uaminifu wake.Hatua ya kuweka fedha kwenye akaunti yake ilitusaidia kukamilisha shughuli za chama kwani baadaye Benki ya NMB ilizuwia kutoa fedha kwenye akaunti zetu zote za Tanzania Bara.
Naomba nisisitize tukio hili la kuhamisha fedha kwenda akaunti ya Masoud Mhina Omari lilitokea Januari 2017 kwa sababu ya tishio la kuzuia kutoa fedha toka akaunti za Chama.
Mgogoro wa Chama umemalizika na taratibu za fedha zinazingatia kanuni za fedha za Chama.
Tunakubaliana na Ushauri wa CAG kuwa mifumo ya udhibiti wa fedha ndani ya chama iimarishwe kwa kufuata sheria na Katiba ya Chama .Hivi sasa Mhasibu anaandaa mfumo imara wa udhibiti wa fedha ndani ya chama.
Prof.Ibrahim Haruna Lipumba
Mwenyekiti waTaifa,27 March 2020.
Kama mwenyekiti wako alivyokua anasambaza korona kwa raia wasiokuwa na hatia.
Nafuu angenyamaza kimya,asubili Takukuru wakati wanamhoji ndipo awajibu,sasa anajibu kwenye vyombo vya habari ,hana hata aibu.
Yalikuwa ni maoni ya wa Cdm, Cuf walikuwa hawajatoa tamko lolote rasmi.mbona wanatofatiana maelezo na idara ya habar ya CUF, niliona uzi humu ndani wakisema kipindi hicho hawausiki,chama kilikuwa chini ya maalimu seif, au nulielewa vibaya wadau?