Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,170
- 6,757
Waziri wa fedha amechemka. Maana hata takwimu alizotoa hazilandani na kilichomo kwenye bajeti.
Na hii bajeti haikufanyiwa utafiti
Profesa Lipumba: Bajeti ya Serikali mbovu kuwahi kutokea.
=========
Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba ameikosoa bajeti ya Serikali akisema ni mbovu kuwahi kutokea tangu apate uzoefu wa kuzichambua bajeti zinazowasilishwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Kutokana na kasoro alizodai kuwemo katika bajeti hiyo, Profesa Lipumba ambaye ni mtaalamu wa uchumi, ameishauri Serikali kujenga utamaduni wa kufanya utafiti wa kina wa sera za kodi ili kutengeneza mipango ya kukuza maendeleo na kuongeza ajira kwa vijana na kutokomeza umaskini.
Ameyasema hayo leo Juni 19 jijini hapa wakati akiichambua bajeti ya Serikali iliyosomwa bungeni Juni 14, akifafanua kuwa bajeti hiyo imeshindwa kuakisi malengo ya Rais Samia Suluhu Hassan likiwemo la kuanzisha Tume huru ya uchaguzi.
"Hotuba hiyo ilikuwa mbovu mbovu kuwahi kutokea kwa Waziri wa Wizara ya fedha tangu kupata uzoefu wangu wa kupitia na kuzichambua bajeti zote," amesema.
Ametoa mfano wa taarifa za Wizara ya Mifugo akisema hazioani na kitabu cha hali ya uchumi.
“Ukirejea kwenye kitabu cha uchumi wa taifa hazipo, napata wasiwasi. Naomba kabla ya kwenda kusoma bajeti ni vizuri zipitiwe na wataalamu kuhakikiwa tarakimu kabla ya kwenda kusomwa zifanane na zile zilizopo kwenye kitabu cha hali ya ukuaji uchumi wa taifa," amesema.
Kuhusu mfumuko wa bei amesema Watanzania wanalalamika kuongezeka kwa gharama za maisha. Kila kitu hasa vyakula na nishati vimepanda bei, lakini taarifa ya Serikali inaeleza kuwa bei zimeongezeka kwa asilimia 4 tu jambo ambalo alilodai kuwa si kweli.
"Vitu ulivyonunua kwa Sh100,000 Mei 2021, watu kwa sasa wanatumia Sh104,000 tu Mei 2022. inashangaza kuona takwimu za Serikali gharama za maisha nchini zimeongezeka kwa kasi ya chini kuliko gharama za maisha Marekani na nchi za Ulaya," amesema.
Kuhusu elimu bila malipo, Profesa Lipumba amesema katika bajeti hiyo Serikali imetangaza kufuta ada za kidato cha tano na sitana kujigamba kuwa sasa Tanzania ina elimu bure toka darasa la kwanza hadi kidato cha sita. lakini ukweli ni kwamba ada ni sehemu ndogo chini ya asilimia 10 kwa kidato cha tano na sita za gharama ambazo mzazi ana wajibika kulipa ili mwanae aenendelee na masomo.
Kuhusu sera za kodi, alisema Waziri huyo amefanya makosa kuunganisha vitambulisho vya taifa na ulipaji wa kodi hasa katika kipindi hiki ambacho Serikali haijakamilisha zoezi la kuwapatia vitambulisho vya taifa watanzania wote baada ya zaidi ya miaka kumi toka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) kuanzishwa.
"Ni muhimu Serikali ikajikita kuharakisha Wananchi kupata vitambulisho vyao, lakini wakiendelea kuongelea suala hilo wanaweza kusababisha watu wasijisajili wakijua kufanya hivyo watatozwa kodi," amesema.
CREDIT: Mwananchi