Prof. Lipumba: Bajeti iliyosomwa ni mbovu haijawahi kutokea tangu tupate uhuru. Takwimu nyingi haziko sahihi

Professor Lupumba ni Professor mbovu kuwahi kutokea toka kuanza kuubwa dunia hii
 
Lakini hata mimi naunga mkono kuwa hii bajeti nadhani ni ya ovyo kwa maana serikali yetu kutenga trilioni moja na kichele kwa ajili ya maendeleo AF trilioni 13 kwa matumizi ya kawaida hilo jambo linatia wasiwasi sana
Revenue expenditure over Capital expenditure....deterioration of an economy..
 
Huyu jamaa hajawahi badili haya maneno tangu aingie siasani
 
Rais Samia kumteua Mwugulu kuwa waziri wa Fedha na uchumi ni kosa kubwa Sana alifanya kwa Sababu huyu waziri kwanza hayupo sirious na kazi pia anautoto mwingi Sana yeye anachokijilua ni kupiga siasa tu.
 
Kasema vizuri ila kisiasa hapo ategemee mambo mawili kulamba asali ili atulie au kinyume chake ,kikubwa atulie .
Ndiye mpinzani anayetegemewa kuchambua bajeti tangu 1996
 
Hiyo point uliyowekea rangi ni ya muhimu sana kwani itafanya watu wasitafute tena hivyo vitambulisho vya NIDA kukwepa kodi. Ni sera ambayo imetolewa bila umakini wowote. Swala la vitambulisho vya uraia lisiunganishwe na kodi, ama sivyo watu hawatavitafuta. Lina unintended consequences nyingi kuliko faida

Mfano mmoja mzuri ni kuwa serikali ya Trump ilitaka kutumia Sensa ya mwaka 2020 kuweka kipengele ambacho kinataka mtu aeleze kama ni raia au si raia. Kifungu hicho kilipingwa vikali kwa sababu kingesababisha watu wasiokuwa raia wasijitokeze kuhesabiwa kwa kuogopa kunyanyaswa na serikali. Sensa inataka kujua widadi ya watu halisi wanaoishi nchini siyo kujua uraia wao; kikafutwa.
 
Mtu mwenye Phd ya uchumi huwezi kupendekeza viga'amuzi kulipiwa tozo. Au kila mtanzamia akifikisha umri wa miaka kumi na nane alipe kodi. Ina maana ukiwa mtu mzima tu kodi.
Kiswahili rahisi kueleweka CCM na serikali yao wangesema tu kuwa, KODI YA KICHWA imerudishwa baada ya kuondolewa miaka zaidi ya 22 iliyopita ili watu tujadili na tujue tunakokwenda...

Huku kuzunguka zunguka badala ya kuwa straight haitamsaidia Mwigulu Nchemba na Rais wake Mama Samia Suluhu...!
 
Huku Mwigulu kule Makamba, tutaelewana tu labda Mama awe na jicho la kuona mbali.
 
Kusema kuwa national ID watu hawatavitafuta, ni kujidanganya tu...

Kwa sababu, serikali inaweza kuweka mazingira ambayo yatamlazimisha kila mtu kukitafuta kitambulisho hicho...

Mfano, linaweza kuwekwa sharti kuwa ili uhudumiwe benki, au kwenye ofisi za umma ikiwemo hospitali,kujiunga chuo, ajira nk lazima uwe na National ID...
 
Ninadhani tatizo lipo kwa watendaji wa Wizara ya fedha na Mipango hawana weledi.Katibu Mkuu ndiyo mtendaji Mkuu, Waziri anapewa kupitia bajeti tu, lakini kama Waziri,ana kiburi, anaweza kubadili mtiririko wa Bajeti aonyeshe kuwa yeye ana PHD
 
Kwa hiyo hicho kilichoandikwa hapo ndio uchambuzi wa Professor Mbobezi na nguli wa uchumi!? Au mmepunguza alichosema? Maana sioni Hizo takwimu (facts and figures) alizotoa hapo!
Tumia akili, soda ilikuwa inauzwa sh 500, sasa inauzwa 600, imepanda kwa aslimia 20. Nauli ilikuwa 400 sasa 500, imepanda kwa asolimia 25. Imflation kwa mwaka ni asilimia 20-25. Huo ni mfano tu, sasa mwigulu anasema inflation ni asilimia 4 amepata wapi. Usichoelewa ni nini hapo. Kifupi ukitaka kuweka watu wako kwenye uongozi haya ndio matokeo yake.
 
Ni ngumu sana kumuamini mwanasiasa kama Lipumba
 
Hali Ni mbay mnasema inflation ipo lkn watu wanamud bidhaa hatari hi hyper inlfatinon
 
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Mhe. Ibrahim Lipumba amesema Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Mchemba amefanya makosa ya kimkakati kuunganisha vitambulisho vya Taifa na ulipaji kodi huku akieleza itaathiri motisha ya wananchi kujisajili kupata vitambulisho hivyo..

Chanzo: DarMpya Blog.

Yaani na Wewe Baba yangu Mzee Lipumba ninavyokuheshimu kwa kuwa na IQ kubwa hukumjua tu huyo ni typical Nut?
 
Anamjua. Pale anamwambia boss wake kwamba kibarua wake ni chenga
 
BAJETI YA KIHUNI HII UONGO MWINGI KULIKO UKWELI ETI TUNABANA MATUMIZI HUWEZI KUBANA MATUMIZI KWA NCHI YENYE VIONGOZI WASIO WAZALENDO KWA NCHI NA WANANCHI

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…