Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba (Ilolangulu): Nichagueni niwe Rais wa nchi hii ili niweze kutokomeza njaa kwa wote na kuhakikisha lishe bora kwa wajawazito na watoto

Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba (Ilolangulu): Nichagueni niwe Rais wa nchi hii ili niweze kutokomeza njaa kwa wote na kuhakikisha lishe bora kwa wajawazito na watoto

CUF Habari

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2019
Posts
239
Reaction score
234
IMG_20200918_092820_541.jpg


NICHAGUENI NIWE RAIS WA NCHI HII ILI NIWEZE KUTOKOMEZA NJAA KWA WOTE NA KUHAKIKISHA LISHE BORA KWA WAJAWAZITO NA WATOTO "PROF.LIPUMBA"ILOLANGULU AKIPITA KUSALIMIA.

Nitahakikisha kuwa kila mwananchi anakuwa na uwezo au kuwezeshwa kupata milo mitatu kwa siku. Hatua za makusudi zitachukuliwa kuhakikisha kuwa kinamama wajawazito na watoto wachanga wanapata lishe bora itakayowasaidia watoto kujengeka vizuri katika viungo vya mwili, kinga ya mwili na ubongo, ili waweze kushiriki kikamilifu katika kujielimisha na kujiendeleza.
 
Hiv hiyu Lipumba alikuwa best student kweli??? kama watu wanavyodai ...mbona anashiindwa kusoma alama za nyakti kabisa anaona na yeye anagombea uraisi?
 
Naomba mnifikishie tu salamu zangu kwa Profesa; Akubali kupumzika. Kiukweli kwa sasa Profesa Lipumba hana mvuto!

Ikiwezekana ajirudie zake Chuo Kikuu akapige kazi. Siasa kwa sasa imeshamtupa mkono. Kiufupi tu Hana Jipya! Habari ya mjini kwa sasa ni Mh. Tundu Lissu, kiboko ya Magufuli.
 
Maswali kwa mgombea

1. Kukosa milo ni matokeo tu ya umasikini, yeye anazungumzia vipi suala hilo na mikakati ya vitendo kuhakikisha tunaondokana nalo kama nchi?

2. Suala la ukosefu wa Ajira ni moja ya sababu ya kukosa milo mitatu, anazungumziaje hilo.

3. Elimu duni au elimu isiyo na ujuzi kamili (Semi-skilled) ni matokeo ya kukosa milo pia Prof anazungumziaje hilo.

Kwanini mgombea aisngejikita kwenye issues material badala yake anakomaa na vijitu petty kabisa hadi watu wanaanza kuhoji uelewa wake wa mambo kama mdau hapo juu?

Au kuna kitu CUF ngangari inaogopa!
 
Nimei zoom picha yake ya ukutani ipo kama cartoon flani🤣🤣. Huyu aliuza chama sasa anataka kuuza nchi?
Screenshot_20200918-110349_Samsung Internet.jpg



Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Hawa intellectual thieves, mawazo ya raisi wangu #Rungwe_2020..kila mtu anayatumia!

Tumshauri a copyright, hawa wadesaji sugu watulipe!

Everyday is Saturday 😎
 
Ajenda ya "Milo na lishe" naona kama mmeidandia kutoka kwa H. Rungwe (imaana sera zeni haziuziki). Kama vipi si mngeungana na Rungwe muwe kitu kimoja ktk suala zima la lishe.
 
Back
Top Bottom