Prof. Lipumba: Kuna vyama vina sera za kutongoza mademu

Prof. Lipumba: Kuna vyama vina sera za kutongoza mademu

Mikutano ya hadhara Imeruhusiwa.

Kwann anangangania press??
 
Makamanda naona wamekuja juu baada ya kupigwa kitu kizito na Professa Lipumba, wakiwa hawaelewi hata nini kinaendelea, waamua kumshambulia yeye binafsi.
 
Anamtukana msajili huyu.

Kwahiyo msajili kasajili barua za mapenzi na sio katiba za vyama vya siasa??
 
Kuna umri ukifika baadhi ya maneno hayatamkiki vinginevyo zimepungua. Mzee huyu hakutakiwa kusema "mademu". Bora angesema "wanawake".
 
Prof. Lipumba: Hitimisho, baraza kuu linatoa wito kwa watanzania pamoja na waandishi wa habari kujiunga na chama cha CUF chenye lengo la kujenga nchi yenye haki sawa na furaha kwa wananchi wote. Kitakachotumia rasilimali za nchi yetu kukuza uchumi unaoongeza ajira utakaowapa na kuwanufaisha wananchi wote, kitakachoimarisha uwajibikaji na kujenga mfumo endelevu wa kupambana na rushwa na ufisadi.

Vyuma vinazidi kukaza, tujiunge na kuimarisha CUF ili hatimaye tupate grisi ya vyuma vilivyokaza na kuna vyama vingine vina sera ya kutongoza mademu, sisi tuna sera ya kujenga nchi yenye haki sawa na furaha kwa wananchi wote.

'...vyama vya kutongoza madem' 😂. Hapo kuna mtu kapigwa kijembe 😂🤣💃🚶🚶
 
Distinguished Professor anaongelea sentensi ya rejareja jukwaani anaita sera.

Usihadaike na akili za darasani mkuu,
Ukiambiwa alikuwaga Tanzania One form six na GPA ya 5 UDSM na Masters alisoma Stanford university hawez amini.
Unapagawa na wanasiasa?,hapo anapiga kabobo taaluma kaweka pembeni
 
Unapagawa na wanasiasa?,hapo anapiga kabobo taaluma kaweka pembeni
Sijapagawa... wanasiasa ni kioo cha jamii yetu...Kwenye akili anatambulika hata akichekesha...

Ulishasikiaga utani wa ki profesa au propaganda ya ki profesa?
 
'...vyama vya kutongoza madem' 😂. Hapo kuna mtu kapigwa kijembe 😂🤣💃🚶🚶

..hiyo ni fair game.

..Mbowe alikosea kwa hiyo ni sahihi kupigwa vijembe / madongo.

..lakini Mbowe alikuwa muungwana kuomba radhi kwa kauli hiyo.

..Prof naye anatakiwa atambue malengo yake, na ajue ni hoja zipi zitakiinua chama chake.
 
Back
Top Bottom