Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba: Kura sio siri tena

Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba: Kura sio siri tena

HAO
Prof. Lipumba ameibua hoja nzito kuhusu USIRI WA KURA kwenye Uchaguzi huu.

Akihojiwa na ITV mchana huu amesema ameshtushwa na Makarani ambao walikuwa wakinakiri namba za Kitambulisho cha Mpiga Kura kwenye Karatasi ya Mpiga Kura.

Hivo Tume au Serikali wakitaka kujua nani kampigia nani ni rahisi sana. Wanaingiza namba ya Kitambulisho halafu Wana Search na jina litaonekana.

Wewe unasemaje?

Tujadili.
NDO SISIEMU SASA KWA WALE WATUMISHI WA UMMA NA WALIOPEWA RUHUSA KWENDA KUPIGA KURA WALIOPIGA KURA KWA WAPINZANI NDO BASI TENA
 
Anazeeka vibaya, namba inaandikwa pale juu ndio lakini baadae inapochanwa karatasi ili upewe ukapige kura, ile namba inabaki kwenye kitabu haitoki na karatasi.
Upo sahihi mkuu, namba inabaki kama kishina cha ticket ktk ballot paper hamna namba.
 
Huyu professor muongo sana karatasi gani iliyoandikwa namba ya kitambulisho? Aache mambo yake yeye ni serial loser na atabkia kuwa hivyo.

Congratulations in advance President Magufuli

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Akiongea na ITV leo saa 6 Mh mgombea urais wa jamuhuri wa muungano wa Tanzania kupitia CUF ,amesema ameshtushwa baada ya kuona namba yake ya kadi ya mpiga kura ikiandikwa katika ballot paper aliyopewa hivyo kupelekea kua kama watachukua namba hizo zilizoandikwa kwenye ballot paper inakua rahisi kujua nani kampigia kura nani na nani na hivyo kura sio za siri tena.

Source;ITV

Nb;Nadhani imewekwa hivyo ili JIWE agundue wasaliti wake ni nani na nani katika uchaguzi huu na ajabu kwanini vyama vya upinzani halijagundua hili mapema.
Bila tume huru ya uchaguzi tutaendelea kuwa na uchafuzi wa haki za kuchagua na kuchaguliwa...
 
Je, kura hii ni Siri?

Kwanini mwaka huu tofauti na miaka mingine, NEC wameweka sehemu ya kujaza namba za kitambulisho.

Huku wakiwataka wafanyakazi wa uma kupiga kura siku moja kabla?

Je, Ajira za watu hasa walio chagua upinzani ziko salama?
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Daaah! Nimepata wasiwasi sana leo wakat msimamiz anajaza number za kadi kwenye karatasi za kura. Huo usiri wa kura cjui uko wap.
TOTᗩᒪ ᑎOᑎՏᗴᑎՏᗴ huu uchaguzi.
 
Prof. Lipumba ameibua hoja nzito kuhusu USIRI WA KURA kwenye Uchaguzi huu.

Akihojiwa na ITV mchana huu amesema ameshtushwa na Makarani ambao walikuwa wakinakiri namba za Kitambulisho cha Mpiga Kura kwenye Karatasi ya Mpiga Kura.

Hivo Tume au Serikali wakitaka kujua nani kampigia nani ni rahisi sana. Wanaingiza namba ya Kitambulisho halafu Wana Search na jina litaonekana.

Wewe unasemaje?

Tujadili.

Mazoea yetu ndiyo huweza kufanya jambo au kitu fulani kionekane sio cha kawaida.

Hata kama ingekuwa kweli, Tanzania haiwezi kuwa nchi ya kwanza kuwa na identifying information kwenye ballot paper. Mail-in/absentee ballot (katika nchi zinazoruhusu hiyo), ikiwemo Marekani, zinaweka identifying information kwenye mail-in/absentee ballot paper. Tena kuna tamko la uthibitisho linalohitaji signature ya mpiga kura. Bila signature, kura inapoteza sifa za kura halali.
 
Mkuu kipande kinachojazwa namba ya mpiga kura kinabaki kwenye kile kijitabu cha kura na wewe unapewa karatasi yenye wagombea na wala ile karatasi haina serial number useme kua wanaweza kuitafuta badae.

Unless kama umeanza kupiga kura mwaka huu au wewe ulipoenda pale kwenye kibox cha kupigia kura karatasi yako ilikua imeandikwa number yako ya mpiga kura?
 
Daah leo wengi wanaumbuka humu. Kumbe hamjapiga kura kazi kulalamika. Waliopiga kura wameona namba ikibaki kwenye kitabu na sio kwenye karatasi la kura
 
Back
Top Bottom