Tetesi: Prof. Lipumba na wafuasi wake wakesha wakiomba radhi kwa Maalim Seif na viongozi wengine

Tetesi: Prof. Lipumba na wafuasi wake wakesha wakiomba radhi kwa Maalim Seif na viongozi wengine

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,903
Wahenga walisema kupanda mchongoma kuushuka ndio ngoma pamoja na usaidizi wa kila Aina anaopewe lipumba na wanaomfadhili ili kuidhoofisha CUF sasa mambo yameharibika upande wa Lipumba ni dhahiri sasa Lipumba ameedhoofika yeye kifikra na kiafya baada ya kutengezewa ziara fake kisiwani Pemba na baada ya kuiona hali ya Pemba ilivyo lipumba aliporudi Dar aliwakusanya wasaliti wenzake akawaambia jamani tusidanganyane alisema lipumba hali kiupande wetu ni mbaya wanaotuunga mkono ni wachache mno na hao wanakimbia siku hadi siku.

Tulitegemea Upande wa bara ungetuunga mkono lakini nako hali imekua mbaya sana mfano mzuri ni jimbo la kinondoni ambalo tunaamini ndo ngome yetu, tumepata kura 1943 kutoka kura 70500 mwaka 2010 ni dhahiri jamani wanachama hawatutaki, na mahakamani sioni tutatokea wapi nimekwiteni tupeane ushauri tufanyeje?

Alimalizia Lipumba ndipo akasimma kibaraka khalifa akasema mimi pia nakubali hili yetu ni mbaya mana tulitakiwa sisi tunaotoka Zanzibar tufanye kazi zanzibar lakini hatuthubutu hata kulikaribia tawi lolote la CUF sote tumejazana Dar nako pia hatutakiwi, mimi naona bora tukubali makosa tuombe radhi viongozi halali na wanachama lakini kwanza anza wewe lipumba ndipo lipumba akampigia simu mkurugenzi mmoja ambae inaaminika ni miongoni mwa vijana wanaoaminika sana katika CUF.

Lipumba akaanza kuomba radhi nakubali nimekosa nimeivuruga cuf, naomba jamani mnisamehe sina shida tena ya uenyekiti hewa nataka heshma yangu tu irudi kama zamani, mwisho alamalizia niombee kwa maalim Seif tukutane yalopita yamepita, baada ya kumalizana na mkurugenzi huyo lipumba akampigia kuongozi mmoja mstaafu aliewahi kushika nyadhifa za juu katika CUF hapo lipumba alishindwa kujizuiya na akalia akasema naomba mnisamehe, tamamaaa imeniponza kimekua kituko katika jamiii, jamani nisameheni aliishia hivo yule mstaafu akakata simu.

Sisi tunawambia viongozi wetu sisi wanachama wa CUF hatuna suluhu na Lipumba, kama mtamsamehe nyinyi kibinafsi sio kichama, wanachama tutamalizana nae mahakamani.

HATUNA SULUHU NA WASALITI,
 
Mtunzi anajifunza kutunga hadithi au ni mbobevu? Inaweza ikawa ni habari ila imekuja ki vigano na ngano na majigambo.... Hadithi.
 
Njia rahisi.
Afute kesi kwa kukubali makosa
Atoke hadharani kusema mimi sio mwenyekiti halali na amwandikie Mutungi kuwa
Akubali nilitumiwa
Basi cuf kitasimama na yeye heshma yake itarudi
 
Lipumba anataka heshima yake irudi
 
Njia rahisi.
Afute kesi kwa kukubali makosa
Atoke hadharani kusema mimi sio mwenyekiti halali na amwandikie Mutungi kuwa
Akubali nilitumiwa
Basi cuf kitasimama na yeye heshma yake itarudi
hakika!
 
Lete vitu vya uhakika katika hili jukwaa ili tujadili mambo kwa waledi. Tuache mambo ya kitoto. Hata chanzo cha habari tu hakuna. Na ndio maana kuna wakati wapinzani wanaonekana kuwa wajinga kumbe sio kila mtu yupo hivyo.
 
Madhara ya kula Mingwee ndiyo haya. Mara unaota upo na Boyance, mara upo na Jay Dee. Leo umeota Lipumba anaomba radhi, kesho utaota Maalim amekununulia daraja la Manzese!!
 
Back
Top Bottom