Halikakagwila
Member
- Mar 8, 2018
- 7
- 4
Kaka, alishawishi wenzake waungane katika uchaguzi mkuu wa 2015 kwa jina la UKAWA, wakiwa wamemuacha nje ya ulingo mwanzilishi wa UKAWA, Marehemu Mchungaji Mtikila. Mkakati ukaonekana unafaa.
Hatua ya kuachiana kiti ilianza, Lipumba akataka yeye awe mgombea wa Urais. Akaulizwa maswali mawili tu, atoe sababu za kwanini apewe yeye na sio mwingine, alipomaliza kujibu swali la kwanza tu akapewa la pili, je unaresource za kufanya kampeni nchi nzima. Mzee wa watu akawa mkiwa. HAPA MAMBO YALIKUWA HAYAJAIVA.
Wakasema twendeni Colloseum kwenye kikao tukatangaze jina la mgombea wetu wa UKAWA. Wengi walimtegemea Dr. Slaa kuwa mteule. Lakini ghafla Kaka (MBOWE) akasema tunakwenda kutangaza chama kitachotoa mgombea URAIS na sio jina. Kikao hakikufanyika maana kuna mwenyekiti mwenza hakutokea.
CUF Zanzibar wakamtuhumu Prof. Lipumba kutaka kuuza Chama, ikabidi aende kujieleza kwenye Baraza Kuu la Chama. Baada ya majadiliano basi Baraza Kuu - CUF likatoa baraka. UKAWA akatangaza Chama kitachotoa mgombea na sio jina la mgombea. DHUMUNI LA KUIFIFISHA CUF ambao ndio ulikuwa mkakati mkuu wa CHADEMA ukaanza kuzaa matunda.
Majadilioano yaliendelea ili CUF wamlete mgombea mweza ambaye atahama CUF na kujiunga na CHADEMA ili apitishwe na TUME ya UCHAGUZI. CUF wakafanya hayo wakiamini eti mwanachama huyo mpya wa CHADEMA aliyehama CUF atakwenda kupigania maslahi ya CUF baada ya kushinda Uchaguzi.
Mara baada ya mchakato wa ndani wa CCM kumpata mgombea wake wa URAIS kukamilika, mambo yakabadilika kwa haraka ndani ya UKAWA. Prof. Lipumba akiwa bado anapigania maslahi ya CUF ndani ya UKAWA na hasa juu ya mgawanjo wa Kata na majimbo, akaonekana anapinga mambo mengi yasiende. Pasipo kujua kwamba Kaka, ameanza mazungumzo ya siri na mgombea mwingine toka CCM. Alipopokelewa tu, Dr. Slaa na Prof. Lipumba walishikwa na butwaa kiasi lakini kwa kuwa walikuwa bado wanaimani na viongozi wao wengine yaani MBOWE na Maalim Seif, wakabakia kuwa wapole na wavumilivu.
Ghafla gia ikabadilishwa hewani na Mbowe kumtangaza Mh. LOWASSA kuwa mgombea wa kiti cha Urais. Na haya yalitokea baada ya Dr. Slaa na Prof. Lipumba kuachwa nje ya mjadala ambao ulifanywa na Mbowe, Maalif Seif kwa upande wa UKAWA na LOWASSA na kundi lake la wataalam kama wageni wapya. Hawa wawili wakaona wameachwa, Prof. LIPUMBA akajiondoa kuwa Mwenyekiti wa Chama na Dr. Slaa akajivua uongozi na uanachama wa CHADEMA.
Maalif Seif aliahidiwa kwamba ataupata urais wa Zanzibar kwa namana yoyote ile kwa maana LOWASSA alikuwa anategemea kushinda, hapa Maalif Seif akaona Lipumba sio chochote kwake kwa kuwa anakwenda kuwa Rais wa visiwani. Mbowe akajua yeye ndiye atakayekuwa Waziri Mkuu, nani tena mwingine wa kumtisha, akamuacha Dr. Slaa achague yeye mwenyewe kusuka ama kunyoa.
Ikumbukwe wakati huu wote, nguvu ya Mbatia wa mwenyekiti wa NLD (sasa marehemu) haikuweza kuonekana, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi macho yalikuwa Vunjo kwenye Ubunge akifikiria kupewa uwaziri. Mwenyekiti NLD macho yalikuwa Kusini akitegemea kupata Ubunge pengine uwaziri baadaye.
Katika matukio kama haya, nani hapa sio msaliti na ni nani hapa ndani ya UKAWA hajasalitiwa? Ikumbukwe lengo kuu la MBOWE lilikuwa ni kukidhoofisha CUF na vyama vingine vyote vya upinzani, lengo ambalo leo liko wazi na tunayaona yanayoendelea. Maalim leo yupo wapi? Lowassa yupo wapi? Haji Duni alisharudi CUF au bado?
"Siasa ni sayansi ... Dr. W.P. Slaa, 2015"