Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba: Nichagueni Oktoba 28 niwe Rais nisimamie elimu bora na matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano

CUF Habari

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2019
Posts
239
Reaction score
234

NICHAGUENI OKTOBA 28, NIWE RAIS NISIMAMIA ELIMU BORA NA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO "PROF.LIPUMBA"

KWIMBA, MWANZA

Serikali ya umoja wa kitaifa chini ya CUF itahakikisha kuwa watoto wote wa Tanzania wanakuwa na haki ya kupata elimu bora ya msingi, elimu ya sekondari na elimu ya juu. Kila raia atahimizwa kujiendeleza kielimu hasa kwa kutumia vizuri teknolojia ya habari na mawasiliano.

Serikali ya umoja wa kitaifa itakayoundwa na CUF itatoa kipaumbele maalum katika kuwaendeleza kielimu wasichana na kujenga misingi imara ya kuendeleza elimu za hisabati, sayansi na teknolojia.

Serikali ya umoja wa kitaifa chini ya CUF itahakikisha kwamba ifikapo 2025 asilimia 50 ya Shule za Umma nchini zinakuwa na uwezo wa Kufundisha wanafunzi wake kwa njia ya TEHAMA na asilimia 100 ifikapo 2028.

Hili litawezesha wanafunzi wengi kuendelea na masomo hata pale shule zitakapofungwa kwa dharura kama tulivyojifunza kupitia janga la CORONA.
 
Mungu mlinde John Pombe Magufuli, Lissu, Mbowe, Lipumba, Zitto, Membe, Maalim Seif, Hussein Mwinyi na wanasiasa wote waandamizi hapa Tanzania.

Tunahitaji siasa safi ili taifa letu lisonge mbele.
 
Safi maalim, Wewe sio msaliti wa Nchi
 
Mungu mlinde J.P Magufuli, Lissu, Mbowe, Lipumba, Zitto, Membe na wanasiasa wote waandamizi hapa Tanzania.
Mzee hilo koti unakojificha lina chawa kunguni viroboto na funza jitahidi ulivue lasivo tunakupoteza
Karibu Denmark tule maisha
 
Ni bora nizikwe hai kuliko kumpigia kura msaliti wa Nchi lissu

Ni bora nikae nyumbani nisipige kura kuliko kufanya dhambi ya kumpigia kura lissu

Ee Mungu niondolee hii nuksi
Kura zote kwa TUNDU LISSU ...wote nyie najua mtampa kura ..posho za elfu saba zinawasumbua tu ila najua kura zote za ndio kwa LISSU...furaha na tumaini la mamilioni ya watanzania karibia milioni 50
 
Safi maalim Wewe sio msaliti wa Nchi
Watanzania wanataka uhuru na haki ndani ya nchi yao. Watanzania hawataki kuonewa na kunyanyaswa na kutukanwa ndani ya nchi yao. Ndiyo maana kipindi cha miaka 5 ya Meko amejisifu kuwa kafanya maendeleo sana, lakini why this REJECTION ? Sasa hivi haongelei tena madaraja na madege
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…