Mkuu nakubalina na wewe 100%, ila nimegunduwa kuna watu wanakuwa na nongwa wakiona wagombea wengine wanajadiliwa, hebu angalia jukwaa la siasa lina thread ngapi anajadiliwa Dr. Slaa, tokea ugombea wake mpaka mambo yake ya siri. Leo katokea mtu, tena mgeni wa jukwaa, kwa mtazamo wake anaona Prof. Lipumba anafaa kuwa rais kwa jinsi alivyomsoma sera zake (raia mwema), watu hawataki, hii ndiyo inaniudhi binafsi na siipendi kuona hapa JF. Kama mtu lazima anataka ajadiliwe Dr. Slaa tu si thread zake zipo tele na asome tu lazima aje hapa kuharibu thread za watu?
Mkuu,
Hapa utakuwa huwatendei haki wana JF. Kama watu wawili au watatu hawataki kitu, huwezi kusema kuwa jukwaa zima halitaki kitu.
Kinachoendelea hapa ni kuwa, Dr Slaa anapendwa na wengi kwa jinsi anavyoibana serikali ya kifisadi ya Kikwete bungeni. Wengi wanaona michango yake na wengi wameamua kumuunga mkono. Thread zinaanza hapa kwa vile watu wanapenda anachofanya.
Wengine hapa ni wanaccm ambao hawana chochote cha kuongelea dhidi ya Slaa bali mambo yake binafsi. Kwa vile hili ni jukwaa huru, huwezi kuwazuia wasiongee hayo mambo.
Kwani unataka mtu kama mimi nianze kuongelea habari za Lipumba wakati sioni kama ni the right candidate katika uchaguzi wa mwaka huu?