Elections 2010 Prof. Lipumba: Tanzania kwanza vyama baadaye

Elections 2010 Prof. Lipumba: Tanzania kwanza vyama baadaye

Mkuu nakubalina na wewe 100%, ila nimegunduwa kuna watu wanakuwa na nongwa wakiona wagombea wengine wanajadiliwa, hebu angalia jukwaa la siasa lina thread ngapi anajadiliwa Dr. Slaa, tokea ugombea wake mpaka mambo yake ya siri. Leo katokea mtu, tena mgeni wa jukwaa, kwa mtazamo wake anaona Prof. Lipumba anafaa kuwa rais kwa jinsi alivyomsoma sera zake (raia mwema), watu hawataki, hii ndiyo inaniudhi binafsi na siipendi kuona hapa JF. Kama mtu lazima anataka ajadiliwe Dr. Slaa tu si thread zake zipo tele na asome tu lazima aje hapa kuharibu thread za watu?

Mkuu,

Hapa utakuwa huwatendei haki wana JF. Kama watu wawili au watatu hawataki kitu, huwezi kusema kuwa jukwaa zima halitaki kitu.

Kinachoendelea hapa ni kuwa, Dr Slaa anapendwa na wengi kwa jinsi anavyoibana serikali ya kifisadi ya Kikwete bungeni. Wengi wanaona michango yake na wengi wameamua kumuunga mkono. Thread zinaanza hapa kwa vile watu wanapenda anachofanya.

Wengine hapa ni wanaccm ambao hawana chochote cha kuongelea dhidi ya Slaa bali mambo yake binafsi. Kwa vile hili ni jukwaa huru, huwezi kuwazuia wasiongee hayo mambo.

Kwani unataka mtu kama mimi nianze kuongelea habari za Lipumba wakati sioni kama ni the right candidate katika uchaguzi wa mwaka huu?
 
karibu sana jamvini.naomba nikuulize swali moja tu. Unamjua DR .Slaa?
Sasa mada ni Prof. Lipumba huyu anakujaje na habari za Dr. Slaa?

Mkuu,

Hapa utakuwa huwatendei haki wana JF. Kama watu wawili au watatu hawataki kitu, huwezi kusema kuwa jukwaa zima halitaki kitu.

Kinachoendelea hapa ni kuwa, Dr Slaa anapendwa na wengi kwa jinsi anavyoibana serikali ya kifisadi ya Kikwete bungeni. Wengi wanaona michango yake na wengi wameamua kumuunga mkono. Thread zinaanza hapa kwa vile watu wanapenda anachofanya.

Wengine hapa ni wanaccm ambao hawana chochote cha kuongelea dhidi ya Slaa bali mambo yake binafsi. Kwa vile hili ni jukwaa huru, huwezi kuwazuia wasiongee hayo mambo.

Kwani unataka mtu kama mimi nianze kuongelea habari za Lipumba wakati sioni kama ni the right candidate katika uchaguzi wa mwaka huu?
Mkuu naona unanikuu vibaya nilitangulia kusema "kuna watu" na kama mtu hataki kuongea habari za Prof. Lipumba halazimishwi ila asiharibu mazungumzo ya watu ndiyo kinachogombwa hapa, hebu wangalie Nyani hapo juu kwani kalazimishwa achangie...au kaambiwa lazima ukiingia humu umzungumze Dr. Slaa tu...if he is wrong candidate to you, it's o.k then bt do'nt impart it to everybody!
 
Sasa mada ni Prof. Lipumba huyu anakujaje na habari za Dr. Slaa?

Mkuu naona unanikuu vibaya nilitangulia kusema "kuna watu" na kama mtu hataki kuongea habari za Prof. Lipumba halazimishwi ila asiharibu mazungumzo ya watu ndiyo kinachogombwa hapa, hebu wangalie Nyani hapo juu kwani kalazimishwa achangie...au kaambiwa lazima ukiingia humu umzungumze Dr. Slaa tu...if he is wrong candidate to you, it's o.k then bt do'nt impart it to everybody!

Huwezi kucontrol kila kitu wanachoandika hapa mkuu. Hata threads za Slaa wanaccm (au wale wanaopretend kuwa wanaCUF) huwa wanaleta mambo kibao tu. Usicheze na side shows endeleza mada.

Swali kwako, kama CHADEMA waliwaunga CUF mwaka 2000, je CUF wataunga chama chochote kile kwenye chaguzi zijazo?
 
Nilimesoma hii Lipumba kaongea vema ila tatizo utekelezaji wake utakuwa mgumu kwa kuwa hana kura za kutosha kumpatia ushindi sopia hutuna historia yake ya utekelezaji mambo zaidi ya kuwa mshauri wa mwinyi.
So ni vema akawambia washabiki wake kuwa waache ushabiki wampe Slaa kura.
Lipumba anafaa kuwa waziri wa uchumi na fedha .
 
maandishi ya herufi kubwa na font kubwa hayatafanya hoja zako kuwa bora zaidi. Kwenye forums kama hizi, ukiandika kwa herufi kubwa hivyo ina maana kwamba unashout... Je kuna sababu yoyote ya wewe kufanya hivyo.

Btw- hasira zote hizi ni za nini kama mna hakika ya ushindi?

huna hoja yoyote, huna la kuongea umebaki kulaumu na kukosoa hata visivyotakiwa kukosolewa, nimeamua kukuandikia kwa herufi kubwa uli uone vizuri na huu ni uamuzi wangu wa kuchaguwa maandishi ninayotaka au jamii forum itaniwekea masharti ya kuchaguwa herufi? Hii kali!!! Nenda zako kalale na ungojee jibu lako tarehe 31.10.2010 tutakapo chukua na kuweka waaaaaaaaa,,,,,

good night!!!
 
Good night
 
Wakuu,
Sioni tatizo katika kujadili hoja hii jinsi ilivyoletwa. Kwa mtazamo wangu mwandishi wa hiyo makala ametoa yale aliyoyashuhudia kwa Prof Lipumba. N vema nasi tukamjadili Prof Lipumba kama mgombea na sera zake. Wengine nao tuwajadili hivyo hivyo na kwa kufanya hivyo mwisho wa siku tutafahamu nani anatufaa.

Nimehidhuria baadhi ya mikutano ya Lipumba, ukimsikiliza utakubaliana na mwandishi kuwa hujadili mambo mazito. Tatizo nilionalo, mathalani kwa Mbeya, CUF haijakubalika bado na inachangiwa na wawakilishi wao kule. Wengi wa viongozi wa CUF ni wasaanii tu, na mfano ni kampeni hizo za karibuni Lipumba akiwa Mbeya, hakukuwa na utangazaji wa kutosha wa ujio namikutano yake.

Tukiacha ushabiki wa vyama, Lipumba anatoa hoja nzito na za kisomi zaidi lakini kwa mikoa ya kama Mbeya, hawajamkubali.
 
Mie si mwananchama wa chama chochote but kama Lipumba engekubaliana na kauli mbiu hiyo ya chama chake na kuangalia upepo wa uchaguzi hivi sasa, naamini angekuwa hero kama angeamua kumuunga mkono Dr. Slaa katika uchaguzi huu. Hata hivyo bado hajachelewa, anaweza kufanya hivyo huku wakipigiana kampeni katika nafasi za ubunge.
 
kwani uongo?

BTW - ule mchongo aliopewa na ccm kule UN (kama sikosei) umeishia wapi? Talk about kununuliwa na ccm hadharani, kuna thread ilikuwa hapa JF miezi kibao iliyopita, ngoja niitafute.

Huku ndio kumpongeza na Kumuunga mkono ulikodai ktk post ya Awali?

Ndio Uongo !!! eti hadharani...!!! ama kweli Mwenzetu "Chongo"

Hio link ya JF ya Kununuliwa ni washabiki wasioitakia mema Nchi Hii...!!! Hivi unaweza pewa mchongo na CCM UN? kwani UN jina la Prof ni geni kwao?....labda ki-protocol kwa nafasi yake kulihitajika baraka za serikali, hilo ni jambo la kawaida kwa post yoyote ya Kimataifa ambapo vettings zinafanyika...Leo hii ukiomba Kazi Ubalozi wa UK, utafanyiwa vettings na hadi watu wa Home Affairs/Foreign Affairs wataulizwa na kutakiwa kusubmit barua ya kuonesha wewe huna crimes zozote. Sembuse International Level...huwezi ukasema huo mchongo kapewa na watu wa CCM...!!!
 
Huwezi kucontrol kila kitu wanachoandika hapa mkuu. Hata threads za Slaa wanaccm (au wale wanaopretend kuwa wanaCUF) huwa wanaleta mambo kibao tu. Usicheze na side shows endeleza mada.

Swali kwako, kama CHADEMA waliwaunga CUF mwaka 2000, je CUF wataunga chama chochote kile kwenye chaguzi zijazo?

Wakikosa Mgombea watawaunga Mkono....!!! kama walivyofanya Chadema mwaka 2000.
 
Wakuu,
Sioni tatizo katika kujadili hoja hii jinsi ilivyoletwa. Kwa mtazamo wangu mwandishi wa hiyo makala ametoa yale aliyoyashuhudia kwa Prof Lipumba. N vema nasi tukamjadili Prof Lipumba kama mgombea na sera zake. Wengine nao tuwajadili hivyo hivyo na kwa kufanya hivyo mwisho wa siku tutafahamu nani anatufaa.

Nimehidhuria baadhi ya mikutano ya Lipumba, ukimsikiliza utakubaliana na mwandishi kuwa hujadili mambo mazito. Tatizo nilionalo, mathalani kwa Mbeya, CUF haijakubalika bado na inachangiwa na wawakilishi wao kule. Wengi wa viongozi wa CUF ni wasaanii tu, na mfano ni kampeni hizo za karibuni Lipumba akiwa Mbeya, hakukuwa na utangazaji wa kutosha wa ujio namikutano yake.

Tukiacha ushabiki wa vyama, Lipumba anatoa hoja nzito na za kisomi zaidi lakini kwa mikoa ya kama Mbeya, hawajamkubali.

....Tatizo la Organization linawasumbua sana Vyama vya Upinzani,
 
Junius

Umeongea point katika hii thread.. nakuunga mkono kwa yote uliyosema
 
Nilimesoma hii Lipumba kaongea vema ila tatizo utekelezaji wake utakuwa mgumu kwa kuwa hana kura za kutosha kumpatia ushindi sopia hutuna historia yake ya utekelezaji mambo zaidi ya kuwa mshauri wa mwinyi.
So ni vema akawambia washabiki wake kuwa waache ushabiki wampe Slaa kura.
Lipumba anafaa kuwa waziri wa uchumi na fedha .

Ndugu wananchi wenzangu, nawaomba tuongee hoja, na tuwachambue wagombea wetu kwa hoja wanazotoa na vyama vyao. Mimi nionavyo:
Prof Ibrahim Lipumba (l1) na Dr Wilbroad Slaa (s1)
1. Wote ni wasomi waliokubuhu
2. Wote ni wanagombea katika nafasi ya uongozi wa taifa letu

Sifa zao
Lipumba:
amewahi kuwa mshauri wa rais AH Mwinyi (l2)
Ni M/Kiti wa Taifa CUF (l3)
Anagombea uraisi kwa mara ya tatu (l4)
Ni mwislam (Ahamadiya?) (l5)

Slaa:
Amewahi kuwa mbunge wa Karatu kwa miaka 15 (s2)
Ni Katibu Mkuu wa CHADEMA (s3)
Anagomea urais kwa mara ya kwanza (s4)
Ni mkristu (Catholic) (s5)

Tofauti zao
Prof I. Lipumba anasimama kwa ticket ya CUF kwa mara ya tatu (l6)
Dr W. Slaa anasimama kwa ticket ya CHADEMA kwa mara ya kwanza (s6)

Dr Slaa ana historia ya kuonesha msimamo usioyumba kwa kutaja orodha ya mafisadi bila kutetereka (s7).
Dr Slaa amekuwa na historia ya kuibua kashafa nyingi dhidi ya serikali ambazo mara zote zimethibitika kuwa ni za kweli (s8).

Kwasababu hiyo umaarufu wa wagombea hao wawili unatokana na sifa zao pamoja na sifa za vyama vyao. Kuhusu vyama hivyo kuna historia tofauti nyuma ya kila chama. Kuanzishwa kwa vyama hivyo kuna mambo yaliyofichika yanayofanya watu wengi kushindwa kuzingatia sifa za wagombea wa vyama hivyo. Kwa mfano watu wanamheshimu Prof Lipumba kwa usomi wake na kwa hoja zake anazotoa majukwaa ni. Lakini watu siku zote wamekuwa wakikitazama chama cha Lipumba kwa wasiwasi kuwa ni chama cha Hamad zaidi kuliko Lipumba, nay a kwamba kipo ili kutetea maslahi ya wapemba. Hivyo watu wanabaki kumpenda Professor na kumtamani lakini bila ya kumshabikia. Hiki ndio kinachomharibia, vinginevyo mambo yake yanaeleweka vizuri.

Chama cha Dr Slaa pia kilikuwa kikitizamwa kama chama cha mwanzilishi wake aliyetofautiana na Nyerere hivyo kulazimika kujiuzuru uongozi wa nchi. Mtizamo huu umekisumbua sana chama cha chadema na ndio maana Mbowe alipogombea mara ya kwanza ni kama wa-Tz walimkataa na hakupata kura nyingi kumpita Prof Lipumba.

Lakini, tofauti na safari hii Dr Slaa, anaonekana kama mwanamapinduzi, mzalendo na anayeumwa na nchi yake kwa dhati ya moyo kabisa. Hilo limejengeka kutokana na mtiririko wa mambo mbalimbali aliyopata kuyafanya huko nyuma. Kwasababu ya ufisadi mkubwa uliofanyika nchini chini ya CCM, Dr Slaa anaonekana kama ndiye dawa ya matatizo hayo. Wengi tunamshabikia kwasababu hiyo.
 
Huku ndio kumpongeza na Kumuunga mkono ulikodai ktk post ya Awali?

Ndio Uongo !!! eti hadharani...!!! ama kweli Mwenzetu "Chongo"

Sikusema kuwa namuunga mkono kwa wakati huu, nilisema namkubali BUT hiyo haipelekei kuunga mkono katika uchaguzi huu. Mwaka 2000 wengi tulimuunga mkono Prof Lipumba, mbona CUF wasifanye hivyo kwa Dr Slaa mwaka huu?

Hio link ya JF ya Kununuliwa ni washabiki wasioitakia mema Nchi Hii...!!! Hivi unaweza pewa mchongo na CCM UN? kwani UN jina la Prof ni geni kwao?....labda ki-protocol kwa nafasi yake kulihitajika baraka za serikali, hilo ni jambo la kawaida kwa post yoyote ya Kimataifa ambapo vettings zinafanyika...Leo hii ukiomba Kazi Ubalozi wa UK, utafanyiwa vettings na hadi watu wa Home Affairs/Foreign Affairs wataulizwa na kutakiwa kusubmit barua ya kuonesha wewe huna crimes zozote. Sembuse International Level...huwezi ukasema huo mchongo kapewa na watu wa CCM...!!!

Hicho ndicho kilifanyika .... wazee wa nyeti (wengine na sio mimi) wakamwaga mboga hapa kuwa huu ni moja ya makubaliano ya ushirikiano kati ya CUF na CCM. Nadhani uchaguzi wa mwaka huu umethibitisha wazi - CUF wanawaandama sana CHADEMA kuliko wanavyowaaandama CCM.
 
Hakuna kisichowezekana katika siasa Mkuu!

Vipi kuhusu mwaka huu?
BTW - mbona CUF wanapondea sana CHADEMA kuliko CCM? au ndio moja ya makubaliano ya viongozi wa juu wa vyama hivi (Kikwete na Lipumba)?
 
safe_image.php
 
Naona CUF na CHADEMA wote ni mateka

sasa suala la mfu kumzika mfu mwenziwe hio ni juu yenu
\

jivueni nguo tuzidi kukufahamuni
 
Nafikiri ni muda muafaka vyama pinzani viweke kando tofauti zao ili kuweza kutunusuru watanzania na hali ya maisha tuliyonayo. Natoa wito kwa uongozi wa CHADEMA na CUF kukaa pamoja ili kuongeza nguvu ya kuweza kushinda uchaguzi huu. Kwa sababu Dr.Slaa, Prof.Lipumba pamoja na vyama vyao wanakubaliana kuwa:
1.Hali ya maisha ya watanzania walio wengi ni duni pamoja na kuwa tumezungukwa na rasilimali nyingi.
2. CCM imeshindwa kuleta ufumbuzi wa matatizo tuliyonayo
3. Kunahitajika fresh thinking katika kupata fumbuzi za matatizo yetu.

Basi katika kuelewa hayo na ikiwa kweli wanasiasa hawa wana NIA ya kweli na UCHUNGU wa kutuongoza katika kututoa hapa tulipo, basi maslahi ya taifa yawekwe mbele kabla ya maslahi ya vyama vyao au wagombea binafsi.

Ikiwa mataifa makubwa kama Uingereza, Ujerumani na Australia wanakaa pamoja na kuwa na memorandum ya kushirikiana katika serikali za umoja (coalition govt), ni muda muafaka sasa Dr.Slaa na Prof.Lipumba kuungana katika kuleta mabadiliko tunayoyataka.

Change is what we need no doubt about that, lakini ili 'changes' zifanikiwe national interests should surpass individual and/or party's interests.
 
Back
Top Bottom