Hapo ndipo wakenya wataanza kuziona rangi zote za pichu za mwanamke kama sisi tz .....lazima walie na kusaga meno
Raila leads Africa and perhaps the planet with six foiled assassination attempts!
Intelijensia yake ni kali kuliko ya State.
Mnajuwa, kuna historia ya ukoo wa Jaramogi Oginga ambayo haijawa documented anywhere lakini inafanyakazi effectively katika mafanikio ya kisiasa ya kizazi chake.
Wakati Tom Mboya anashauriwa na Jaramogi kwamba asiende Nairobi aenda Kisumu baada ya ziara ya nje, kwamba Jaramogi ameona kuna damu inamwagika nchini na roho ya Mboya inatafutwa, alikaidi ushauri na kesho yake 5 Julai 1969 Jomo akatangazia dunia kuwa bendera za Kenya zipepee nusu mlingoti, Tom Mboya hatunaye! Mwili wake umeokotwa Moi Avenue mkabala na mtaa busy wa Victoria ukiwa na majeraha ya risasi.
Wajaluo wakaliamsha kumlipiza Jomo. Ndani ya masaa 10 (hakukuwa na mitandao jamii enzi hizo bali redio ya VOK sasa KBC tu) vurugu zikasambaa nchi nzima yenye ukubwa wa kilomita za mraba 580,367.
Jaramogi alikuwa na kipawa cha kuona mbele kwa mida mifupi na mirefu, soma hata kile kitabu chake cha Not Yet Uhuru utakubaliana na ukweli huu kwamba he was a fore-teller, ndiyo maana hata akina Nyerere walimtumiaga sana kwenye PAN AFRICANISM na PAFMECA nk. Alikuwa kifaa.
Mimi nafuatiliaga sana historia yao kwa sababu wanani-inspire, alafu ni historia tamu, pia ni historia ya watu wenye mafanikio.
Jaramogi mwenyewe wakati anaenda Lancaster kudai uhuru, alipata habari za kijasusi sijui kwa njia ya mizimu/roho za utambuzi au nini, kwamba Waingereza wamepanga assassination yake kwa njia ya sumu kwenye chakula (dhifa) (kwa sababu tayari walijuwa kuwa Jomo lazima tu atafia gerezani Kapenguria West-Pokot, hivyo wamalizane na Jaramogi pia ili waendelee kutawala Kenya).
Kwa siri hiyo iliyovuja, Jaramogi alibeba chakula cha asili ya Wajaluo na Wakikuyu cha kutosha delegation yake yote kwa siku zote za mkutano, Waingereza wakaduwaa.