Actual building construction cost unategemea material specifications na quality and cost of labor.
Bei ya beer Tanzania unategemea brand, ujazo, na mahali ulipo. Ukiwa Buguruni, Airport, jeshini, Kilimanjaro hotel nk bei ni tofauti.
Kwahiyo tusichukulie kuwa cost per unit in area kama ni standard. Tutakosea sana!
Quality na bei za materials na labor haziwezi kuwa sawa kila siku kila mahali.
Mifano:
Bati. Zipo za material, size, gauge na bei tofauti. Vivyohivyo na mbao, misumari, nondo, mchnga, maji, kokoto, cement, rangi, tiles, wire za umeme, bomba, nk.
Pili mafundi na vibarua wako wenye ujuzi na uzoefu tofauti kwahiyo hulipwa kutegemea na uwezo wa mwajiri, sheria zenu za kazi na mshahara wa kima cha chini; narudia: SHERIA ZENU ZA KAZI NA KIMA CHA CHINI CHA MISHAHARA.
Tatu mahali linapojengwa hilo jengo: mjini, kijijini, juu au chini ya maji au barafu eg bandari nk. Halafu majira gani! Kiangazi, masika, kwa Tanzania unaweza kuambiwa ghafla ujenge usiku na mchana!
Nne muda na mazingira yasiyotabirika: Mfano mzuri ni hivi sasa tuko mwanzo wa mwaka tunasubiri Bajeti ya Serikali ya 2020-21. Nani anajua kama gharama za maisha zitapanda au kushuka?
Mjuwe kwamba mkipandisha kodi tu, na bei za vitu zitapanda. Sukari ikipanda bei, chai itapanda bei, maandazi na vitumbua vitapanda bei, la sivyo vitakuwa vidogo zaidi. Mikate hali kadhalika! Kwasababu bei za mchele, mafuta na mkaa vyote vitapanda bei! Dawa hospitalini zitapanda bei, gharama za usafiri, na UJENZI zitapanda bei!
Lakini haiishii hapo. Majengo yakijengwa chini ya kiwango yanasababisha gharama za ujenzi kupanda. Kwasababu yatalazimika kurudiwa ujenzi au kukarabatiwa kwa gharama za ziada. Hasara katika ujenzi maana yake ni gharama kwa mlipaji (Serikali) ambaye ni sisi wananchi.
Kwahiyo MH Waziri kama una uchungu na wananchi anzia bungeni kwenye Bajeti ya Serikali. Punguzeni matumizi ya Serikali kwenye utawala bila kuzingatia sheria na taratibu za tenda na sheria za manunuzi.
Mkiendelea na utaratibu wa miradi ya papo kwa papo mnakaribisha hayo mnayokemea. Kwasababu kama wewe Mkuu wa mkoa au Waziri ukitoa amri "nataka darasa lijengwe hapa kwa wiki mbili kwa shillings kadhaa, watu watajenga watakupakia rangi nzuri utalizindua kwa vigelegele na mapicha! Baada ya mwaka jengo linameguka vipande vipande! Utalaumu wataalamu?
Sent using
Jamii Forums mobile app