Prof. Manji wa MUHAS ashinda tuzo ya mhitimu bora wa Harvard University. Rais Samia Ampongeza

Prof. Manji wa MUHAS ashinda tuzo ya mhitimu bora wa Harvard University. Rais Samia Ampongeza

MAJITA hao akina MANJI ni wengi mno na hata mimi nina mpwa wangu anaitwa MANJI.
Sasa huwa ninajiuliza,hivi SISI WAJITA tuna undugu na WAHINDI? Maana MANJI ni jina linalotumiwa sana UJITANI na lina maana ya MAJI.

Ebu muulize huyo pro aniambie kwa KIHINDI Manji humaanisha nini?
Kwa wajita hilo jina la Manji walipewa sababu wao ni vichwa maji vichwani hamna kitu
 
My Take:
Ukoo wa kina Manji sio vilaza na Kwa mara nyingine Wahindi wanaonesha jinsi gani ni vipanga kwenye sekta ya Afya na Hesabu.

Hongera Prof Karim Manji Kwa kuitangaza Tanzania na Muhimbili University
================

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amempongeza Profesa Karim Manji wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas) aliyechaguliwa kuwa miongoni mwa washindi wa tuzo ya muhitimu bora wa Chuo Kikuu cha Harvard.

Profesa Karim Manji ameokoa maisha ya watoto wengi wachanga pamoja na waliozaliwa kabla ya wakati na wenye uzito mdogo yaani ‘njiti’ katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) miaka 30 iliyopita.

Rais Samia ametoa pongezi hizo leo Jumapili, Septemba 15, 2024 kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

“Pongezi za dhati kwa Profesa Karim Manji, bingwa, mkufunzi na mtafiti katika eneo la tiba ya watoto na afya ya vijana, kwa ushindi wa tuzo ya Alumni Award of Merit kutoka Shule ya Afya ya Chuo Kikuu cha Harvard (Harvard T.H. Chan School of Public Health).”

“Kwa zaidi ya miaka 30, Profesa Manji amekuwa daktari, mkufunzi na mtumishi wa kupigiwa mfano katika Hospitali ya Taifa na Chuo Kikuu cha Afya na Tiba Shirikishi, Muhimbili. Tunajivunia kujitoa kwako kwa nchi yetu, utafiti, ushauri, utumishi na malezi yako kwa mamia ya wanafunzi ambao sasa ni madaktari katika eneo hili muhimu la afya kwa nchi yetu,” ameandika Rais Samia.


Tuzo hiyo inayotambulika kwa jina la 'Harvard T.H Chan School of Public Health Alumni Merit Award 2024' hutolewa kwa aliyewahi kuwa muhitimu wa chuo hicho mashuhuri kwa wanafunzi ‘vipanga’ duniani na aliyejitoa kwa ajili ya afya ya jamii.

Na yule mwingine yy amewahi kushinda ipi......yule anaesemaga kila kitu ni hamnaa tusile
 
2 December 2024

Joram Nkumbi akifanya mahojiano na Prof. Karim Manji kupata udani wa mchango wake katika fani ya utabibu, uhadhiri chuo kikuu na utafiti nchini Tanzania

View: https://m.youtube.com/watch?v=wMIcLwGPxdk
Prof. Karim Manji from MUHAS has made history as the first Tanzanian to win the Harvard T.H. Chan School of Public Health Alumni Merit Award 2024.
 
Back
Top Bottom