Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Profesa Shukrani Elisha Manya, ameapishwa kuwa Naibu Waziri wa Madini, baada ya Francis Kumba Ndulane kushindwa kuapa na kuteuliwa mwingine
Manya ni mbunge wa kuteuliwa aliyeapishwa masaa machache yaliyopita katika viwanja vya bunge na Spika wa Bunge. Job Ndugai
Kassim Majaliwa amuambia rais kuwa anaweza akaangaliangalia pa kumuweka Francis Ndulane
Waziri Mkuu: Profesa Manya tunamfahamu, kati ya mambo makubwa yaliyofanyika kwenye madini, yeye akiwa mtendaji wa tume amekuwa na mchango mkubwa sana, uteuzi wako ni uteuzi sahihi.
Sitaki sana kuzungumzia alilosema mheshimiwa Spika, naamini na mimi najua, eneo hili mheshimiwa Rais sio eneo la mzaha mzaha sana. Hata mimi siku ile naapa, ukitamkwa pale kuvuka mpaka hapa unatakiwa utumie nguvu kidogo. Kwa hiyo mheshimiwa Rais yaliyotokea Juzi si tu ya Lindi bali tuendelee kumuombea kijana wetu. Naamini bado unaweza ukaangalia angalia.
Katika Hotuba yake Rais Magufuli amesema tangu juzi walisema wana reserve ya kutosha
RAIS MAGUFULI: Umepata hii nafasi ya kuwa Naibu waziri wa madini, siku tulipokuwa tukiwaapisha mawaziri na manaibu waziri hapa, mheshimiwa Makamu wa Rais aliwadokeza kwamba 'Reserve' tunao wengi na ukiwa na timu nzuri na ukiwa na timu nzuri ambayo unataka ifanye kazi vizuri lazima uwe na 'Reserve' kwa hiyo nataka kuwahakikishia kwamba 'Reserve' hukuwa wewe tu, bado tuna 'Reserve' nyingine. Kwa hiyo wachezaji mliochaguliwa pamoja na wewe lazima mkachape kazi.
Tumekuchagua wewe kwenda kuwa Naibu Waziri kwa sababu wizara hii tuliona kwenye nafasi za juu inayumba proffesions kwa sababu waziri hajui madini, yeye proffesion yake ni mwalimu, katibu mkuu ni profesa lakini nafikiri amechukua mambo ya komputa hivi au statistics, kitu kama hicho.
Kwa hiyo hayana uhusiano na Copper na Red. Tumeona tukuweke wewe ukawe link nzuri kwenye wizara hii. Wewe ni profesa lakini haina maana maprofesa waliowahi kukaa wizara ya madini walifanya vizuri kwa hiyo uende na observasion hii kwa sababu tumewahi kuwa na waziri Profesa, tumewahi kuwa na katibu mkuu profesa tena wa madini, mambo hayakwenda vizuri na hili nataka niku-caution ili utakapoenda kule usije ukaangukia kwenye mtego huo ambao maprofesa wenzako waliufanya walipokuwa wizara ya madini, sitaki kukuficha.
Wakati wanaingia kina Biteko mapato yalikuwa bilioni 168 leo makusanyo mwaka huu ni bilioni 527, sasa mkiamua sekta ya madini inaweza ikatoa mchango mkubwa sana kwenye Taifa hili.