Prof. Manya aapishwa kuwa Naibu waziri wa Madini. Rais Magufuli ataka wachezaji waliochaguliwa wakachape kazi kwani ana 'Reserve' wengi

Prof. Manya aapishwa kuwa Naibu waziri wa Madini. Rais Magufuli ataka wachezaji waliochaguliwa wakachape kazi kwani ana 'Reserve' wengi

Kwani mh rais asingeweza kutengua uteuzi wake kabla ya kiapo kama kulikua na makandokando kama unavyodai .ingekua vizuri kama ungetaja hayo makandokando ambayo raisi hawezi kutengua uteuzi hadi hiyo unayodai ni FUTUHI inafanyike
Kweli JF sasa wamejaa "GRITI SINKER" yaani haujui kumuapisha mtu halafu uje kumtengua ni aibu kwa mkulu kuliko hii futuhi ya kuonyesha kwamba mwenye kosa ni Francis? Kutengeua ni kashfa kwa vyombo vya uteuzi.
 
Yes ni FUTUHI mkuu!! Hadi Katibu Kiongozi alikuwa anajua KIFUATACHO ITV....Ndio maana MEKO alionyesha ishara tu,Katibu Kiongozi akatekeleza.......Msikubali vitu kiwepesi wepesi....hiyo kitu staged.
Duh, haya bhana. Yawezekana uko ndani ya duara na unajua kinachojiri.
Chura akitoka kwenye maji ya kisimani akakuambia hayo maji ni ya moto inakubidi uamini tu mkuu.
 
Profesa Shukrani Elisha Manya, ameapishwa kuwa Naibu Waziri wa Madini, baada ya Francis Kumba Ndulane kushindwa kuapa na kuteuliwa mwingine

Manya ni mbunge wa kuteuliwa aliyeapishwa masaa machache yaliyopita katika viwanja vya bunge na Spika wa Bunge. Job Ndugai

Kassim Majaliwa amuambia rais kuwa anaweza akaangaliangalia pa kumuweka Francis Ndulane

Waziri Mkuu:
Profesa Manya tunamfahamu, kati ya mambo makubwa yaliyofanyika kwenye madini, yeye akiwa mtendaji wa tume amekuwa na mchango mkubwa sana, uteuzi wako ni uteuzi sahihi.

Sitaki sana kuzungumzia alilosema mheshimiwa Spika, naamini na mimi najua, eneo hili mheshimiwa Rais sio eneo la mzaha mzaha sana. Hata mimi siku ile naapa, ukitamkwa pale kuvuka mpaka hapa unatakiwa utumie nguvu kidogo. Kwa hiyo mheshimiwa Rais yaliyotokea Juzi si tu ya Lindi bali tuendelee kumuombea kijana wetu. Naamini bado unaweza ukaangalia angalia.

Katika Hotuba yake Rais Magufuli amesema tangu juzi walisema wana reserve ya kutosha

RAIS MAGUFULI:
Umepata hii nafasi ya kuwa Naibu waziri wa madini, siku tulipokuwa tukiwaapisha mawaziri na manaibu waziri hapa, mheshimiwa Makamu wa Rais aliwadokeza kwamba 'Reserve' tunao wengi na ukiwa na timu nzuri na ukiwa na timu nzuri ambayo unataka ifanye kazi vizuri lazima uwe na 'Reserve' kwa hiyo nataka kuwahakikishia kwamba 'Reserve' hukuwa wewe tu, bado tuna 'Reserve' nyingine. Kwa hiyo wachezaji mliochaguliwa pamoja na wewe lazima mkachape kazi.

Tumekuchagua wewe kwenda kuwa Naibu Waziri kwa sababu wizara hii tuliona kwenye nafasi za juu inayumba proffesions kwa sababu waziri hajui madini, yeye proffesion yake ni mwalimu, katibu mkuu ni profesa lakini nafikiri amechukua mambo ya komputa hivi au statistics, kitu kama hicho.

Kwa hiyo hayana uhusiano na Copper na Red. Tumeona tukuweke wewe ukawe link nzuri kwenye wizara hii. Wewe ni profesa lakini haina maana maprofesa waliowahi kukaa wizara ya madini walifanya vizuri kwa hiyo uende na observasion hii kwa sababu tumewahi kuwa na waziri Profesa, tumewahi kuwa na katibu mkuu profesa tena wa madini, mambo hayakwenda vizuri na hili nataka niku-caution ili utakapoenda kule usije ukaangukia kwenye mtego huo ambao maprofesa wenzako waliufanya walipokuwa wizara ya madini, sitaki kukuficha.

Wakati wanaingia kina Biteko mapato yalikuwa bilioni 168 leo makusanyo mwaka huu ni bilioni 527, sasa mkiamua sekta ya madini inaweza ikatoa mchango mkubwa sana kwenye Taifa hili.
Ukiniteua kazi na kuniambia nifqnye kazi, kuna reserve wengi, najiuzulu hapo hapo kuwapa nafasi reserve.

Kuniteua mimi, maana yake umeona mimi nafaa kuliko hao reserve. Sasa habari za reserve hata kabla sijaanza kazi zinakuja vipi hapo?

Haya si masimango yasiyo na sababu kazini?

Hicho ni kitisho chenye dharau.

Hizi kejeli ndiyo zinetufanya wengine tukatae kufanya kazi za kiserikali/ kisiasa.
 
Duh, haya bhana. Yawezekana uko ndani ya duara na unajua kinachojiri.
Chura akitoka kwenye maji ya kisimani akakuambia hayo maji ni ya moto inakubidi uamini tu mkuu.
Ah wapi wazee wa kujiongeza tu hawa wala hana lolote ajualo
 
Ndiyo maana kuna watu wanaamini jamaa alipigwa zongo [emoji3][emoji3]

Cc
Mshana Jr
Wabongo wanapenda sana stories hizo.

Mtu anaweza kushikwa na kihoro, kigugumizi au akawa anahitqji miwani tu, wabongo watasema yao.

Wakati wa utoto kuna siku nilishikwa kwa kufanya zali nikapelekwa lupango.

Basi mshikaji wangu mmoja akawa kaenda home kutoa taarifa.

Jamaa ana kigugumizi.Kwa uzito wa ile habari, na alivyokuwa na kihoro kwenye kuwataarifu wazazi wangu, jamaa aligonga hodi home, akafunguliwa mlango, aliganda kama dakika moja nzima hivi ameshindwa kuongea.

Ikabidi Mama amtulize amketishe chini kwanza. Baada ya hapo ndipo akawapa habari Kiranga kafanya zali kawekwa lupango huko mkiona hajarudi nyumbani leo sababu ndiyo hiyo, mfuateni kituo cha polisi.

Huyo jamaa aliyeapishwa kwa mbinde, kama ana matatizo ya macho, angetafuta miwani.

Kama ana kigugumizi, angefanya mazoezi kama kwenye ile movie "The King's Speech".

Habari za ndumba ni hadithi tu.

 
Ah wapi wazee wa kujiongeza tu hawa wala hana lolote ajualo
Ujue kukubali kudhalilika vile na kuukosa uwaziri sio mchezo.

Naamini kuna kitu hakikuwa sawa kwa Francis kisaikolojia na Meko akaamua amfanyie finishing
 
Kwani mh Rais asingeweza kutengua uteuzi wake kabla ya kiapo kama kulikua na makandokando kama unavyodai .ingekua vizuri kama ungetaja hayo makandokando ambayo raisi hawezi kutengua uteuzi hadi hiyo unayodai ni FUTUHI inafanyike

Ile ilikuwa futuhi km ya Charles mafiga matatu.
Kuingia kujibu swali akiwa pombe.
 
Back
Top Bottom