Prof. Manya aapishwa kuwa Naibu waziri wa Madini. Rais Magufuli ataka wachezaji waliochaguliwa wakachape kazi kwani ana 'Reserve' wengi

Kwani mh rais asingeweza kutengua uteuzi wake kabla ya kiapo kama kulikua na makandokando kama unavyodai .ingekua vizuri kama ungetaja hayo makandokando ambayo raisi hawezi kutengua uteuzi hadi hiyo unayodai ni FUTUHI inafanyike
Kweli JF sasa wamejaa "GRITI SINKER" yaani haujui kumuapisha mtu halafu uje kumtengua ni aibu kwa mkulu kuliko hii futuhi ya kuonyesha kwamba mwenye kosa ni Francis? Kutengeua ni kashfa kwa vyombo vya uteuzi.
 
Uwezo wa kiuongozi kwa mara nyingi huwa hautegemei werevu za darasani.
 
huyu Prof kakubali kuukabithi uprof wake mtaa wa Lumumba, ataupitia siku akistaafu.
Nimecheeka [emoji23][emoji23][emoji23] kama namuona saa anauulizia kama wameuona...mbaya kama wameupoteza sijui itakuwaje.
 
Yes ni FUTUHI mkuu!! Hadi Katibu Kiongozi alikuwa anajua KIFUATACHO ITV....Ndio maana MEKO alionyesha ishara tu,Katibu Kiongozi akatekeleza.......Msikubali vitu kiwepesi wepesi....hiyo kitu staged.
Duh, haya bhana. Yawezekana uko ndani ya duara na unajua kinachojiri.
Chura akitoka kwenye maji ya kisimani akakuambia hayo maji ni ya moto inakubidi uamini tu mkuu.
 
Ukiniteua kazi na kuniambia nifqnye kazi, kuna reserve wengi, najiuzulu hapo hapo kuwapa nafasi reserve.

Kuniteua mimi, maana yake umeona mimi nafaa kuliko hao reserve. Sasa habari za reserve hata kabla sijaanza kazi zinakuja vipi hapo?

Haya si masimango yasiyo na sababu kazini?

Hicho ni kitisho chenye dharau.

Hizi kejeli ndiyo zinetufanya wengine tukatae kufanya kazi za kiserikali/ kisiasa.
 
Duh, haya bhana. Yawezekana uko ndani ya duara na unajua kinachojiri.
Chura akitoka kwenye maji ya kisimani akakuambia hayo maji ni ya moto inakubidi uamini tu mkuu.
Ah wapi wazee wa kujiongeza tu hawa wala hana lolote ajualo
 
Ndiyo maana kuna watu wanaamini jamaa alipigwa zongo [emoji3][emoji3]

Cc
Mshana Jr
Wabongo wanapenda sana stories hizo.

Mtu anaweza kushikwa na kihoro, kigugumizi au akawa anahitqji miwani tu, wabongo watasema yao.

Wakati wa utoto kuna siku nilishikwa kwa kufanya zali nikapelekwa lupango.

Basi mshikaji wangu mmoja akawa kaenda home kutoa taarifa.

Jamaa ana kigugumizi.Kwa uzito wa ile habari, na alivyokuwa na kihoro kwenye kuwataarifu wazazi wangu, jamaa aligonga hodi home, akafunguliwa mlango, aliganda kama dakika moja nzima hivi ameshindwa kuongea.

Ikabidi Mama amtulize amketishe chini kwanza. Baada ya hapo ndipo akawapa habari Kiranga kafanya zali kawekwa lupango huko mkiona hajarudi nyumbani leo sababu ndiyo hiyo, mfuateni kituo cha polisi.

Huyo jamaa aliyeapishwa kwa mbinde, kama ana matatizo ya macho, angetafuta miwani.

Kama ana kigugumizi, angefanya mazoezi kama kwenye ile movie "The King's Speech".

Habari za ndumba ni hadithi tu.

 
Ah wapi wazee wa kujiongeza tu hawa wala hana lolote ajualo
Ujue kukubali kudhalilika vile na kuukosa uwaziri sio mchezo.

Naamini kuna kitu hakikuwa sawa kwa Francis kisaikolojia na Meko akaamua amfanyie finishing
 
Kwani mh Rais asingeweza kutengua uteuzi wake kabla ya kiapo kama kulikua na makandokando kama unavyodai .ingekua vizuri kama ungetaja hayo makandokando ambayo raisi hawezi kutengua uteuzi hadi hiyo unayodai ni FUTUHI inafanyike

Ile ilikuwa futuhi km ya Charles mafiga matatu.
Kuingia kujibu swali akiwa pombe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…