Prof. Mbarawa arudi kuwa Waziri wa Ujenzi, tutegemee nini katika sekta hii?

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,207
Reaction score
13,839
Ama kweli dunia tambara bovu.

Prof Makame Mbarawa siyo siri, ni adui mkubwa wa Makandarasi katika sekta zote za Ujenzi na hata hapo mwisho Maji.

Mbarawa ni kama mtu wa kisirani na mara nyingi hana focused objectives.

Tutegemee nini sasa sekta hii ya ujenzi maana huku mwishoni aliwaita makandarasi kuwa wezi na akataka miradi yote ya Maji ifanywe kwa Force Account.

Karibu Mbarawa.

2173187_20190929_070741.jpg
 
Karibu Mbarawa.
Naona aligusa penye maslahi yako panapoumiza kweli, maanake nakumbuka wakati huo ulimwanzishia mada kama hii ya leo.

Huko kwenye kandarasi zenu naona kuna uozo mkubwa sana msiopenda uguswe. Sijui Magufuli mlimpendea nini, au ilikuwa ni kumwogopa, maanake sijawahi kusikia mkimlalamikia yeye. Pengine ni kwamba mlijua jinsi ya kula na kipofu?
 
Jamaa hana upendo na makandarasi wazalendo, na kandarasi za ujenzi ndiyo maisha yetu.
 
Inawezekana ni kutomwelewa tu anachotaka mfanye.

Hata mimi makandarasi wananchi nawapenda kweli kama wanafanya kazi zao bila ubabaishaji, kwa sababu kuinuka kwa hawa ndiyo kuinuka kwa taifa letu.

Naona kwenye barua uliyoibandika hapo juu, kuna malalamishi amabyo sijaona ukiyapatia jibu hapa. Je, kuna ukweli wowote juu ya hayo aliyoyalalamikia? Kama hayo mambo yapo, huoni kwamba ni haki yake kuwanyima kazi?

Inaeleweka, hakuna asiyetaka cha chee kama hakuna uangalizi mahususi, lakini vya chee ndivyo vinavyoturudisha nyuma katika maendeleo ya nchi yetu.
 
Hakuna kitu haoi zaidi ya kuwajaza wazenji wenzake tu na kina mama kwa kutaka aioate 50/50
 
Inawezekana ni kutomwelewa tu anachotaka mfanye.

Hata mimi makandarasi wananchi nawapenda kweli kama wanafanya kazi zao bila ubabaishaji, kwa sababu kuinuka kwa hawa ndiyo kuinuka kwa taifa letu.

Naona kwenye barua uliyoibandika hapo juu, kuna malalamishi amabyo sijaona ukiyapatia jibu hapa. Je, kuna ukweli wowote juu ya hayo aliyoyalalamikia? Kama hayo mambo yapo, huoni kwamba ni haki yake kuwanyima kazi?

Inaeleweka, hakuna asiyetaka cha chee kama hakuna uangalizi mahususi, lakini vya chee ndivyo vinavyoturudisha nyuma katika maendeleo ya nchi yetu.
Barua hiyo ni kichaka tu cha dhamira iliyojificha.
Hakuna mtu anaandika barua kuwa atawakomoa na mtakoma ubishi.
Lakini barua hiyo inaelekea huko.
 
Bora mzee Chamuriho ametolewa ujenzi maana alikuwa mzigo mzito,
sasa Prof Mbarawa fuatilia ujenzi wa barabara,
 
Professor Mbarawa alishawahi kuwa waziri wa Ujenzi na kwa mujibu wa Magufuli alisema hadharani kuwa ile wizara ilimshinda na hivyo kumuhamishia wizara ya maji. Ghafla leo analetwa tena wizara hiyo hiyo ya Ujenzi, kuna kitu gani kipya atafanya?
 
Back
Top Bottom