Prof. Mbarawa arudi kuwa Waziri wa Ujenzi, tutegemee nini katika sekta hii?

Prof. Mbarawa arudi kuwa Waziri wa Ujenzi, tutegemee nini katika sekta hii?

alikuwa hawajibiki kabisaa, yani yupo kama hayupo......wizara ili dorora, alikuwa anazuga tu, bora kawekwa benchi.

Sasa Prof Mbarawa ni Mfuatiliaji mzuri, ila tunamuomba awe mkali, tunafahamu kuwa hapo wizarani kuna vidudu watu, tunawafahamu kwa majina yao.
Kwa hiyo alikuwa anasubiri atolewe,bora hajauliwa maisha yaendelee
 
Ngoja tuone ingawa mtoto wa nyoka ni nyoka lakini mara zingine hua na tabia za mjusi...
 
Hongera Professor Mbarawa,kwa kurejeshwa tena kwenye wizara ya Ujenzi na uchukuzi.Awamu ya tano ulichapa Sana kazi,katika wizara ulizopewa kusimamia lakini wasaidizi wako ndiyo walikuwa wanakuangusha au wanakuchomekea au hawatekelezi maagizo yako na ulikuwa huwachukulii hatua
Ushauri
1). Wizara ya Ujenzi na uchukuzi ijielekeze kwenye kuteleza Ilani ya Uchaguzi ya 2020-2025 pamoja na ahadi za Mgombea na Mgembea Mwenza wa Rais, walizotoa sehemu mbalimbali wakati wa Kampeni.
2). Mgombea Mwenza 2020 (Rais SSH) akiwa Kitangari wakati wa Kampeni alitoa ahadi ya kujenga kwa kiwango Cha lami Barabara ya mkoa ( TANROAD) kutoka Mtama-Mkoa wa Lindi kupitia Kitangari mpaka Amkeni Newala.(barabara ilisahaulika kwenye jedwali la barabara za TANROAD).
3). Waziri na Wasaidizi wake wasimamie kwa karibu Wakandarasi wa miradi mbalimbali,ili kupata thamani ya kazi (value for money) na kuepuka variations.
4) Kuna wananchi wa kipunguni ambao walifanyiwa valuation mwaka 2005 kupisha upanuzi wa JNIA, lakini mpaka leo bado kulipwa fidia, japokuwa viwanja wameshaanza kugawiwa.
 
Back
Top Bottom