Prof. Mbarawa: Treni hii ya Tanzania siyo high speed train kama zile za vichwa vilivyochongoka, Wananchi eleweni hilo


Kulikua na haja ya Mh Waziri kuja na hii kauli ya ufafanuzi kipindi hiki? Kwa nini?
 
Kwa Bongo inawezekana, na ikiwa hivyo basi wasituharibie umeme wetu!!

Hii nchi raha sana... umeme wa matumizi ya kawaida hatuna lakini tuna reli ya umeme!!

Usishangae siku zijazo mtu akatoka na mpango wa kufunga treni masolar pannels ya kutosha. Utasikia mkandarasi ameletwa kwa gharama kubwa ili train zisisimame kutoa huduma.
 
Ni kweli..lakini mbona kwenye picha zao za mwanzo hao TRC walituonesha kitu tofauti na tulicholetewa?
Weka hiyo picha tuione acha gubu,,, mimi nilivyojua ni kwamba hizo treni zitakuwa na mfumo wa umeme kiundeshwaji lkn si zile zenye vichwa vya kuchongoka,, zile za vichwa vya kuchongoka zipo south Africa tu kwa ukanda huu wa SADC,, tena south Africa yenyewe ni Pretoria mpaka joberg ruti moja tu tena fupi na nchi ina uchumi mzuri, sembuse sisi uchumi wenyewe ungaunga mwana, ivo nyie na akili zenu mlijua hizo treni zitakuwa zile za vichwa vilivyochongoka 😃
 
johnthebaptist hii nchi ni shida. Viongozi hutuona watanzania hatuna akili. Kulikua na sababu gani kutudanganya hapo mwanzo na picha za vichwa mchongoko?? Ila tukumbuke kilikua kipindi cha bwana yule, ambaye kudanganya ilikua ni sifa nzuri.
Ina maana haya makontena ndiyo yalimfanya bwana yule atekeleze reli ya treni za umeme??kweli jamani?? Na minyaya yooote ile ilivyotandazwa kama ulaya? au ni hawa walamba asali ndio wameshatoboa mzinga wa asali wakaleta makontena haya?? Basi tunaombeni mrudishe haya makontena mtuletee katreni kapo kama mjusi kamoja tuu hata kama ni ka mabehewa matano katatupooza moyo jameniii eeeeh..
 
Usipost habari nusunusu, alisema kutakuaa na awamu tatu, awamu ya mwisho kabisa ndo wataleta vichwa na mabehewa yake ya treni ya high speed.
 
Ccm na ilaaniwe
 
Hatuhitaji ukweli zaidi tunataka katreni kapo kama mjusi, kanakoendana na reli zake, haijalishi ni nani kadanganya ilimradi reli kama ulaya ipo basi tunaitaka treni inayoendana na reli zake..hatutaki makontena haya, watuletee 'mjusi' wetu
 
Basi waachane na hizi kontena watuletee mchongoko wetu,
 
Hivi walitwambia yatakuwa yanatembea kilometa ngapi kwa saa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…