Prof. Mbarawa: Treni hii ya Tanzania siyo high speed train kama zile za vichwa vilivyochongoka, Wananchi eleweni hilo

Prof. Mbarawa: Treni hii ya Tanzania siyo high speed train kama zile za vichwa vilivyochongoka, Wananchi eleweni hilo

Hapana... tusichanganye mambo!!

Reli kuwa ya umeme haina maana kwamba itatumia high speed trains. Tofauti ya electrified SGR na ile isiyokuwa electrified ni kwamba Train zitakazopita kwenye electrified SGR zitakuwa za kasi zaidi kuliko zile zisizo electrified lakini bado kasi hiyo haitakuwa sawa na high speed train.

Which means, trains zitakazotumia SGR yetu zitakuwa za kasi zaidi kuliko zile za Kenya!!

Makame kasema ukweli, sema tu watu tunajisahaulisha. Mara kadhaa, tangu wakati wa uzinduzi wake ilishasemwa SGR itawezesha trains kutembea kwa speed ya 160KM/HOUR kwa sababu ni electrified.

In contrary, high speed trains ni zile zinazoenda kwa speed ya 250km/hour na kuendelea, na ujenzi wa hizo reli ni very expensive.

Kulikua na haja ya Mh Waziri kuja na hii kauli ya ufafanuzi kipindi hiki? Kwa nini?
 
Kwa Bongo inawezekana, na ikiwa hivyo basi wasituharibie umeme wetu!!

Hii nchi raha sana... umeme wa matumizi ya kawaida hatuna lakini tuna reli ya umeme!!

Usishangae siku zijazo mtu akatoka na mpango wa kufunga treni masolar pannels ya kutosha. Utasikia mkandarasi ameletwa kwa gharama kubwa ili train zisisimame kutoa huduma.
 
Ni kweli..lakini mbona kwenye picha zao za mwanzo hao TRC walituonesha kitu tofauti na tulicholetewa?
Weka hiyo picha tuione acha gubu,,, mimi nilivyojua ni kwamba hizo treni zitakuwa na mfumo wa umeme kiundeshwaji lkn si zile zenye vichwa vya kuchongoka,, zile za vichwa vya kuchongoka zipo south Africa tu kwa ukanda huu wa SADC,, tena south Africa yenyewe ni Pretoria mpaka joberg ruti moja tu tena fupi na nchi ina uchumi mzuri, sembuse sisi uchumi wenyewe ungaunga mwana, ivo nyie na akili zenu mlijua hizo treni zitakuwa zile za vichwa vilivyochongoka 😃
 
johnthebaptist hii nchi ni shida. Viongozi hutuona watanzania hatuna akili. Kulikua na sababu gani kutudanganya hapo mwanzo na picha za vichwa mchongoko?? Ila tukumbuke kilikua kipindi cha bwana yule, ambaye kudanganya ilikua ni sifa nzuri.
Ina maana haya makontena ndiyo yalimfanya bwana yule atekeleze reli ya treni za umeme??kweli jamani?? Na minyaya yooote ile ilivyotandazwa kama ulaya? au ni hawa walamba asali ndio wameshatoboa mzinga wa asali wakaleta makontena haya?? Basi tunaombeni mrudishe haya makontena mtuletee katreni kapo kama mjusi kamoja tuu hata kama ni ka mabehewa matano katatupooza moyo jameniii eeeeh..
 
Waziri wa Uchukuzi Prof Mbarawa amewataka Wananchi kutochanganya Treni hii ya Tanzania na zile za high speed zenye vichwa vilivyochongoka

Prof Mbarawa amesema picha zinazorushwa mitandaoni na watu wasio na nia njema ni zile za high speed zinazotembea zaidi ya km 200 kwa saa

Za kwetu ni hizi mnazoona tunazipokea na haya ni Mabehewa 14 ya Daraja la tatu( economy) na mwezi February mwakani tutapokea Ya Business class na First class

Mabehewa haya ni kwa ajili ya masafa marefu na yatavutwa na Vichwa vya Umeme lakini yale ya high speed Vichwa vyake vinaunganishwa direct na mabehewa, amesisitiza Mbarawa

Source ITV Habari
Usipost habari nusunusu, alisema kutakuaa na awamu tatu, awamu ya mwisho kabisa ndo wataleta vichwa na mabehewa yake ya treni ya high speed.
 
Sasa kwanza mjue hivo vichwa vitavyokuja mtaambiwa vina mifumo miwili yaani umeme na mafuta, kwahiyo kwakua kuna matengenezo makubwa ya umeme wa uhakika inamaana watatumia mafuta hapo miaka inasogea, wakikaribia uchaguzi italetwa treni tena nyingine ya kuzugia hadi moro ya umeme itaenda kwa ajili ya kampeni halafu mkiingia kingi kuwapa kura za kishindo story inaishia hapo
Ccm na ilaaniwe
 
Tukiisha anza kuitana watu wasio na nia njema!, kama naanza kuogopa ogopa hivi!, hivi kwa bandiko kama hili... Hongera TRL kwa Mabehewa Mapya. SGR ni Reli Mpya ya Kisasa; Je, Mabehewa Haya ni Mapya ya Kisasa? Hakuna Ubaya Kutumia Mitumba, Ila Tuambiwe Ukweli!, hivi viji tenda vya kutangaza uzuri wa tereni hizi mupya, tutapata kweli?.
P
Hatuhitaji ukweli zaidi tunataka katreni kapo kama mjusi, kanakoendana na reli zake, haijalishi ni nani kadanganya ilimradi reli kama ulaya ipo basi tunaitaka treni inayoendana na reli zake..hatutaki makontena haya, watuletee 'mjusi' wetu
 
Weka hiyo picha tuione acha gubu,,, mimi nilivyojua ni kwamba hizo treni zitakuwa na mfumo wa umeme kiundeshwaji lkn si zile zenye vichwa vya kuchongoka,, zile za vichwa vya kuchongoka zipo south Africa tu kwa ukanda huu wa SADC,, tena south Africa yenyewe ni Pretoria mpaka joberg ruti moja tu tena fupi na nchi ina uchumi mzuri, sembuse sisi uchumi wenyewe ungaunga mwana, ivo nyie na akili zenu mlijua hizo treni zitakuwa zile za vichwa vilivyochongoka [emoji2]
Basi waachane na hizi kontena watuletee mchongoko wetu,
 
Inatia UCHUNGU sanaaa hii nchi manina[emoji34]
IMG_20211209_230005.jpg
 
Waziri wa Uchukuzi Prof Mbarawa amewataka Wananchi kutochanganya Treni hii ya Tanzania na zile za high speed zenye vichwa vilivyochongoka

Prof Mbarawa amesema picha zinazorushwa mitandaoni na watu wasio na nia njema ni zile za high speed zinazotembea zaidi ya km 200 kwa saa

Za kwetu ni hizi mnazoona tunazipokea na haya ni Mabehewa 14 ya Daraja la tatu( economy) na mwezi February mwakani tutapokea Ya Business class na First class

Mabehewa haya ni kwa ajili ya masafa marefu na yatavutwa na Vichwa vya Umeme lakini yale ya high speed Vichwa vyake vinaunganishwa direct na mabehewa, amesisitiza Mbarawa

Source ITV Habari
Hivi walitwambia yatakuwa yanatembea kilometa ngapi kwa saa?
 
Back
Top Bottom