Katika hotuba yake Mhe. Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa na utekelezaji wa mradi huo ambao amesema utasaidia kurahisisha na kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo na abiria, na pia utaokoa barabara ambazo zinaharibika kutokana na kusafirisha mizigo mizito kwa magari.
“Kwa kutumia Reli hii mtu atasafiri kutoka Dar es Salaam hadi hapa Dodoma kwa saa 3 tu ikilinganishwa na saa 5 hadi 6 zinazotumika hivi sasa kusafiri kwa gari na pia mtu atasafiri kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa saa 9 ikilinganishwa na saa 36 anazotumia hivi sasa kusafiri kwa Treni” amesema Rais Magufuli na kuongeza kuwa Reli hiyo itakuwa na uwezo wa kusafirisha Tani milioni 17 za Mizigo kwa Mwaka ikilinganishwa na ya sasa yenye uwezo wa kusafirisha Tani milioni 5 tu.
Hii hotuba ya JPM, kudhihirisha alishozema waziri ni sahihi toka mwanzi ilikuwa train ya speed mpaka 180kmh kwa hiyo hakuna jipya rudieni hotuba za JPM aliyeanzisha huu mradi hakuna sehemu waliseme bullet speed maana ingekuwa 1.5 yu Dar to Dom