Prof.
Heshima kuu kwako!! Nina maswali machache ambayo naomba kama una wasaa utusaidie na ikiwezekana nawe unisikilize labda naweza kukufaa kwa leo.
Kwanza binafsi na kwa uelewa wangu na elimu kidogo niliyo nayo kuliza swali kuwa corona ipo au haipo kwa Tanzania ni kama kuuliza "mama mkwe kavaa nguo ya ndani ya rangi gani",hivyo sitauliza swali hilo.
- WHO wasema kuwa hamjatoa takwimu za corona tangu May 2020.Kama ni kweli ni sababu zipi ambazo zimefanya tusitoe takwimu hizo"
- Corona ni ugonjwa wa mlipuko lakini mpaka sasa tuna terminology mbili zimezuka,Pneumonia kali na changamoto za upumuaji.Magonjwa haya mawili yana uhusiano wowote na corona?
- Tuchukulie kwa mfano wewe kama Prof unaita waandishi wa habari na unasema haya yafuatayo,je utapata hasara gani?Maneno yenyewe ni haya,"Tanzania hatuna corona lakini corona ipo nchi jirani.Kwa kuwa tuna muingiliano na mataifa haya naagiza yafuatayo,abiria ndani ya vyombo vya usafiri vya watu wengi wavae barakoa,kila nyumba iwe na maji tiririka na sabuni....................."