Prof. Mkenda, hivi Rais Samia anajua hizi shule zinazofunguliwa hazina walimu na wanagawana walewale wachache?

Pole Mzee, mungu amtupi mja wake šŸ™
 
Hilo kweli aisee; nina ndugu yangu amemaliza degree, bachelor of education in primary education, tangu 2018 lakini mpaka leo hakuna kinachoeleweka.......yupo tu anahangaika na kujitolea. Umri unaenda, wadogo zake wanaomaliza 2019,2020,2021 wanaajiriwa ye yupo tu. Inauma kweli lkn ndo hivyo, wenye nafasi wameamua.
 
Nafasi za ajira,nina uhakika watatangaza tena mwaka huu,aendelee kuomba Kama wengine tutakavyoomba,ila sasa kinachokuja kushangaza sasa,yaani mtu aliyemaliza 2021 au 2020 anapangiwa shule,huyo wa 2018 au sisi wa 2017 tunaachwa.
Haijulikani vigezo ni vipi hasa vinavyotumikaga hasa.
Anyway,asichoke kuomba,japo ukweli ni kwamba walimu ni wachache sana ukilinganisha na wastani wa wanafunzi wanaotakiwa kufundishwa.
 
Kwa kawaida serikali inahitaji madarasa 40,000 na Walimu 170,000 ili kuondoa upungufu.

Tatizo bajeti


Japo wanatumia Milioni 400 kununua LC300 V6
 
Yaani mngejua jinsi hawa walimu wanavyozembea huko mashuleni, acha tu. Mtu anaingia darasani mara moja kwa wiki.
Wapeni motisha..imagin mwalimu anapokea mshahara laki mbili na elfu kumi🤣 halafu anadeni la laki moja na nusu. Teaching allowance ni dawa ya haya yote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…