Mambo mazuri ya kuiga kutoka dunia ya kwanza kama (invasion of technology) hatuyaigi...ila ya hovyo kama haya ndio fasta tunayaiga
O-Level nimesoma private school!
Ingawaje kwa sasa inaonekana ni shule ya kawaida sana lakini wakati ule ilikuwa ni shule ambayo majority of middle class wangependa kusoma!!
Ada tuliyokuwa tunalipa pale ni zaidi ya mara 10 ya ada ya shule za serikali! Ukichanganya na michango hii na ile, basi ilikuwa taabu tupu!!
Darasani kwetu tulikuwa tunasoma na msichana ambae alihamia pale akiwa Form III. Kwavile nilikuwa karibu nae, baadae nikagundua hapo kabla alikuwa anasoma shule ya serikali lakini akatimuliwa baada ya kupata ujauzito!
Kwavile home kwao kulikuwa na visenti kidogo vya kubadili mboga, ndipo akahamishiwa Private School!!
Now assume huyo binti angekuwa ni mtoto wa maskini...
Je, hiyo private school angeinusa au ingekuwa ndo mwisho wake wa kupata elimu?!
Ukiyatafakari hayo ndipo utagundua ni wewe kutoka Dunia ya Tatu ndie unahitaji zaidi mtoto akipata ujauzito aruhusiwe kuendelea kuliko huyo wa Dunia ya Kwanza mwenye MULTIPLE OPTION!
My classmate hakuhitaji serikali iruhusu mwenye ujauzito aendelee ili nae aweze kuendelea na shule!
Inawezekana hata wewe huhitaji serikali iruhusu mtoto wako aendelee na shule akipata ujauzito but am certain majority ya ndugu zako wanahitaji ruhusa hii ya serikali ili watoto wao waweze kuendelea na masomo inapotokea wamepata ujauzito kwa sababu bila hivyo hawataweza ku-afford gharama za private schools!!
Ingewaje imeshakuwa proved beyond reasonable doubt kwamba jamii IMESHINDWA kudhibiti ngono za utotoni, njia pekee ya kuwasaidia hao ambao nyinyi wenyewe mmeshindwa kuwadhibiti ni kuwaruhusu waendelee na shule!
That being said, hiyo misimamo yenu isiyo na msingi inamuathiri zaidi mtoto wa maskini kuliko mtoto wa mwenye nacho!! Hakuna mtoto wa mwenye nacho ambae atashindwa kuendelea na elimu eti kisa kapata ujauzito!!
Hapa anatetewa mtoto wa maskini ambae hana alternative na wala msilete unafiki wa kwamba kwanini aanze ngono wakati ni mwanafunzi! Nasema msilete huo unafiki kwa sababu am certain hata huko makwenu majority walianza ngono wakiwa bado wanafunzi, but just by chance, or by means of good lucky wakabahatika kutopata ujauzito!!
They did nothing kutopata mimba... IT'S JUST LUCKY!