Prof. Mkenda: Wazazi wana haki ya kuzuia Watoto kwenda Shule nyakati za Mvua kubwa

Prof. Mkenda: Wazazi wana haki ya kuzuia Watoto kwenda Shule nyakati za Mvua kubwa

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Wizara ya Elimu imezipongeza shule zilizochukua hatua ya kuwapumzisha wanafunzi wake kwa muda kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha huku ikisema inaendelea kuwasiliana na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) ili kuona kama kuna umuhimu wakuchukua hatua zaidi.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Aprili 24, 2024 na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Profesa Adolf Mkenda alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Profesa Mkenda amesema kutokana na hali ya hewa inayoendelea na baadhi ya maeneo kuathiriwa kwa kiasi kikubwa; na miundombinu kuharibika, kuna haja ya kuchukua hatua zaidi.

Ameahidi kuwa, Kamishna wa Elimu atakuja kutoa utaratibu ikiwamo ratiba ya ufiadiaji vipindi.

Sambamba na hilo, pia amesema wazazi wana haki ya kuwakataza watoto wao wasiende shule pindi wanapoona hali ya hewa sio nzuri ukizingatia wengi wanatoka nyumbani asubuhi na kurudi jioni.

"Katika hili naomba wamiliki wa shule wawe waungwana hasa shule binafsi, watoto wengi wanakaa mbali na maeneo wanayosoma hivyo inapotokea wameona hali ya hewa imebadilika au kuanza kubadilika wawaruhusu mapema na wahakikishe wanawasiliana ma wazazi wao,"amesema Waziri Mkenda.


MWANANCHI
 
Back
Top Bottom