Prof. Mkumbo ameshindwa kujibu maswali ya Boniface wa CHADEMA kwenye mdahalo wa Tathimini ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Kwani Watanzania tuliambiwa na Mungu tutaishi milele?
Ndio mtu apigwe risasi kwa sbb eti Mungu alisema tutakufa, ww utakuwa agent wa shetani
 
Eti hawana wakati walichokitaka ni kushinda na wameshinda kwa kishindo, halafu dogo mitandaoni eti hawana raha! Ahahahahaha!!!'
walitaka Chauma ichukue viti vingi kidogo ili ndio kiwe mbadala wa chadema, lengo sijui kama limefikiwa
 
Kwetu miaka mitano iliyopita wananchi walikuwa wakijiongoza na wamesema hata sasa watajiongoza, hawaoni sababu ya kupewa kiongozi wasiyemchagua.
 
Lakini boni yai nae pia sio mtulivu,anapapara,hajui kupangilia hoja ikaeleweka,sana sana anaatack personal kuliko kuongea hoja ya kushawishi.

..Boni alikuwa vizuri.

..jukumu lake lilikuwa kupangua hoja za Prof.Kitila.

..pia kubomoa imani ya wasikilizaji kwa Prof.Kitila ndio maana akamuita mtu asiye na aibu.

..Prof.Kitila alikwenda kupotosha wafuatiliaji kipindi. Kwa mfano alishiriki kudanganya kwamba hakuwa ndani ya Chadema / Ukawa wakati wa mkutano wa Katiba Mpya 2013.
 
Alikuwa hana hoja kabisa, alishia kusema wapinzani hawakujiandaaa
 
Kila baada ya uchaguzi story ni "Wameshinda lakini hawana furaha" if it bothers them si ilibidi waache?
 
Alikuwa hana hoja kabisa, alishia kusema wapinzani hawakujiandaaa

..Ni ngumu sana kujitokeza mbele ya vyombo vya habari kuitetea Ccm.

..Inahitaji mtu asiye na aibu kufanya hivyo, na hicho ndicho tulichokishuhudia kwa Prof.Kitila Mkumbo.
 
Alikuwa hana hoja kabisa, alishia kusema wapinzani hawakujiandaaa

..kuna wakati Prof.Kitila alisema Ccm waliishauri serikali lakini watendaji hawakutekeleza.

..Sasa Mwenyekiti wa Ccm pia ndio Raisi wa Jamhuri ya Tanzania. Sasa imekuwaje maagizo na ushauri wa chama chake usitekelezwe na serikali?

..Ukiacha hilo Mwenyekiti wa Ccm ndiye Waziri wa Tamisemi. Sasa inawezekana vipi ushauri wa Mwenyekiti usitekelezwe na Tamisemi?

..Naibu Waziri wa Tamisemi ni mkwe wa Mwenyekiti wa Ccm, Rais wa Jamhuri, na Waziri wa Tamisemi.

..Katika mazingira na uhalisia huo inawezekana vipi ushauri wa CCM usifanyiwe kazi na watendaji wa Tamisemi?
 
Ushindi usio na haki haina furaha. Wameshinda Asilimia 99.
Mi nakisia tu.
Ukimweleza Mchengerwa habari hiyo ya kukosa furaha, atakushangaa sana!

Mchengerwa alipo, atakuwa anajipongeza sana kwa kazi kubwa aliyo mfanyia mama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…