Prof. Mkumbo ameshindwa kujibu maswali ya Boniface wa CHADEMA kwenye mdahalo wa Tathimini ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Prof. Mkumbo ameshindwa kujibu maswali ya Boniface wa CHADEMA kwenye mdahalo wa Tathimini ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Gabeji

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2024
Posts
1,530
Reaction score
1,903
Tathmini ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika jana chini ya kituo cha Star TV, uliongozwa na Chief Odemba.

CHADEMA iliwakilishwa na Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani, Boniface, CCM iliwakilishwa na Prof. Mkumbwa, na ACT Wazalendo walikuwa na Makamu Mwenyekiti wao.

Prof., kwa akili kabisa, alikiri kuwa wapinzani walienguliwa. Aliulizwa swali: "Ni sheria gani inasema mgombea akishindwa kujaza fomu aenguliwe?" Prof. alishindwa kujibu swali hilo, lililoulizwa na Boniface wa CHADEMA.

Ukimwangalia Prof., sura yake inaonesha wazi kuwa ndani ya nafsi yake anasumbuliwa sana kwa matokeo ya uchaguzi. Hana raha kabisa, japo ndiye aliyetumwa na chama chake cha CCM.

NB: CCM imeshinda uchaguzi, lakini hawana furaha kabisa. Watanzania wamekata tamaa.

Think tank ya CCM inapaswa kukaa chini na kujiuliza: kipi bora, ushindi wa 99% 💯 au uhai wa Watanzania?

Mungu ibariki Tanzania.
By mwinjilisti wenu, Gabeji.
 
Tathimini ya uchaguzi wa serikali za mitaa,ulifanya jana chini ya kituo cha star tv,kingingozwa na chief Odemba.
Chadema iliwakilishwa na mwenyekiti wa kanda ya pwani Boniface, na ccm iliwakilishwa na prof mkumbwa, act wazalendo na MAKAMU mweyeikiti.
Prof,akili kabisa kuwa wapinzani walienguliwa, aliulizwa swali ni sheria gani inasema mgombea akishindwa kujaza form aengulie? Prof.alishindwa kujibu swali hilo ,liloulizwa na Boniface wa chadema.
Ukimwangalia prof.sura yake naonesha ndani ya nafsi yake inamsuta kabisa kwa matokeo ya uchaguzi. Hana raha kabisa, japo ndio alie tumwa na CHAMA chake cha ccm.
NB. Ccm imeshida uchaguzi lakini ccm hawana furaha kabisa, watanzania wamekata tamaaa.
Thinking tank, ya ccm wakae chini wangalie,kipi bora ushindi 99💯 au uhai wa watanzania?
Mungu ibariki Tanzania by mwinjilist wenu Gabeji.
Ukimwangalia prof.sura yake naonesha ndani ya nafsi yake inamsuta kabisa kwa matokeo ya uchaguzi. Hana raha kabisa, japo ndio alie tumwa na CHAMA chake cha ccm.
20241201_064532.jpg
 
Huwa mnajifariji sana badala mfanye siasa muwaeleze watu sera zenu nyie mnapiga porojo mitandaoni
Utaeleza sera wapi wakati umeenguliwa kwani nyie mpita kwa sera au mabavu, kwani kuna Chama hatakimoja kinasera yakubomoa madarasa na kuvunja hospitali kikiingia madarakani. CCM kimekosa ushawishi kwa wananchi kwahiyo kwa sasa kinatumia vitisho na mabavu ili wananchi waogope kwenda upinzani.
 
Ccm wamebakisa wizi wakura na kutumia mapolisi tofauti na hapo hakuna chama cha siasa hapo no genge la wanyanganyi
 
Lakini boni yai nae pia sio mtulivu,anapapara,hajui kupangilia hoja ikaeleweka,sana sana anaatack personal kuliko kuongea hoja ya kushawishi.
 
Pamoja na kwamba wametangaza Wameshinda lakini wanaona aibu hata kupita mbele ya Wananchi wao.
 
CCM wanajitengenezea image mbaya kwa wananchi na Jeshi la wananchi. Nina hakika miaka ya mbele kunaweza kutokea revolution waache waone kua wamefika kwenye ujinga wanaofanya.
 
Ccm wamebakisa wizi wakura na kutumia mapolisi tofauti na hapo hakuna chama cha siasa hapo no genge la wanyanganyi
Kila siku hàyo hàyo, mnaibiwaaaa mnaibiwaaaa! Nendeni mkafanye kazi mnayoiweza, hiyo ya kupàta 0.79% hamuiwezi kila siku kulialia tuu mñàkerà.
 
Huwa mnajifariji sana badala mfanye siasa muwaeleze watu sera zenu nyie mnapiga porojo mitandaoni
Nyie CCM mnasera gani zaidi kuuw watu na kujaza kura feki kwenye masanduku ya kupigia kura
 
Huwa mnajifariji sana badala mfanye siasa muwaeleze watu sera zenu nyie mnapiga porojo mitandaoni
Sio kwa hapa nchi ilipofika, utapigiwa kura ila anaetaja matokeo ni mwingine, so point yako ni irrelevant
 
Huwa mnajifariji sana badala mfanye siasa muwaeleze watu sera zenu nyie mnapiga porojo mitandaoni
Ninyi mnaowaeleza watu sera zenu inakuwaje mtumie nguvu za Polisi na wasimamizi wa uchaguzi kujipa ushindi?
 
Back
Top Bottom