Mzee wa kupambania
JF-Expert Member
- Aug 14, 2022
- 21,767
- 54,912
Mimi sioni faida za kushinda kwake labda nyie makada wenzake mnaweza kuwa na majibu 😅Kama n hvy mbona unatokwa na mishipa ya kichwa kuuliza manufaa akishinda? Bila kuuliza akishindwa.
Vumilia tuu mkuu, Najua unateseka Ila ndo hvy ameshashinda, kuwa kimya kama haters wenzako wengine wanaoumia taratibu 😂
Hii nafasi ilikiwa yetu kabisa hii.Hii ni taarifa ya hivi punde.
Prof. Mohamed Janabi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili amechaguliwa kuongoza Shirika la Afya Duniani ukanda wa Africa.
Pongezi nyingi kwake na watanzania.
===============
Profesa Mohamed Janabi, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), amechaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa Shirika la Afya Duniani (WHO). Uchaguzi huo umefanyika leo, Jumapili Mei 18, 2025, huko Geneva, Uswisi.
Prof. Janabi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Faustine Ndugulile, aliyekuwa Mkurugenzi Mteule wa Kanda hiyo na Waziri wa zamani wa Afya wa Tanzania, aliyefariki dunia Novemba 2024.
Katika nafasi hii mpya, Prof. Janabi atahudumu kwa kipindi cha miaka mitano, akiwa na fursa ya kuchaguliwa tena kwa muhula mmoja zaidi. Kazi yake kuu itakuwa ni kuongoza juhudi za kuunda sera za afya, kuratibu huduma za dharura za afya, pamoja na kushinikiza suluhu bunifu kwa changamoto za kiafya barani Afrika.
Wagombea wengine walioshiriki katika uchaguzi huo lakini hawakufanikiwa ni pamoja na:
- Moustafa Mijiyawa (Togo)
- Dk. N’Da Konan Michel Yao (Ivory Coast)
- Mohamed Lamine Dramé (Guinea)
VIDEO: Rais Samia amuombea kura za Ukurugenzi wa WHO Mohammedi Janabi
Ndugu zangu Watanzania, Nashindwa niandike nini ,nashindwa niseme nini ,nashindwa nieleze vipi juu ya uwezo mkubwa wa kiakili alionao na aliojaliwa kuwa nao Rais wetu Mpendwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan. Rais Samia ni Mpango wa Mungu,ni chaguo la Mungu na kapewa akili nyingi na...www.jamiiforums.com
View attachment 3338251
Hee! Wewe mama kwani una umri gani hasa au ni mdada upo under 20?Kura za kuhonga wallah ,maana ni Janabi ni zero brain. Kulinganisha na wenzake.
Mkuu unazunguka Sana Aisee, Sawa tupe hasara za yeye kushinda.Mimi sioni faida za kushinda kwake labda nyie makada wenzake mnaweza kuwa na majibu 😅
Sijui kwa kwelii maana mimi ni mmoja wapoooWale watu sijui watajificha wapi
Zaidi ya manufaa kwa familia zao hizo nafasi wewe zinakusaidia nini?Prof. Yupo vizuri. Naamini ataitendea haki hii nafasi.
Ukweli ni kwamba kuna Watanzania Wazuri tuu, kama wangepata support ya taifa wangeipeperusha vyema bendera yetu.
Mpaka sasa sijui kwa nini Tz haikuweka candidate kwa nafasi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola.
Wangemuweka Balozi Mulamula, naamini angepata ile nafasi. Sasa imeenda Ghana.
Pia tuwe aggressive UN na AU na hizi nafasi za mashirika ya kikanda.
Waziri wa mambo ya nje, kila mwaka atoe report ya Watanzania waliopata nyadhifa kubwa kimataifa. Mabalozi wetu wapimwe kwa ushawishi katika hili pia.
Mabalozi wetu wengi wamelala. Wawajibike.
Yani ashinde Dr Ndugulile ndio ashindwe Profesa Janabi?Kuna watu walikuwa wanasema hatoshinda kisa uwezo mdogo sijui wako wapi now
Yani umfananishe Janabi na Ndugulile ? Anyway simsemi vibaya Janabi lakini Ndugulile alikuwa na CV nzuri kuliko huyu wa sasa.Yani ashinde Dr Ndugulile ndio ashindwe Profesa Janabi?
Dr Ndugulile ana sifa zipi za kumzidi Janabi na alishinda bila kufanyiwa kampeni nzito kama alizofanyiwa Janabi na Rais.
Mlivyokuwa mnaponda hamkujua kama kuna izo fadhila??Punguza kelele basi si kapewa tu kulipa fadhira za yule Marehemu NDUNGULILE
Mpumbavu wew hapo unayeumia kwa Prof Janabi kushinda nafasi ya WHO!!! Una husda na husda mwisho wake ni uchawi!!Maelezo marefu kama gazeti ila hakuna sehemu yoyote uliyojibu swali nililouliza.
Kati ya mimi na wewe nani mpumbavu?
Yani Profesa anazidiwa Cv na Dr Ndugulile?Yani umfananishe Janabi na Ndugulile ? Anyway simsemi vibaya Janabi lakini Ndugulile alikuwa na CV nzuri kuliko huyu wa sasa.
Sababu ya kununa ni nini ?CHADEMA watanuna mbaya..!
Umepiga panapoumaHahakikishe wazazi wa Tanzania wanajifungua bila kulazimishwa kununua gloves
Watoto na wazee wa Tanzania watibiwe bure
Other wise atakuwa hapo kuwatumikia mafisadi waliomuweka ili wapige pesa kupitia miradi ya afya
Ni hayo tu kwa janabi!!