Prof. Muhongo amuunga mkono Prof. Mwandosya, TCU kimya!

Kwa mara ya kwanza Muhongo kaongea point. Point kubwa na ya msingi ni kwamba akina Sospeter wangebaki vyuoni kama maprofesa wangekuwa useful zaidi kwenye jamii kuliko walivyoingia kwenye siasa.
Hii ndio point ambayo nae inabidi ambiwe. Alitakiwa atulize ball huko chuoni sio kuja kwenye siasa. Yeye mwenyewe mnganga njaa tuu.
 
Kama umefikia hatua ya ku question elimu ya Mhongo basi una tatizo mahali.
 
Umeandika utumbo kabisa
hujaelewa msingi was hoja juu ya PhD za hao mawaziri. Taratibu za kupata PhD ni universal na Zina guidelines sio Mambo ya Senate sijui imeridhika Wala Nini Rudi ukasome vizuri argument za profesa Muhongo then utaelewa, unless elimu yako ni ya mchongo🤣🤣🤣
 
Hapa ukichokonao zaidi yanaweza kuwa ya Ben Sanane,mwamba alioji Phd ya jamaa mpaka leo Mungu ndo anajua kama yu mzima au la
 
Hawa kina Prof Mwandosya, Prof Muhongo, Dkt Mwakyembe, Dkt Kijaji, Dkt Jasmine Tiisekwa, Dkt Tito Mwinuka (DG wa zamani TANESCO), Dkt Bashiru Ally, Dkt Leonard Chamuriho, Dkt Pudensiana Kikwembe, Prof Adelardus Kilangi, Prof Palamagamba Kabudi na wengine wengi inabidi warudi vyuoni wakafundishe. Huku kwenye practice wawaachie tenure-track practitioners huko wizarani na kwenye taasisi. Kwani kuna shida gani hawa practitioners waiwa promoted wakachukua hizo nafasi za juu ?

Kwani kuna ulazima wa kiasi hicho wa kuwatoa hawa wahadhiri vyuoni ?

Binafsi siamini kama kuna umuhimu wa kiasi hicho (labda kwenye exception kadhaa nitakubali). Ila hawa practitioners waliopo wizarani na

kwenye taasisi kadhaa za serikali wanatosha kushika hizo nafasi.

Nafikiri sauti inatosha.

Ujumbe uwafikie
 
Nakubaliana kabisa.
Hawa wasomi warudi vyuini kuweka msimamo na quality ya elimu, hasa ya juu.

Mpaka tunaona mbele ya macho yetu, Mwenyejiti wa University Council ni mwalimu wa sekondari na mwenyekiti wa jumuiya ya chama, ni aibu kubwa.
 
Kwa hiyo hii PhD ni copy and paste kutokea huko garissa kenya? maajabu haya........mbali na abstract tungependa pia kusoma introducton, objectives, some literature review, methodologies, results and a hint on discussion........
Wazee wa kufukua makaburi mpoo
 
Habari za jioni wana JF,
Awali ya yote nianze kwa kuwapongeza Prof. Mark Mwandosya pamoja na Prof. Sospeter Muhongo juu ya kile walichokieleza dhidi ya wahitimu hawa wapya wa PhD. Pia nimpongeze Prof. William Anangsye , Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na baadhi ya Wahadhiri kama walivyoeleza kwa ufasaha namna ya upatikanaji wa PhD. Tunaomba mamlaka zinazohusika zijitokeze kujibu hoja kwa manufaa mapana na ustawi wa Taifa letu. Sisi wanazuoni:
1. Tunaomba andiko la research proposal la hao wahitimu
2. Tunaomba minutes za kikao za ku-defend research proposal zao
3. Tunahitaji minutes za vikao vya mara kwa kwa mara kati yao na supervisors wao au wabobezi wengine katika idara za shule zao (progress presentation)
4. Tunaomba barua za intention to submit hizo thesis zao
5. Tunaomba report za internal n a external examiners ziwekwe wazi pia
6. Tunaomba barua zenye kuonesha tarehe ya ku-defend kazi zao
7. Tunaomba orodha ya wale waliohudhuria defense zao
8. Tunaomba thesis zao
9 Tunaomba chapisho walau moja kutoka kwa kila mmoja lililochapishwa katika journals zinazotambulika kimataifa.
 
Nafikiri unaweza kubahatika kupata thesis kama watakuwa wameiweka kwenye library ya chuo na journal publications kama zipo.....cha muhimu TCU wafanye evaluation kama UDOM ina capacity ya kufanya enrolment na ku offer undergraduate na graduate degrees based on technical staff competency and experience na namna wanavyokuwa promoted........hilo ni la muhimu sana, vinginevyo hicho chuo kitabaki kutambulika tu hapa tandale.
 
Mh,nyie!🤭
 
Kaka nimekuelewa wanafanya wenye PhD za kweli wavunjike moyo
 
Hapa ukichokonao zaidi yanaweza kuwa ya Ben Sanane,mwamba alioji Phd ya jamaa mpaka leo Mungu ndo anajua kama yu mzima au la
Usiwe na wasi mkuu.
Kutangulia kwa Muumba ni kwa zamu za uhakika.
Aliyempoteza Ben Saanane si ajabu wako pamoja huko majuu lakini upande kusikowaka jua.
 
Yes!
Lazima wasomi mtetee intergrity ya PhD achievements.
La sivyo tutalalamika elimu ya juu imefitinika, kumbe kuna wahadiri wenye PhD za mchongo.
 
Nakubaliana kabisa.
Hawa wasomi warudi vyuini kuweka msimamo na quality ya elimu, hasa ya juu.

Mpaka tunaona mbele ya macho yetu, Mwenyejiti wa University Council ni mwalimu wa sekondari na mwenyekiti wa jumuiya ya chama, ni aibu kubwa.
Usijitie usahaulifu kushangaa huyo unayemwita mwalimu wa secondary kuwa chairwoman wa University Council na hukumshangaa huyohuyo mwalimu alipokuwa Waziri wa Elimu,Sayansi na Technology
 
Unamaanisha nini kusema kitafahamika Tandale wakati international ranking katika vyanzo mbalimbali vinavyoaminika ikiwemo Webomatrics wanaki-rank hicho chuo kuwa ni cha 4 kwa ubora Tanzania mwaka wa tano sasa mfululizo?

Mimi naona ni uzwazwa kukilaumu chuo pekee badala ya kukemea huu upuuzi wa wanasiasa kuingilia taaluma. Nakuapia chuo chochote kile unachokiheshimu hapa Tanzania, hawa vilaza wanasiasa hawashindwi kufanya waliyoyafanya UDOM. Fuatilia records UDSM,MZUMBE na Open University uthibitishe nisemalo.


Pia ukitaka kujua kuwa huu upuuzi unaendekezwa kwa wanasiasa tu basi jaribu wewe kapuku mwenzangu kujiunga PhD hapohapo UDOM uone mziki utakaokutana nao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…