masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,207
- 13,839
Wote wawili si academicians lakini mfano wa mama Kabaka ni mnaya zaidi.Ha ha haa! Niombe radhi, PhD kwa sisi makapuku tunawaachia academicians na researchers. Degree moja tu imenitosha kuniwezesha kumudu maisha japo kwa mbinde.
Back to the main issue! Haya hebu nipe utofauti kati ya hao wawili huku ukizingatia kuwa huyu mwalimu ana-experience zaidi kwenye masuala ya elimu Tz maana ameshakuwa naibu na waziri kamili wa elimu kwa miaka kadhaa.
Huyu Lubuva baada ya kumaliza shahada yake ya kwanza/pili mambo ya elimu hayajawahi kumshughulisha kabisa.
Kama kigezo cha kuwateua hawa wenyeviti wa council vyuo vikuu ni pamoja na experience kwenye mambo ya elimu basi UDOM wamefanya vizuri zaidi ya UDSM.
Lakini kabla ya kwenda mbali hebu tuainishe kwanza power na majukumu ya hawa wenyeviti kwenye vyuo vikuu. Huenda tunachanganya kati ya Chairman/woman of univ council, Chancellor na Vice-chancellor.
Anawezaje kusimamia wana taaluma kiwango cha PhD, kitaaluma huku akiwa na Diploma ya ualimu?