Prof. Mussa Assad: Nilipokuwa ofisini niliomba nyaraka za SGR, Air Tanzania na mradi wa Stiegler's Gorge lakini sikupewa hata moja

Nitamwelewa cag wa zamani kama atazungumzia ripoti yake kuhusu Ndugai vinginevyo ni unafiki tu
 
Jama jama eti kuna viumbe wanamuona Assad kama mnafiki!!! Hivi ni nani aliekua na uwezo wa kumokosoa jiwe akabaki salama ndani ya nchi hii. Hao kina Lisu walikua wanakosoa wakiwa ughaibuni uko, nao ni baada ya kuponea chupuchupu kukutana na izilaeli. Ana familia inamtegemea huyu eti aseme halafu atekwe. Na nyie mnaomuita sasa ivi mnafki mngesema anaichafua serikali acha limtokee ni vigeugeu nyie ili tu mueke jambo liwe kwenye matakwa yenu. Wacha watu wafunguke tumepata uhuruu
 
Binadamu wa sasa ile kitu inaitwa aibu hakuna kabisa.

Yaani mtu anaitisha press kumsuta marehemu ilhali anajua kabisa mhusika hayupo na hataweza kujitetea.
Rais ni taasisi, kwani magu alipokufa alizikwa nayo, si imjibu?

angeongea haya kipindi kile, tunajua nini kingempata..

hamtaki yasemwe, maana mnaona haya mlichokuwa mnakitetea na kumtetea, na pengine ndiyo nyie wanufaika na huo ubadhirifu..

mbona yy alikuwa akisema ya wenzie. embu tulia kwanza
 
Kweli mataga mnaruka na kukanyagana
Disco limeingia maasai, blues wanacheza reggae! 😂 😂 😂
Hakuna rangi tutaacha kuiona.
Looh! Hayati alijua kutumia madaraka yake! Mpaka 40 wanamalizia msiba tutakuwa hatuna hamu naye.

Everyday is Saturday................................😎
 
Binadamu wa sasa ile kitu inaitwa aibu hakuna kabisa.

Yaani mtu anaitisha press kumsuta marehemu ilhali anajua kabisa mhusika hayupo na hataweza kujitetea.
Marehemu hakuwa Marehemu tu Kama ambavyo anavyoweza kuwa jirani yako , Marehemu Alikuwa Raisi wa Nchi , kwa muktadha huo hatuwezi kukaa kimya na kutomjali kwa sababu Nchi yetu Ina Umuhimu mkubwa kuliko huo umarehemu wake Kama kuna madudu aliyo yafanya yanapaswa kuwekwa wazi ili iwe fundisho kwa watu wengine na ili Kama Kuna walio husika wachukuliwe hatua za kisheria ,Taifa Lina Umuhimu mkubwa kuliko umarehemu wa Mtu
 
ana tetea taifa lake hadi tone la mwisho, na huo ndiyo uzalendo hasa wa kuexpose ubadhirifu wa mali ya umma.

kuna kazi zingine hata ukistaafu, bado unahesabika upo kazini
 
Marehemu akifa husingiziwa mengi sababu hawezi kutoka aliko kujitetea. Tutasikia mengi. Kila mtu akijinadibu ohhh matehemu. Marehemu alisema ohh!!!
kama mtu aliyekuwa rais, ila ofisi yake ya taasisi ya urais ipo inaweza kutoa majibu, maana hajazikwa nayo
 
Marehemu akifa husingiziwa mengi sababu hawezi kutoka aliko kujitetea. Tutasikia mengi. Kila mtu akijinadibu ohhh matehemu. Marehemu alisema ohh!!!
Matendo yako ndio yataamua watu wakuzungumzie vipi baada ya Uhai wako , [emoji3]
 
Lilikuwa jitu la Ajabu sana
 
ATCL ilikuwa na madeni makubwa ya huko nyuma pesa zingeingia akaunti ya ATCL zingelambwa zote na wadai wengine wakiwa hewa.Serikali ndio ikazinunua na kuzikodisha kwa ATCL
ndiyo iwekwe wazi tuone, siyo story za vijiweni
 
Unafiki gani wakati alipishana na mkuu alipotaka kuanza kukagua ndege

Bunge lilimuomba akakague ndege, Huko ndiko nyaraka watu wakaficha

Ni mwalimu wako Yes lakini wewe ni kilaza na mpumbavu ulifaulu kwa kujaza makaratasi lakini hukuelewa kitu
Exactly [emoji419]
 
Hilo lizee lilikuwa linaongoza Nchi Kama family yake

Ndio maana Waka mnovichock [emoji3]
 
Hakuna mtu mpumbavu kama Prof. Assad. Kwanza asije kujidanganya kama yuko popular kiasi cha kutumika kuua heshima ya JPM. Ndiyo maana limekaa kama nguruwe pori hata umbo lake. Kwani nani hajuwi kama Assad anamchukia JPM hata kabla hajawa Rais? Huyu si ndiye alisemaga JPM siyo waziri na hafai kwa kuwa ni mjasiriamali wa kisiasa? Pamoja na sigida yake hana Mungu ni mpumbavu fulani.

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Eti niliomba nyaraka nikanyimwa,

Itakua walishazifahamu tabia zake za kupenda kufanya yasiyomhusu ndio maana wakamnyima ,

Ingawa hajasema ni nyaraka zipi ili tujue kama alikua anastahili kupewa ama la.
pale unapo jiita mzalendo, kumbe hutaki wizi na uovu wako uanikwe pale mzalendo wa kweli anapo hoji..

taifa linahitaji watu kama Assad
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…