Hao ndio ma Professor wetu hawana mawazo ya kujenga Taifa ,wanachowaza ni mishahara kwa mwezi. Yeye ni msoni mzuri huwezi sikia anasema ATCL miaka hii tumekula hasara, tufanye hivi tuimarishe shirika letu liwe shirika shindani duniani na tupate faida, ni bora hata watu wa darasa la saba wanaweza wakasimamia kampuni na ikaendelea kuliko hizi ngonjera za ma professor wetu. Leo hii Jirani zetu ethiopia wana sherekea miaka 75 ya shirika lao la ethiopia airways kuwa angani, wanajivunia, sisi Rais kawanunulia watanzania mil60 ndege 8 na zingine 3 ambazo hazijawasili bado hatuwezi kuendesha shirika hili, sasa elimu zetu zinatusaidia nini? kubishana tu mitandaoni?, hivi kweli sisi watanzania tunashindwa kuendesha shirika hili la ATCL? ATCL hatuwezi endesha, TTCL hatuwezi, Reli tuliua tukakimbilia kwenye malori, viwanda tulikula vyote tukakimbilia kuagiza mizigo china, bandari hatuwezi endesha, elimu hatuwezi at the same time kila siku wana post kumlaumu magufuli eti hakuajiri watanzania, mnataka ajira zipi wakati huo hamtaki kusimamia makampuni yetu yakuwe na kuajiri watanzania wengi? hamuwezi kuwaza ajira za ualimu ,nurse na halmashauri tu? ni lazima tujifunze kwa kila aina kusimamia makampuni yetu yakuwe na yatoe ajira kwa watanzania wengi, sasa Professor anaposema ndege ziuzwe anafikiri vijana walioajiriwa ATCL waende wapi? suppliers wachakula ATCL wata muuzia nani? wakala wa tickets ATCL wafanyakazi wake waende wapi?, utakuta mtu ana bwabwaja tu eti hakuna faida, hivi hamuoni chain ndefu ya watanzania wenzetu wanalisha familia zao kwa uwepo wa ATCL?