Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof Mussa Assad ameeleza namna alivyopata taarifa za kutenguliwa kwake katika nafasi hiyo.
“Utenguzi wangu kuna mtu alinipigia simu siku moja kabla kuhusu utenguzi wangu, na saa moja kabla ya taarifa kutoka nikapigiwa simu tena basi nikampa funguo yule dereva wangu yeye akarudi Dodoma mimi nikapanda ndege kurudi Dar” Prof Mussa Assad CAG wa zamani.
Lakini pia siku naenda ofisi ambapo nilikuwa bado ni CAG kwa sababu nilikuwa naondosha tarehe nne lakini nakutana na vijana Ofisi kwangu, vijana wananiambia Profesa huko juu kuna watu na tunahisi hautoweza kuingia ofisi kwako. Ni kawambia no hakuna mtu anaweza kuniingilia leo tarehe 3 nataka kuangalia ofisi yangu kuclose mafails ili kesho niondoe vitu vyangu.
Nikapanda juu gholofa ya 3 naona vijana wawili kwenye mlango wamekaa nikawafuata, jamani vipi haa Profesa sisi tumetumwa tukae hapa na wewe leo usiingie ofisini kwako. Nikasema nani amewatuma? wakajibu sisi tumetumwa na viongozi wetu. Nikauliza hivi kiongozi wako anajuwa leo tarehe 3? Akajibu anajuwa lakini sisi tumeambiwa tukae hapa tusiondoke.
Basi mimi nikawaambia napiga simu sahivi nikashuka chini gholofa ya pili kijana mmoja naye akashuka eh Profesa wewe njoo kesho asubhi hapa utaingia mimi nikamwambia nataka kuingia leo nikampigia simu Chief secretary. Lakini si kutaka kurudi tena juu nikaamua kuondoka zangu kurudi nyumbani kwangu.
Prof Mussa Assad aliteuliwa kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 05, mwezi Novemba 2014 na kuhudumu katika nafasi hii mpaka tarehe 04, Novemba 2019 ambapo muda wake wa utumishi ulimalizika.
Soma Pia:

- Prof. Mussa Assad atoa maoni yake kuhusu Ripoti ya CAG, asikitishwa na yanayoendelea
- Profesa Assad: Nashutumiwa bila ya makosa na naichukulia hatua hiyo ya Bunge kwa utulivu, suala hilo halinisumbui
- CAG Prof. Assad astaafu, Charles Kichere ateuliwa kuwa CAG mpya