Kuna baadhi ya watu, japo tunafurahia kutumia ID zilizofichika, lakini unatamani, tufahamiane. Wewe ni Kaka yangu. Mungu akujalie afya njema na maisha marefu yenye furaha, na amani tele.
Nina Kaka yangu mkubwa, sasa yupo 90, bado ana akili na hekima yake timilifu, alikuwa anaendesha gari, lakini tumemshauri tangu mwakajuzi asiendeshe, lakini bado anafuata ratiba yake ya tangu ujana ya kufanya mazoezi kila siku.
Kaka yangu mwingine ana 80, bado yupo very energetic. Alipata Covid 19 lakini akapona bila kupata complication yoyote. Hii Covid, inategemea sana nna ilivyokujia. Wakati Kaka yangu akipona Covid bila ya kuzidiwa, wala kulala hata siku moja kutokana na hayo mararhi, mtoto wa kakangu mwingine, mwenye 38, aliugua na kupata complication kubwa ya kupumua, akapoteza maisha. Kila Covid ikitamkwa, namkumbuka huyu mtoto wetu. Niishie hapa maana molyo wangu ni mzito sana. Namwba Mungu amjalie pumziko la milele maana jitihada na moyo wake wa kutaka kuwaokoa wengine, huenda ilichangie kuondoka kwake wakati huu.