Prof. Palamagamba Kabudi has admitted on BBC FOCUS ON AFRICA that Azory Gwanda has “disappeared and died”

Prof. Palamagamba Kabudi has admitted on BBC FOCUS ON AFRICA that Azory Gwanda has “disappeared and died”

Akihojiwa na mtangazaji Zuhura Yunus wa BBC, waziri Kabudi amesema Tanzania kuna uhuru wa kutosha wa vyombo vya habari.

Alipoulizwa kuhusu kupotea kwa mwandishi Azory, Prof Kabudi amesema serikali inaendelea na uchunguzi.

Waziri amesema hali ya Kibiti na Mkuranga ilikuwa tete na haijawahi kutokea tangu Tanzania ipate uhuru wake.

Askari wa polisi, viongozi wa serikali za mitaa na viongozi wa chama tawala CCM waliuawa katika kadhia hiyo lakini kwa sasa amani imerejea na hali ni shwari.

Chanzo: BBC Dira ya Dunia!

UPDATES;

Palamagamba has just admitted on BBC FOCUS ON AFRICA that Azory has “disappeared and died”.

WAZIRI wa Mambo ya ndani Palamagamba Kabudi akiri mwandishi wa Habari Azory Gwanda alitoweka na kufariki, ikiwa ni zaidi ya siku 500 tangu kutoweka kwa mwandishi huyo wa habari za uchunguzi.

UPDATES;

Kabudi akana kusema kwamba alithibitisha Azory Gwanda alifariki, zaidi soma;

View attachment 1150947
Mungu anawaona mlioamua kuangamiza maisha ya Azori gwanda.
 
unapomsoma na kumsikiliza Prof.Kabudi kama unamsikiliza Mbowe au Sugu lazima utoke kapa. that man ability is beyond your understanding, hivyo jitahidi kumuelewa zaidi
pamoja na hayo, aliulizwa swali la mtego kwa kudandia lugha ya mdhungu akajifunga mwenyewe.
 
Nilichokisikia Kabudi alichosema na mnukuu "in Rufiji area not only Azory has dissapeared and die"

Wenye kujua lugha ya malikia tutafsirieni kwa kibantu.
 
Nilichokisikia Kabudi alichosema na mnukuu "in Rufiji area not only Azory has dissapeared and die"

Wenye kujua lugha ya malikia tutafsirieni kwa kibantu.
Katika eneo la Rufiji si Azory pekee aliyepotea na kufa
 
July 12, 2019
London, Uingereza

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Prof. Palamagamba Kabudi ametoa taarifa rasmi juu ya kuhuzunishwa na habari zinazosambaa mitandaoni juu ya mahojiano yake na BBC kuhusu mwandishi wa habari Azory Gwanda aliyetoweka.

Prof. Kabudi akiisoma taarifa yake fupi na kwa umakini mkubwa mbele ya kamera, amesema alinukuliwa vibaya katika mahojiano yake na BBC Focus on Africa.

Na ukweli ni kuwa, hakuthibitisha kifo cha Azory Gwanda kutokea na bado vyombo vya usalama vya Tanzania vinaendelea na uchunguzi kufahamu alipo mwandishi Azory Gwanda.

Source : Millard Ayo
 
unapomsoma na kumsikiliza Prof.Kabudi kama unamsikiliza Mbowe au Sugu lazima utoke kapa. that man ability is beyond your understanding, hivyo jitahidi kumuelewa zaidi

Bila shaka na wewe, kama ilivyo kwa Kabudi, umetolewa Jalalani!
 
Akili zemu nyepesi sana..
Mnangangania tafsiri yenu ndio iwe universal..?!

Kusema amepotea na kufa bado ni assumption sababu hakupatikana, sasa nyny vichwa panzi mshatengeneza script..
Wewe naona unachangia mada tu ila hukusikikiliza the actual interview!
 
Nimesoma kichwa cha thread, nikasema kama kapotea, Waziri atajuaje kwamba kafariki?

Nikasema ngoja nisikilize clip nimsikie Waziri.

Nimemsikia Waziri anachemka kama kawaida yake, kakosea jina, anataja Azory Rwanda.

Naona Rwanda imemkaa sana kichwani.

Lakini sijasikia Waziri akisema lolote kuhusu kifo.

Mtoa mada anaweza kutupa uhakikisho kwamba hiyo habari ya kifo kusemwa na Waziri ni ya kweli na si ya kutungwa tu?
hukusikia maneno: “DISPPEARED AND DIED”?
 
Nimemuona katika kipindi cha Focus on Africa akihojiwa na Peter Okoche; the guy seems to be an incorrigible liar! Alipoulizwa kuhusu magazeti na vituo vya radio kufungiwa alikana na kudai kuwa ni gazeti moja tu, The Citizen ndiyo iliyopata kufungiwa; tena kwa wiki moja! Kwa hiyo kulingana na waziri wetu Mseto, Mwanahalisi, Mawio, nk yamejifungia yenyewe! Incredible.
Mnapoquote mje na evidences, msije kijinga as if ni chadema. Prof alimuuliza mwandishi nipe evidence ni gazeti lipi limefungiwa tofauti na alilolitaja, mwandishi zuhura yunus hakutaja. Pia prof hajasema kuwa mwandishi alikufa. Labda kingereza hamjui nyie watu. Prof aliulizwa kuhusu mwandishi kupotea alichoongea ni general hakutaja mtu mmoja amesema waliopotea na kuuawa so hajajustfy kuwa mwandishi aliuliwa
 
Nimesikiliza mahojiano yote. Hajasema Azory ameuawa, ametumia utetezi ambao si mgeni toka matukio hayo yatokee.

Wengi mnaopiga kelele na kumbeza Prof Kabudi mngewekwa kwenye nafasi yake mngeongea hivyo hivyo. Wengine kwenye taasisi zenu huko ni waoga na waunga mkono juhudi wakubwa lakini ukishaingia kwenye fake ID ndio unajifanya kushangaa wengine.

Nimeangalia video yote wala haina mjadala mpya. Alafu tukumbushane uchaguzi wa serikali za mitaa unanukia, jamaa zetu wapo wapo tu alafu baadae watalia na wizi wa kura.
Umeandika ujïnga mtupu
 
Mnapoquote mje na evidences, msije kijinga as if ni chadema. Prof alimuuliza mwandishi nipe evidence ni gazeti lipi limefungiwa tofauti na alilolitaja, mwandishi zuhura yunus hakutaja. Pia prof hajasema kuwa mwandishi alikufa. Labda kingereza hamjui nyie watu. Prof aliulizwa kuhusu mwandishi kupotea alichoongea ni general hakutaja mtu mmoja amesema waliopotea na kuuawa so hajajustfy kuwa mwandishi aliuliwa
Acha unafiki.....disappeared and died Hujui tafsir hii
 
Mnapoquote mje na evidences, msije kijinga as if ni chadema. Prof alimuuliza mwandishi nipe evidence ni gazeti lipi limefungiwa tofauti na alilolitaja, mwandishi zuhura yunus hakutaja. Pia prof hajasema kuwa mwandishi alikufa. Labda kingereza hamjui nyie watu. Prof aliulizwa kuhusu mwandishi kupotea alichoongea ni general hakutaja mtu mmoja amesema waliopotea na kuuawa so hajajustfy kuwa mwandishi aliuliwa
Kuna mpaka transcripts watu wameweka hapa, profesa kasema Azory na wenzake who "disappeared and died".

Maana yake wamepotea na kufa, si wamepotea au kufa.

Maneno "na" au "au" yanabadilisha kabisa maana.
 
Nimeshindwa kuconclude hii kashfa kwa serikali ya kuhusiana na usalama wa watu wake kwa kwa kauli hii alio itoa huyu profesa ya kusema it is not only personal disappeared and died mkuranga Rufiji kuna hoja mbili kwa member wezangu wazitafakali huwenda majibu yatapatikana kwa vile wakati unavyo onyesha
Kwanza kwanini ameweza kudhibitisha kuwa uwenda azory ngwanda ame kufa na wengine hi hali mwili wa marehemu hatujauona
Pili kwani baada ya mazungumzo yake .kwa lugha ya kimombo kwanini alikana maneno yake kunani kwa hili
Na mwisho niwape pole kwa wale wote waliopoteza ndugu na jamaa katika ile ajali ya Coaster ilikuwa inatoka dar es Salam kueleke chato mkoani geita tukio lilipotokea kati ya barabara ya singida na igunga.
 
Akihojiwa na mtangazaji Zuhura Yunus wa BBC, waziri Kabudi amesema Tanzania kuna uhuru wa kutosha wa vyombo vya habari.

Alipoulizwa kuhusu kupotea kwa mwandishi Azory, Prof Kabudi amesema serikali inaendelea na uchunguzi.

Waziri amesema hali ya Kibiti na Mkuranga ilikuwa tete na haijawahi kutokea tangu Tanzania ipate uhuru wake.

Askari wa polisi, viongozi wa serikali za mitaa na viongozi wa chama tawala CCM waliuawa katika kadhia hiyo lakini kwa sasa amani imerejea na hali ni shwari.

Chanzo: BBC Dira ya Dunia!

UPDATES;

Palamagamba has just admitted on BBC FOCUS ON AFRICA that Azory has “disappeared and died”.

WAZIRI wa Mambo ya ndani Palamagamba Kabudi akiri mwandishi wa Habari Azory Gwanda alitoweka na kufariki, ikiwa ni zaidi ya siku 500 tangu kutoweka kwa mwandishi huyo wa habari za uchunguzi.

UPDATES;

Kabudi akana kusema kwamba alithibitisha Azory Gwanda alifariki, zaidi soma;

View attachment 1150947
Rufiji area...dissapeared and died.....

The level of conviction and assurance over the matter🙌🏽🙌🏽🙌🏽

RIP Azory
 
Back
Top Bottom