Prof. Palamagamba Kabudi has admitted on BBC FOCUS ON AFRICA that Azory Gwanda has “disappeared and died”

Prof. Palamagamba Kabudi has admitted on BBC FOCUS ON AFRICA that Azory Gwanda has “disappeared and died”

Akihojiwa na mtangazaji Zuhura Yunus wa BBC, waziri Kabudi amesema Tanzania kuna uhuru wa kutosha wa vyombo vya habari.

Alipoulizwa kuhusu kupotea kwa mwandishi Azory, Prof Kabudi amesema serikali inaendelea na uchunguzi.

Waziri amesema hali ya Kibiti na Mkuranga ilikuwa tete na haijawahi kutokea tangu Tanzania ipate uhuru wake.

Askari wa polisi, viongozi wa serikali za mitaa na viongozi wa chama tawala CCM waliuawa katika kadhia hiyo lakini kwa sasa amani imerejea na hali ni shwari.

Chanzo: BBC Dira ya Dunia!

UPDATES;

Palamagamba has just admitted on BBC FOCUS ON AFRICA that Azory has “disappeared and died”.

WAZIRI wa Mambo ya ndani Palamagamba Kabudi akiri mwandishi wa Habari Azory Gwanda alitoweka na kufariki, ikiwa ni zaidi ya siku 500 tangu kutoweka kwa mwandishi huyo wa habari za uchunguzi.
View attachment 1150947
Amejuaje kwamba kafariki?Mimi ni mwana CCM,naipenda nchi yangu na serikali ya awamu ya tano,lakini haya mambo siyapendi kabisa.Yanaleta ukakasi na yanakichafua chama na serikali sana.Tatizo ni kwamba wema huwa hauvumi,ubaya ndio unaovuma.
 
Wasio julikanawatajitambulisha tu wenyewe.
Kumbe wanajua kuwa alisha kufa lakini wanatuambia hawajui aliko. Damu ya mtu mbaya sana haijawahi acha mtu salama. Watajitaja wote bila wao kujitambua kuwa wanatajana.
 
Aiseee porofesa kabugi hapo alipotumia "and" kwenye ishu ya Azory..angetumia "or" wala huu uzi usingepandishwa hapa. Nadhani angesema [In the rufiji area, it is not only Azory who has disappeared OR died] ila aliposema "In the rufiji area, it is not only Azory who has disappeared AND died" hapo ndo ukakasi ulipoanzia....facial expression ya mwandishi tho.....mmmmhhh...Kabudi weeeee....Kama namuona Jiwe.
Hakika!
 
Palamagamba kaonyeshe wapi mlitupa mwili wa Azory
Huu muziki utaucheza kwa visigino
Mmezoea kuona WaTz mabwege leo ulimi umeteleza
Hahahhh reshuffle inakuja waziri
Mmetoboa siri
 
Nadhani kiingereza bado ni lugha ngumu kwetu kama si hivyo mnapotosha makusudi. Hakuna sentensi ambayo waziri amesema azory amekufa. Mwandishi amemuuliza yupo wapi azory Gwanda? Waziri amejibu kiujumla kwamba, MKIRU ni moja kati ya matukio mabaya ambayo nchi iliipata toka tumepata uhuru, viongozi wa serikali za mtaa, viongozi wa CCM, na polisi waliuwawa. Serikali inafanya jitihada kuzuia matukio kama hayo kuendelea maeneo mengine nchini.

Japo najua pro kabudi hapendwi na baadhi ya watanzania, il kwasasa nchi imepata FM bora kabisa kuwahi kutokea

The irreplaceable
Utakua na wewe ni wale waliookotwa jalalani, wapumbavu wenye kujipendekeza.
 
Umesikia hivyo tu?
Itendee haki nafsi yako ndugu mtanzania, upotoshaji hautosaidia taifa hili bali kujaza chuki zisizo sababu..
Ukisha jilisha upepo Wa aina hii kisha unarejeshaje maisha ya hao watu waliopotea na kufa mkiru?
Nimesikia akitoa maelezo mengi kuhusu kuuawa kwa watu wengi akiwemo Azory Gwanda.

Una swali lingine ?
 
Mimi sipo kumtetea mtu yeyote. Natetea ukweli.

Nimesikiliza clip lakini sijasikia Waziri aliposema khusu kufariki.

Unaweza kutuwekea clip hiyo tumsikie Waziri mwenyewe anaongea kuhusu kufariki?

Jambo hili ni muhimu. Kwa sababu kama Waziri kasema habari za kufariki, tunataka tumbane, amejuaje habari za kwamba mtu aliyepotea amefariki?

Tuwekee clip ya Waziri kusema habari ya kufariki.
Umepata wasaa wa kusikiliza mahojiano yake na Zuhura Yunus kwa lugha ya kiswahili ?
 
unapomsoma na kumsikiliza Prof.Kabudi kama unamsikiliza Mbowe au Sugu lazima utoke kapa. that man ability is beyond your understanding, hivyo jitahidi kumuelewa zaidi
maneno hayo hayawezi kutoka kwa mtu makini na guru la sheria Tanzania kwa sababu anajua kabisa yatamhukumu. Jaribu upotoshaji mwingine
Hii ndiyo statement ya Kabudi mwenyewe:
IN THE RUFIJI AREA, IT IS NOT ONLY AZORY RWANDA, AAAHHH, AZORY, WHO HAS DISSAPEARED AND DIED
kama angekuwa kasema WHO HAS DISSAPEARED OR DIED au kama angesema tu WHO HAS DISSAPEARED. Hapo mbona kusingekuwa na shida? hiyo DISSAPEARED AND DIED, hapo anaongelea wale ambao wamepotea na kuthibitishwa kwamba wamekufa, na ni katika kundi hilo Palamagamba anamuweka Azory.
Hapo Kabudi alitakiwa kuomba radhi kwa kuteleza ulimi, lakini siyo kutoa visingizio. alichoongea kina maana hiyo kwamba Azory kapotea na amethibitishwa kuwa amekufa. sasa wewe ndio hujui lugha ila UNA MAHABA YANAYOKUTIA UKIZIWI
 
Back
Top Bottom