Prof. Safari: Kuna haja ya kufungua kesi kuhoji uhalali wa Wabunge 19 wa Viti Maalum CHADEMA

Prof. Safari: Kuna haja ya kufungua kesi kuhoji uhalali wa Wabunge 19 wa Viti Maalum CHADEMA

Hapa unaonyesha upumbavu wako. Umeniona nikiwa CHADEMA?
Nilikujibu nikidhani kichwani zimo kumbe ni mmoja wa walewale wanaoshinda hapa JF ili mradi waende chooni?

Usitafute kuendelea kujibizana na mimi, huwa sina muda na wapuuzi wa aina yenu.
Ungekuwa ni mwerevu kama usemavyo usingeongelea usichokijua...kisa tu kimekujia KICHWANI....
 
Ungekuwa ni mwerevu kama usemavyo usingeongelea usichokijua...kisa tu kimekujia KICHWANI....
Uliponipachika uanachama wa chama ulijiona wewe ni "mwerevu"? Hukujiandikia "usichokijua... kisa tu kimekujia KICHWANI"?
Kama wewe sio mpuuzi nikupe jina gani?
 
Uliponipachika uanachama wa chama ulijiona wewe ni "mwerevu"? Hukujiandikia "usichokijua... kisa tu kimekujia KICHWANI"?
Kama wewe sio mpuuzi nikupe jina gani?
Nilikupachika baada ya kutoonyesha huo werevu uliojidai nao kwa kumchafua mtu kuwa anatumiwa na kutumika......
 
... kuna shida! Umeshavuliwa uanachama halafu unajitambulisha kwa jina la chama kilichokuvua uanachama; sio sahihi. Chadema hawana shida na ubunge wao; kisichotakiwa ni wao kujitambulisha kama wanachama wa Chadema. Membe alivuliwa uanachama wa CCM na ukakoma muda ule ule; vivyo hivyo kwa Sofia Simba, na wengine wengi!
Walijitambulisha wana chadema bfr kuvuliwa uanachama wao

Wakienda bungeni hawatoongea lolote kuhusu chadema
 
Mahakamani?matokeo hayatakua tofauti na kesi ile ya mwambe
 
Ibara hiyo ya katiba inasema mtu atapoteza ubunge iwapo “ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa mbunge”.
Huko mahakamani watatafsri kwamba hakuna mbunge aliyeacha bali alichishwa na hivyo kufunga kesi.
 
Wakili wa kujitegemea, Profesa Abdallah Safari ameishauri CHADEMA kwenda mahakamani kuomba tafsiri ya uhalali wa ubunge wa makada 19 wa chama hicho walioadhibiwa baada ya kwenda kuapa kuwa wabunge wa viti maalum na kutotokea mbele ya Kamati Kuu kujieleza.

Wanachama hao, ambao ni pamoja na mwenyekiti wa Baraza la Wanawake (Bawacha), Halima Mdee waliapishwa Novemba 24 wakati kukiwa na utata wa barua iliyopelekwa Tume ya Uchaguzi (NEC) kuhusu uteuzi wa wabunge wa viti maalum, baada ya katibu mkuu wa Chadema, John Mnyika kusema hakuiandika wala Kamati Kuu haikukutana kupitisha orodha.

Kitendo hicho kiliifanya Chadema iwate mbele ya Kamati Kuu kujielezas, lakini wote hawakutokea na hivyo chombo hicho kufikia hatua ya kuwavua uanachama, lakini Spika Job Ndugai alisema hatatambua uamuzi huo aliodai wa kuonea wanawake baada ya kuhukumiwa bila ya kusikilizwa.

Nafasi za viti maalum ni za vyama ambavyo hupata zaidi ya asilimia tano ya kura za wabunge, tofauti na za ubunge wa jimbo ambazo hupatikana kutokana na vyama humdhamini mgombea.

“Kama wataenda bungeni, njia pekee ni kuomba tafsiri ya mahakama ili chombo hiki kiseme katika mazingira haya ibara ya 71 (1) f hawa ni wanachama halali,” alisema Profesa Safari, ambaye amebobea katika sheria.

Ibara hiyo ya katiba inasema mtu atapoteza ubunge iwapo “ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa mbunge”.

Profesa Safari, aliyewahi kuwa makamu mwenyekiti wa Chadema kuanzia 2014 hadi 2019, alisema kuna haja ya kufungua kesi kupata tafsiri kama Mdee na wenzake bado ni wabunge halali baada ya Kamati Kuu ya Chadema kuwavua uanachama.

“Mahakama ndiyo ina haki ya kutafsiri,” alisema.

Profesa Safari alisema suala la Mdee na wenzake kufukuzwa Chadema lipo wazi kwa mujibu wa ibara ya 71 (1) (f) ya Katiba ya jamhuri ya Muungano inayoeleza kuhusu mbunge kufukuzwa uanachama na pia sifa za kugombea zinazoelezwa katika ibara 67 (1)b, inayotaka mgombea ubunge apendekezwe na chama chake.

“Dhana ya kuwa na chama ni muhimu. Ukishatimuliwa huwezi ukakingikiwa kifua na mtu yeyote. Bahati nzuri matukio yametokea mara nyingi sana. Wakati wa Tanu walifukuzwa kina Anangisye, halafu wabunge wa CUF walitimuliwa. Mara nyingi tu (haya yanatokea),” alisema Safari.

Pia alielezwa kushangazwa na kitendo cha Spika kuwatetea makada hao akihoji wameanza urafiki lini.
Naona viongozi wa Chadema wazingatie ushauri huu. Pamoja na mahakama kutoaminika kuwa huru, lakini kumbukumbu itakuwa imewekwa hata swala hili likitupwa. Pia ninawashauri Chadema wawafukuze wote walioapishwa akiwemo mbuge wa Nkasi pamoja na wale madiwani.
 
Mahakamani kufanya nini? Huko ni kupoteza muda. La kufanya ni haya:

1) Report kesi ya jinai polisi na sema hao watu wamefoji documents, nembo, signature ya Katibu na muhuri wa ofisi. Haijalishi kama Mambosasa ataact ama la, chadema wao watimize wajibu wao

2) Peleka barua kwa Msajiri wa Vyama kumwambia hao watu wamefutwa uanachama

3 Teua wanawake wengine 19 na peleka majina yao sehemu husika. Maelezo kwamba uchaguzi huu haukubaliki na kwamba eti kuteua ni kubariki haramu ni mtazamo finyu. Kwanini Aida Khenani yupo Bungeni kwa baraka zote kama uchaguzi hautambuliki?

Kuna kigugumizi gani kufanya angalau jambo moja kati ya haya? Hii tabia ya kulialia kwenye social media bila kuchukua hatua stahiki ni dalili ya uzwazwa - unless ofcourse chama kina maslahi na hao 19
 
CDM tabu yote hii ya nini?? Maamuzi yenu ni kwamba mmeshawavua uanachama, kwanini mnateseka ?
Wananchi wameshawashitukia kwa taarifa yenu
Ni heri mkubali tu mapema raia waanze kuzoea kulikoni mje mkubali mwishoni na vidonda havitapona (muwaruhusu hao covid19 sababu mlikubaliana wenyewe,msicheze na akili zetu)
Mi sina uchama lakini kuna wachangiaji wengine wanafikiria kutumia down under
 
kumbuka kote huko unakopeleka mashitaka ni wana CCM kidakindaki - ambao wanajua lengo lao ni nini hasa.. unaweza kupeleka docs za fojare kwa Msajiri akakwambia hapokei hadi upite Police, ukifika police unaswekwa ndani kwaza - kosa umepata wapi nembo ya adamu na hawa... ukiwa huko unapewa kesi ya utakatishaji wa fedha... hadi utoke uchaguzi wa 2025 unakaribia..
 
Profesa Safari huwa namkubali sana.
Yuko vizuri sana na hili jambo kalielezea vizuri sana kuliko hata lilivyowakilishwa hapa. Ungepata kumsikiliza wakati analielezea hili amesema kina mdee wamejidhalilisha wenyewe kisiasa na hili ndio litakuwa anguko lao Kama hawataomba radhi kwa wanachadema na kamati kuu. Wanapoenda kukata rufaa maana ake wana nia ya kuendeleza huu mjadala wakiamini wako sahihi.
 
kumbuka kote huko unakopeleka mashitaka ni wana CCM kidakindaki - ambao wanajua lengo lao ni nini hasa.. unaweza kupeleka docs za fojare kwa Msajiri akakwambia hapokei hadi upite Police, ukifika police unaswekwa ndani kwanza
Kaka, normally you cross the bridge ukilifikia. Hizi assumptions hazitakiwi kuzuia watu kuchukua hatua.
 
Mi sina uchama lakini kuna wachangiaji wengine wanafikiria kutumia down under
Nilitaka nimjibu huyu jamaa uliyemquote Ila nikajiridhisha kuwa wengine haeatumii vichwa kufikiri.
 
U
CDM tabu yote hii ya nini?? Maamuzi yenu ni kwamba mmeshawavua uanachama, kwanini mnateseka ?
Wananchi wameshawashitukia kwa taarifa yenu.

Ni heri mkubali tu mapema raia waanze kuzoea kulikoni mje mkubali mwishoni na vidonda havitapona (muwaruhusu hao covid19 sababu mlikubaliana wenyewe,msicheze na akili zetu)
Nawe unajiita great thinker eti?!!
 
Katiba ya Nchi INAVUNJWA ili kumfurahisha huyo anayejiita Mwendawazimu na udikteta wake halafu wewe huoni shida yoyote? Akili za wapi hizi!? 😳
Shida yote ya nini?

Kama ni uanachama tayari wamewavua.

Na kama nafasi za ubunge Chadema haizitaki Sasa mapambano hayo ya kila siku kwa ajili ya nn?
 
Mpaka sasahivi hao siyo wanachama wa CHADEMA
... Chadema wanasema wasaliti sio wanachama wao na ni kweli wako sahihi; kwa upande mwingine wao (wasaliti) wanasema wao ni wanachema wa Chadema na wanajitambulisha hivyo na wanakubalika hivyo (kama wanachama wa Chadema) Bungeni na wanaingia mule kwa tiketi ya Chadema! Lazima kuwe na namna ya kuwazuia wao na wanaowapa sapoti kujitambulisha kama wanachama wa Chadema.
 
Walijitambulisha wana chadema bfr kuvuliwa uanachama wao

Wakienda bungeni hawatoongea lolote kuhusu chadema
... sio suala la wao kuongelea lolote kuhusu Chadema bali kutambulishwa kama wanachama wa Chadema. Kumbuka kwenye ile press yao baada ya kuvuliwa uanachama walijitambulisha wakiwa na mavazi rasmi ya Chadema; mmeshavuliwa uanachama attire za Chadema za nini tena?
 
Back
Top Bottom