Prof. Safari: Tume ya Warioba ifikirie kuingiza mahakama ya kadhi ndani ya katiba mpya

Prof. Safari: Tume ya Warioba ifikirie kuingiza mahakama ya kadhi ndani ya katiba mpya

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
9,524
Reaction score
13,682
Akihitimisha hoja zake katika kipindi cha this week in perspective kinachoongozwa na Adam Simbeye (TBC) leo usiku saa 4 tarehe 14/06/2013, Prof. Safari amesema kuna mambo mawili yanayosababisha kutokuelewana miongoni mwa watu duniani; migogoro ya kidini na kugombea rasilimali.

Hivyo ili kuliepusha taifa la Tanzania katika migogoro ya kidini ni budi tume ya mabadiliko ya katiba inayoongozwa na Jaji Warioba ione uwezekano wa kuingiza mahakama ya kadhi katika rasimu ya katiba mpya! Kwa maoni yake ni kwamba nchi zote zinazotuzunguka zimeanzisha mahakama hizo, hivyo Tanzania haiwezi ikawa tofauti! Suala hili ni kwa maslahi ya ustawi wa Tanzania!

Jadili!
 
Mtei atamvua uanachama shauri yake! Ukiwa huko ni Marufuku, Strictly prohibited kutetea Waislam ikibidi unaruhusiwa kuwa Wakili wa Serikal kwa muda, Slaa kwenye ishu ya Sensa na MOU alijikabidhi kazi ya kuwa mtetezi wa serikal, namshauri huyo Prof kuhakikisha vigezo na masharti ya kuwa huko vinazingatiwa!
 
me naona sawa manake itasaidia kupunguza msongamano wa kesi mahakani pia hao ndio watatoa haki kwa usawa maana mahakama zetu haziko fair kabisa yani.
 
Unafki ni kitu kibaya sana..hayoni maoni ya Profesa sasa cdm imefata nini hapa.
Mtei atamvua uanachama shauri yake! Ukiwa huko ni Marufuku, Strictly prohibited kutetea Waislam ikibidi unaruhusiwa kuwa Wakili wa Serikal kwa muda, Slaa kwenye ishu ya Sensa na MOU alijikabidhi kazi ya kuwa mtetezi wa serikal, namshauri huyo Prof kuhakikisha vigezo na masharti ya kuwa huko vinazingatiwa!
 
Serikali ya ccm ilishasema suala la dini lifanywe na dini yenyewe! Sasa mambo ya kuweka kwenye katiba itakuwaje...
Catholic nao wana mahakama yao mbona haipo kwenye katiba...

Kwanza kiislam si sawa kupokea hela haram za kodi ya makafiri, kitimoto,pombe, sigara, dhuluma,wizi
 
Sheria za dini haziwezi kuingizwa kwenye katiba kwasababu Tanzania sio nchi ya dini moja. Hivyo mahakama zifanye kazi kwenye sehemu za ibada na si kwenye serikali katiba haiwezi kuwa na sheria mbili tofauti na serikali ni lazima iwe na mfumo mmoja wa sheria. Mfano mambo ya ndoa yanaweza kutatuliwa na makanisa na misikiti lakini kuna sheria ya katiba ambayo haina dini. Kuweka sheria za dini kwenye katiba zitaongeza vurugu kwasababu Watanzania wengi wana dini lakini mila na desturi ndiyo ziko zaidi kwenye maisha ya watu kuliko dini.
 
Serikali ya ccm ilishasema suala la dini lifanywe na dini yenyewe! Sasa mambo ya kuweka kwenye katiba itakuwaje...
Catholic nao wana mahakama yao mbona haipo kwenye katiba...

Kwanza kiislam si sawa kupokea hela haram za kodi ya makafiri, kitimoto,pombe, sigara, dhuluma,wizi

Unaposema Katoliki wana Mahakama yao unamaanisha nini? Mahakama ya Katoliki si ndiyo hii tunayoitumia wote?,
 
CCM haikubali mahakama za kadhi! Chadema pia haitaki! Waislamu wanasubiri chama kinachokubali mahakama ya kadhi ili wapate kura zao! CCM na Chadema msimamo wao ni mmoja!
 
Unaposema Katoliki wana Mahakama yao unamaanisha nini? Mahakama ya Katoliki si ndiyo hii tunayoitumia wote?,[/QUOTE]

Hapana, Katoliki wanayo mahakama yao nje ya hii ya ki-secular.
 
Hahahha sasa hivi watamgeuka prof safari ngoja waamke kesho utaona povu lao hapa,na wataokuja kumpiga safari sio wafuasi wa ccm ni hao hao wenzake,rangi ya cdm bwana huwa haijifichi kwenye masuala kama haya,
 
Ni vizuri Watanzania kujifunza kusikiliza maoni ya watu wengine. Mimi si Muislam lakini siwezi kamwe kukimbilia kusema kuwa ni wazo baya kama sina ufahamu wa kutosha kuhusu maoni yaliyotolewa.

Naamini hakuna mtu anayepinga uanzishaji wa Mahakama ya Kadhi, mjadala mkubwa ilikuwa iendeshwe kwa gharama ya nani, serikali au waislam wenyewe? Wengi tungependa kusema iendeshwe kwa gharama za Waislam wenyewe, lakini hizo kesi za Mirathi na Ndoa, za waumini wa kiislam ambazo sasa zinaenda kwenye mahakama za kawaida, zinagharamiwa na nani? Serikali au Waislam?

me naona sawa manake itasaidia kupunguza msongamano wa kesi mahakani pia hao ndio watatoa haki kwa usawa maana mahakama zetu haziko fair kabisa yani.
 
Unaposema Katoliki wana Mahakama yao unamaanisha nini? Mahakama ya Katoliki si ndiyo hii tunayoitumia wote?,
Haha..hiyo tunayotumia ina misingi iliyoichukua ktk ustaarabu uliozaliwa chini ya tamaduni za Rome.Ila si zitumikazo katoliki leo.
 
Unaposema Katoliki wana Mahakama yao unamaanisha nini? Mahakama ya Katoliki si ndiyo hii tunayoitumia wote?,
very iiresponsible..logic yake ya kwamba mataifa mengine yameweka ,sijui akisikia mataifa jirani yote yamepitisha ushoga,nao atawakatalia kutumia sababua hiyohiyo? Hawezi kuwa serious hata kama ni maoni binafsi...anajua kila kundi likitaka sheria hakutakua na sababu ya kuwanyima,mwishowe kila mtu atakuwa ana sheria yake,sijui matataizo ya watu wa dini tofauti watahukumiwa na sheria gani? Kwanini waislam wanataka nguvu ya sheria ya dunya,na si nguvu Mungu na hofu ya muumini kwa Mungu.Waumini waipendayo dini yao.wataheshimu sheria na kukubali adhabu wa moyo mmoja.
 
Mtei atamvua uanachama shauri yake! Ukiwa huko ni Marufuku, Strictly prohibited kutetea Waislam ikibidi unaruhusiwa kuwa Wakili wa Serikal kwa muda, Slaa kwenye ishu ya Sensa na MOU alijikabidhi kazi ya kuwa mtetezi wa serikal, namshauri huyo Prof kuhakikisha vigezo na masharti ya kuwa huko vinazingatiwa!

Chadema inaunga mkono mahakama ya kadhi iendeshwe na waislam wenyewe sio na serikali inayotegemea kodi kwenye Bia, Sigara, Kondom, Guest houses, mabucha ya nguruwe n.k...Kwa kutaka Serikali iiendeshe hiyo mahakama ni kuinajisi.

Wabilah Tawfiq,
Mzito Kabwela
 
Profe Lipumba + Profe Safari =?????
 
very iiresponsible..logic yake ya kwamba mataifa mengine yameweka ,sijui akisikia mataifa jirani yote yamepitisha ushoga,nao atawakatalia kutumia sababua hiyohiyo? Hawezi kuwa serious hata kama ni maoni binafsi...anajua kila kundi likitaka sheria hakutakua na sababu ya kuwanyima,mwishowe kila mtu atakuwa ana sheria yake,sijui matataizo ya watu wa dini tofauti watahukumiwa na sheria gani? Kwanini waislam wanataka nguvu ya sheria ya dunya,na si nguvu Mungu na hofu ya muumini kwa Mungu.Waumini waipendayo dini yao.wataheshimu sheria na kukubali adhabu wa moyo mmoja.

Mkuu kuna kitu watanzania wakiislam wanachanganya. Population ya Waislam Uganda na Kenya ni very minimal kiasi kwamba hata ukiruhusu matakwa yote ya waislam nchi haitavurugika. Huku kwetu ni tofauti. Ni kama Nigeria. Tupo karibu idadi sawa. Sasa Serikali lazima iwe makini yasitokee ya Nigeria au Sudan kiasi cha nchi kugawanywa ingawa kwa Sudan udini was not the case lakini ulikuwepo. Ni sawa huku kwetu mabudha waseme wanataka mahakama yao...ukiwaruhusu hutaona kelele kwakuwa ni kundi dogo sana
 
Back
Top Bottom