Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Profe Lipumba + Profe Safari = janga la la wakristo na wapaganiProfe Lipumba + Profe Safari =?????
Bahati mbaya sikuona jinsi Prof. Safari alivyoainisha hoja zake. Hilo ndio la msingi. Kwa nini mahakama ya kadhi iwe kwenye katiba - ningependa kujua hoja zake ni zipi. Lakini hili la kusema nchi zinazotunguka zina mahakama ya kadhi katika katiba zao peke yake haina mashiko. Kuna vitu vingi wanavyo sisi hatuna au sisi tunavyo wao hawana. Yote ni kufuatana na hali halisi ya kila nchi. Kimsingi hakuna anayekataa mahakama ya kadhi kwa sasa. Tatizo lilipo ni kwamba nani ainzishe na iendeshwe kwa gharama ya nani. Hata kama ikianzishwa kwa sasa, nahisi kunaweza kutokea mtafaruku mkubwa kati ya BAKWATA na akina Ponda. Pengine ni vizuri kuanza kuweka vizuri mgogoro wa muda mrefu kati ya taasisi mbalimbali za kiislamu.Akihitimisha hoja zake katika kipindi cha this week in perspective kinachoongozwa na Adam Simbeye (TBC) leo usiku saa 4 tarehe 14/06/2013, Prof. Safari amesema kuna mambo mawili yanayosababisha kutokuelewana miongoni mwa watu duniani; migogoro ya kidini na kugombea rasilimali.
Hivyo ili kuliepusha taifa la Tanzania katika migogoro ya kidini ni budi tume ya mabadiliko ya katiba inayoongozwa na Jaji Warioba ione uwezekano wa kuingiza mahakama ya kadhi katika rasimu ya katiba mpya! Kwa maoni yake ni kwamba nchi zote zinazotuzunguka zimeanzisha mahakama hizo, hivyo Tanzania haiwezi ikawa tofauti! Suala hili ni kwa maslahi ya ustawi wa Tanzania!
Jadili!