Prof. Safari: Tume ya Warioba ifikirie kuingiza mahakama ya kadhi ndani ya katiba mpya

mbna waislamu tushaelewa huyo prof safari anataka kutuchanganya, haiwezekan pesa inayotokana na pombe, nguruwe, riba na hata makafiri ikaendesha mahakama zetu.
 
Professor, mambo yanayohusu dini, iwe ya kikristo, kiislam, nk yagharamiwe na dini husika na tena yawe nje ya katiba. Usiwafanye wale ambao siyo wa dini yako kuwa ni wajinga yahee.
 
Bahati mbaya sikuona jinsi Prof. Safari alivyoainisha hoja zake. Hilo ndio la msingi. Kwa nini mahakama ya kadhi iwe kwenye katiba - ningependa kujua hoja zake ni zipi. Lakini hili la kusema nchi zinazotunguka zina mahakama ya kadhi katika katiba zao peke yake haina mashiko. Kuna vitu vingi wanavyo sisi hatuna au sisi tunavyo wao hawana. Yote ni kufuatana na hali halisi ya kila nchi. Kimsingi hakuna anayekataa mahakama ya kadhi kwa sasa. Tatizo lilipo ni kwamba nani ainzishe na iendeshwe kwa gharama ya nani. Hata kama ikianzishwa kwa sasa, nahisi kunaweza kutokea mtafaruku mkubwa kati ya BAKWATA na akina Ponda. Pengine ni vizuri kuanza kuweka vizuri mgogoro wa muda mrefu kati ya taasisi mbalimbali za kiislamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…