Kama kweli Serikali ya Tanganyika ina nia njema na Zanzibar na kuamini juu ya misingi ya Muungano wenye maslahi ya pamoja na fursa sawa (win - win situation) na kwamba Zanzibar inafaidika na mfumo wa Muungano uliopo ! SUALA:
Je, Serikali ya Tanganyika iko tayari katika kufuata mfumo na utaratibu huo huo iliyouasisi kwa kuona Zanzibar ambayo ni mbia na mshirika wake - inafutika, na badala yake ii...ngie ndani ya Serikali ya Muungano kama vile ilivyo sasa Tanganyika ndani ya Serikali ya Muungano? Yaani tuwe na Serikali ya Tanganyika na ile ya Muungano badala ya kuwa na Serikali ya Zanzibar na ile ya Muungano.
Na kwamba Makao Makuu ya Serikali ya Muungano yawe Zanzibar?
Na kwamba Tanganyika ipate 4.5% katika mgao wa mambo ya Muungano kama inavyopata sasa Zanzibar?
Na kwamba Tanganyika kwa kipindi cha miaka 48 isiwe na: Polisi yake, usalama, usafiri wa anga, bandari, leseni za viwanda, ushirikiano wa kimataifa, utafiti, takwimu, ushuru wa bidhaa, kodi ya mapato, biashara za nje, simu, posta, elimu ya juu, mafuta na gesi asilia, uraia, uhamiaji, Mahakama ya rufaa, mambo ya nje, mikopo ya nje, sensa ya watu na baraza lake la mitihani - na kwamba yote haya yawe chini ya mamlaka ya Zanzibar? Kwann hamkubali tubadilishane kwa utaratibu huo muliouweka?