Halafu ngoja kwanza, hivi udiwani na ubunge upi ambao ni local election?
Fasili ya diwani, mbunge, na bunge, kwa mujibu ya Kamusi ya Kiswahili Sanifu ya Oxford, Toleo la Pili chapisho la mwaka 2012 (na ukitaka namba ya Cheti cha Ithibati kutoka Wizara ya Elimu na Utamaduni nitakupatia, lol) ni kama ifuatavyo;
Nani kati ya mbunge na diwani anayekuhusu zaidi kama mwananchi?
Kwani mahakama kuu imesema kuwa hukumu yake ina-apply kwa wabunge tuu?
Aliyejiandikisha Chake Chake ana haki ya kupinga matokeo ya Ubunge wa Karatu kisheria, kwa sababu kimantiki Mbunge wa Karatu akiwa Bungeni atajadili na kuya-impact maisha ya Chake Chake.
Pia ni wajibu wa kila mwananchi kuhakikisha sheria za nchi zinatekelezwa
Mkuu EMT unaweza kusoma hapa na hii ndio basis ya uamuzi wa majaji hao kwenye kesi hii.
Katika uamuzi wake Mahakama ya Rufani ilisema kumbukumbu za Mahakama hazionyeshi iwapo vitambulisho vya wapiga kura viliwasilishwa na kupokewa mahakamani na ikaenda mbali zaidi kwa kutilia shaka jinsi rekodi ya kadi hizo zilivyochukuliwa.
Ilisema kinachoonekana katika kumbukumbu za Mahakama ni kiambatisho na maelezo tu kuwa wajiburufani ni wapiga kura waliosajiliwa na kwamba badala yake wakili wao ndiye aliyejaribu kuthibitisha hilo kwa maelezo, badala ya vielelezo.
Ilisema Wakili wa wajibu rufaa, Alute Mughway aliwasilisha kadi za wateja wake kwa Jaji Aloyce Mujulizi kuthibitisha kuwa walikuwa wapiga kura halali, lakini Mahakama hiyo ikasisitiza kuwa utaratibu huo ni kinyume cha sheria kwa kuwa ushahidi kama huo ulipaswa uwasilishwe moja kwa moja mahakamani na utolewe na wamiliki wa nyaraka husika.
Ilisema hata kama ingethibitika kuwa wajibu rufani walikuwa wapiga kura waliosajiliwa, bado hawakuwa na haki kisheria kufungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi kwa madai ya mrufani kutumia lugha za matusi kwenye kampeni zake."
Mahakama kuu tena?
Sorry, I meant Mahakama ya Rufaa.
Hapana! Pamoja na kwamba sikubaliani na argument ya Prof. Shivji sidhani kama amewatusi majaji waliotoa hukumu.
It is normal in the legal field to criticise court judgements. Ndiyo maana kwenye nchi za watu controversial decision kama hii inazalisha articles hata 500 within the first few months, some applauding, others, criticising, the decision.
It is normal kabisa na kufanya hivyo haina maana kuwa mtu ana-question intergrity ya jaji aliyetoa hukumu.
Tumefundishwa kukubaliana kutokubaliana. Kwa vile sijakubaliana na wewe haina maana kuwa nimekudharau au nimekutusi.
You will still be my learned brother/sister. lol.[/hata kama mimi si mwanasheria haki imetendeka hata kama haikufuata sheria Lema alichaguliwa kwa kura nyingi,na wala hakumtukana batilda,ina maana wao watu watatu tu ndio walisikia hayo matusi,kwa nini wasitoe mkanda kuonyesha mahakamani,cha msingi ni haki sio sheria,
Okay, no problem.
Lakini, je, unaona ingefaa zaidi kama mahakama ingekuwa more specific?
hiyo statement uliyoiweka mwishoni, inabeba sababu ya kwa nini wafungua kesi wengi mahakamani huwa wanashindwa kesi hizo na kutakiwa kulipa gharama za kesi. Wengi huwa hawatazami legal reasons za kufawafanya washinde, wengi huwa wanajikita kwenye social reasons na kusahau kuwa only legal reasons will make them win any case.lol. Kwa hiyo wewe ukim defame NN basi mie nikamshtaki kwa sababu ni wajibu wangu kuhakikisha kuwa sheria za nchi zinatekelezwa?
A court of law is a court of justice and not an academy of law.
Neither is a court of law a place to test your legal theories.
Thus, to maintain an action before a court of law a litigant must assert interference with or deprivation of, or threat of interference with or deprivation of, his/her own right.
The fact that you have a right sue anyone does not mean that you have the legal reasons to do so.
Vp kuhusu kipengele kilichotumika katika kufungua kesi husika?
Inawezekana kabisa kuna kipengele kinachompa mpiga kura haki ya kufungua kesi huku kikiambatanisha mazingira, lakini labda wapiga kura hao (walalamikaji) walikuja kufungua kesi wakitumia kipengele kingine (pacha), ambacho hakitoi wide ground kwa mpiga kura, mnaliongeleaje hili?
Shivji kaamua kuchafua hewa kwa makusudi kabisa na hii ni dhambi ambayo itamrudia tu.
Hii ni 2012 awareness ya binadamu inazidi kuongezeka kila sekunde inayopita.
Tutarajie kuna madudu mengi kutoka kwa watu wenye majina kama Shivji.
Ni kweli awareness ni kubwa ndiyo maana watu wanaona wazi upuuzi uliomo kwenye sehemu ya hukumu ya kesi ya Lema. Kama huelewi tafsiri ya mbali zaidi ya anachokisema Shivji, katika masuala ya uchaguzi na mengine kwa ujumla ....nguvu ya umma kwanza, nguvu ya umma ni wananchi (wapiga kura) na si mgombea. Hoja ya Shivji na wengine iko wazi, tena nashangaa watu wa Chadema kupingana nayo wakati ipo upande wa kutetea haki za wengi (wapiga kura) dhidi ya wachache (wagombea).
Shivja anaijadili sheria ilivyo lakini hakuangalia sheria hiyo katika uchaguzi huo wanaopinga matokea waliathiriwaje na madai yao kitu ambacho mahakama imeegemea kutoa hukumu yake. Hao wapiga kura hawakutukanwa na Lema sasa wanasimamaje kudai haki mahakamani wakati aliyetukanwa hakulalamika wala kuwa mmoja wapo wa mashahidi. Pamoja na ugwiji wa sheria katika hali kachemka sana.