Prof. Shivji apinga sehemu ya hukumu ya kesi ya Lema

Prof. Shivji apinga sehemu ya hukumu ya kesi ya Lema

Halafu ngoja kwanza, hivi udiwani na ubunge upi ambao ni local election?

Fasili ya diwani, mbunge, na bunge, kwa mujibu ya Kamusi ya Kiswahili Sanifu ya Oxford, Toleo la Pili chapisho la mwaka 2012 (na ukitaka namba ya Cheti cha Ithibati kutoka Wizara ya Elimu na Utamaduni nitakupatia, lol) ni kama ifuatavyo;

Nani kati ya mbunge na diwani anayekuhusu zaidi kama mwananchi?

Kwani mahakama kuu imesema kuwa hukumu yake ina-apply kwa wabunge tuu?
 
Aliyejiandikisha Chake Chake ana haki ya kupinga matokeo ya Ubunge wa Karatu kisheria, kwa sababu kimantiki Mbunge wa Karatu akiwa Bungeni atajadili na kuya-impact maisha ya Chake Chake.

Pia ni wajibu wa kila mwananchi kuhakikisha sheria za nchi zinatekelezwa

lol. Kwa hiyo wewe ukim defame NN basi mie nikamshtaki kwa sababu ni wajibu wangu kuhakikisha kuwa sheria za nchi zinatekelezwa?

A court of law is a court of justice and not an academy of law.

Neither is a court of law a place to test your legal theories.

Thus, to maintain an action before a court of law a litigant must assert interference with or deprivation of, or threat of interference with or deprivation of, his/her own right.

The fact that you have a right sue anyone does not mean that you have the legal reasons to do so.
 
Mkuu EMT unaweza kusoma hapa na hii ndio basis ya uamuzi wa majaji hao kwenye kesi hii.

Katika uamuzi wake Mahakama ya Rufani ilisema kumbukumbu za Mahakama hazionyeshi iwapo vitambulisho vya wapiga kura viliwasilishwa na kupokewa mahakamani na ikaenda mbali zaidi kwa kutilia shaka jinsi rekodi ya kadi hizo zilivyochukuliwa.
Ilisema kinachoonekana katika kumbukumbu za Mahakama ni kiambatisho na maelezo tu kuwa wajiburufani ni wapiga kura waliosajiliwa na kwamba badala yake wakili wao ndiye aliyejaribu kuthibitisha hilo kwa maelezo, badala ya vielelezo.


Ilisema Wakili wa wajibu rufaa, Alute Mughway aliwasilisha kadi za wateja wake kwa Jaji Aloyce Mujulizi kuthibitisha kuwa walikuwa wapiga kura halali, lakini Mahakama hiyo ikasisitiza kuwa utaratibu huo ni kinyume cha sheria kwa kuwa ushahidi kama huo ulipaswa uwasilishwe moja kwa moja mahakamani na utolewe na wamiliki wa nyaraka husika.

Ilisema hata kama ingethibitika kuwa wajibu rufani walikuwa wapiga kura waliosajiliwa, bado hawakuwa na haki kisheria kufungua kesi kupinga matokeo ya uchaguzi kwa madai ya mrufani kutumia lugha za matusi kwenye kampeni zake."

Naona kama suala linaloleta mgogoro hapa siyo ratio decidendi (reason) ya hukumu bali orbiter dicta (said in passing) ya hukumu.
 
Hapana! Pamoja na kwamba sikubaliani na argument ya Prof. Shivji sidhani kama amewatusi majaji waliotoa hukumu.

It is normal in the legal field to criticise court judgements. Ndiyo maana kwenye nchi za watu controversial decision kama hii inazalisha articles hata 500 within the first few months, some applauding, others, criticising, the decision.

It is normal kabisa na kufanya hivyo haina maana kuwa mtu ana-question intergrity ya jaji aliyetoa hukumu.

Tumefundishwa kukubaliana kutokubaliana. Kwa vile sijakubaliana na wewe haina maana kuwa nimekudharau au nimekutusi.

You will still be my learned brother/sister. lol.[/hata kama mimi si mwanasheria haki imetendeka hata kama haikufuata sheria Lema alichaguliwa kwa kura nyingi,na wala hakumtukana batilda,ina maana wao watu watatu tu ndio walisikia hayo matusi,kwa nini wasitoe mkanda kuonyesha mahakamani,cha msingi ni haki sio sheria,
 

EMT, Richard,

..je, nitakuwa nimekosea nikidai kwamba mwaka 82, katika hukumu yake dhidi ya Mgonja, mahakama ya rufaa ilifanya makosa kwa kumpa haki mpiga kura yeyote yule, kupinga matokeo ya uchaguzi wowote, kwa sababu zozote zile??

Ndiyo maana kwenye kesi ya Lema Mahakama ya Rufaa imesema kuwa kesi ya Mgonja wa wrongly decided.

Labda mahakama ingeenda mbali zaidi na kueleza why the thought it was wrong decided.

May be tatizo ni kwamba hukumu ya Lema is not detailed. Waheshimiwa majaji kama vile walifanya summary tuu ya principles.

Kwa hiyo, inakuwa ngumu kujua how they analysed the issues and applied the relevant laws, japokuwa issues zilikuwa straightforward.

But it is good to have these sort of decisions. Kesi kama hizi zinaamsha wale waliolala.

Subiri bunge likianza kuna mbunge atatoa povu bungeni kuwa Mahakama ya Rufaa imeingilia mamlaka ya bunge ya kutunga sheria.
 
Vp kuhusu kipengele kilichotumika katika kufungua kesi husika?
Inawezekana kabisa kuna kipengele kinachompa mpiga kura haki ya kufungua kesi huku kikiambatanisha mazingira, lakini labda wapiga kura hao (walalamikaji) walikuja kufungua kesi wakitumia kipengele kingine (pacha), ambacho hakitoi wide ground kwa mpiga kura, mnaliongeleaje hili?
 
kwa uelewa wangu, Shivji anataka mpiga kura awe na haki ya kupinga mtokea ambacho ndo kilitokea kwa kesi ya Lema, lakini anasahau kuwa kurudishiwa ubunge kwa Lema hakikutokana na kama mpiga kura ana haki ya kupinga matokea au la, bali madai ya wapiga kura wale hayakuwa na athari yoyote kwenye matokeo ya uchaguzi.
 
Okay, no problem.

Lakini, je, unaona ingefaa zaidi kama mahakama ingekuwa more specific?

Not only specific but also in detail.

Kwanza tuna wabunge wa kuchaguliwa, kuteuliwa na wanaopita bila kupingwa. Je, hukumu yao una-apply kwa wabunge wote?

Nani atawashtaki wabunge wa kuteuliwa au wale wanaopita bila kuoingwa kama Waheshimiwa Mizengo Pinda na January Makamba?

As it stands, hukumu inaonyesha kama ina-apply both kwa wabunge na madiwani. Lakini ingekuwa more specific, the better.

Kuna suala la "election litigation is not a public interest litigation" Labda wangefafanua kidogo. Does this include all election litigation?

Lakini kama nilivyosema kwenye ile thread nyingine, tunaweza kusema kuwa there is an important public interest in clarifying the legitimacy of the ballot.

However, for electoral policy to be policed by what are, in effect private civil law actions brought at the expense of the litigant (plaintiff), cannot be acceptable.
 
lol. Kwa hiyo wewe ukim defame NN basi mie nikamshtaki kwa sababu ni wajibu wangu kuhakikisha kuwa sheria za nchi zinatekelezwa?

A court of law is a court of justice and not an academy of law.

Neither is a court of law a place to test your legal theories.

Thus, to maintain an action before a court of law a litigant must assert interference with or deprivation of, or threat of interference with or deprivation of, his/her own right.

The fact that you have a right sue anyone does not mean that you have the legal reasons to do so.
hiyo statement uliyoiweka mwishoni, inabeba sababu ya kwa nini wafungua kesi wengi mahakamani huwa wanashindwa kesi hizo na kutakiwa kulipa gharama za kesi. Wengi huwa hawatazami legal reasons za kufawafanya washinde, wengi huwa wanajikita kwenye social reasons na kusahau kuwa only legal reasons will make them win any case.
 
Vp kuhusu kipengele kilichotumika katika kufungua kesi husika?
Inawezekana kabisa kuna kipengele kinachompa mpiga kura haki ya kufungua kesi huku kikiambatanisha mazingira, lakini labda wapiga kura hao (walalamikaji) walikuja kufungua kesi wakitumia kipengele kingine (pacha), ambacho hakitoi wide ground kwa mpiga kura, mnaliongeleaje hili?

Wangeweza kufungua chini ya Ibara 26(2) ya Katiba inayosema kuwa "Kila mtu ana haki, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria, kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba na sheria za nchi."

Kwa mujibu wa Mahakama ya Rufaa "Article 26(2) of the Constitution..permits any person to bring a public interest litigation."

Lakini walalamikaji na hasa Mussa Mkanga labda aliona hakuna haja hiyo kwa sababu tayari alishashinda kesi nyingine kwa kutumia kifungu hicho hicho cha sheria ya uchaguzi (refer kesi ya Makongoro Nyerere).

Na kama Mkanga angeshinda kesi ya Lema, kuna uwezekano jamaa angefungua tena kesi kama in future angeshinda tena mgombea wa upinzani. Ila sasa kapigwa stop na Mahakama ya Rufaa.
 
naomba kuwa mmoja wa wanaaomshangaa shivji...hivi ni kweli sheria inaruhusu kufunguliana kesi? nimetukanwa mimi wewe umeumia hata ukaenda mahakamani? haki ya mungu tena haya filauni
 
Shivji kaamua kuchafua hewa kwa makusudi kabisa na hii ni dhambi ambayo itamrudia tu.
Hii ni 2012 awareness ya binadamu inazidi kuongezeka kila sekunde inayopita.
Tutarajie kuna madudu mengi kutoka kwa watu wenye majina kama Shivji.

Ni kweli awareness ni kubwa ndiyo maana watu wanaona wazi upuuzi uliomo kwenye sehemu ya hukumu ya kesi ya Lema. Kama huelewi tafsiri ya mbali zaidi ya anachokisema Shivji, katika masuala ya uchaguzi na mengine kwa ujumla ....nguvu ya umma kwanza, nguvu ya umma ni wananchi (wapiga kura) na si mgombea. Hoja ya Shivji na wengine iko wazi, tena nashangaa watu wa Chadema kupingana nayo wakati ipo upande wa kutetea haki za wengi (wapiga kura) dhidi ya wachache (wagombea).
 
Ni kweli awareness ni kubwa ndiyo maana watu wanaona wazi upuuzi uliomo kwenye sehemu ya hukumu ya kesi ya Lema. Kama huelewi tafsiri ya mbali zaidi ya anachokisema Shivji, katika masuala ya uchaguzi na mengine kwa ujumla ....nguvu ya umma kwanza, nguvu ya umma ni wananchi (wapiga kura) na si mgombea. Hoja ya Shivji na wengine iko wazi, tena nashangaa watu wa Chadema kupingana nayo wakati ipo upande wa kutetea haki za wengi (wapiga kura) dhidi ya wachache (wagombea).

Watu wa Chadema wametoka wapi? Si muijadili hiyo sheria tu bila kuweka siasa kama magwiji ya sheria hapa JF akina EMT walivyofanya?

Wengine kusoma na ku like inatosha!
 
Last edited by a moderator:
Shivja anaijadili sheria ilivyo lakini hakuangalia sheria hiyo katika uchaguzi huo wanaopinga matokea waliathiriwaje na madai yao kitu ambacho mahakama imeegemea kutoa hukumu yake. Hao wapiga kura hawakutukanwa na Lema sasa wanasimamaje kudai haki mahakamani wakati aliyetukanwa hakulalamika wala kuwa mmoja wapo wa mashahidi. Pamoja na ugwiji wa sheria katika hali kachemka sana.

Mkuu msome vizuri Prof Shivji yeye anaelezea tafsiri za sheria wewe umejikita zaidi kwenye ushabiki wa kisiasa.
 
Naogopa kuongea pumba...sitachangia chochote
Ila naomba modes waiweke hii thread kuwa sticky...
 
Back
Top Bottom