Prof. Shivji apinga sehemu ya hukumu ya kesi ya Lema

Prof. Shivji apinga sehemu ya hukumu ya kesi ya Lema

Sawa professor shivji,wanasema Lema alitumia matusi kwenye kampeni,lakini je matusi hayo yaliathiri vp uchaguzi na huyo mchaguaji aliathirika vp?Mimi nadhani mahakama imewatendea haki wanachi wa Arusha mjini kuwarudishia mwakilishi wao kipenzi mjengoni.Na tumuunge mkono mbunge huyo kimawazo,kiushauri ili Arusha mjini irudi juu
 
Nimeyakuza na kuyapaka rangi maneno yako hapo juu ili kuonyesha msisitizo.. infact hizo ndio sifa zako kwa sababu huoni hata hoja iliyopo nyumba ya wanaopinga hukumu hii.. umeshindwa kuona jinsi mahakama ilivyopinda sheria(bila kujali uzuri au ubaya wa sheria husika) na umeshindwa kuona hata mawakili na wanasheria waliobobea wanapotoa matamshi kwaba"""" HAPA MAHAKAMA IMETUNGA SHERIA MPYA""""

Kwanini kwa makusudi uchagua maneno hayo machache bila kuzingatia maneno yaliyotangulia?
Haya hapa by Mag3

Sisi tuliobahatika kupata exposure kwa wenzetu ambako demokrasia imekomaa, no voter would dream of going to court to challenge an election result based on mgombea anayemtaka kushindwa uchaguzi kwa sababu alikashifiwa kwenye kampeni huku mhusika hayuko tayari hata kuwa shahidi mahakamani.
 
Last edited by a moderator:
EMT.
Mimi sio mtaalamu wa sheria lakini kwa jinsi nilivyofuatilia wataalamu wengi wa sheria wanachopinga ile statement ya "mpiga kura hana haki ya kufungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi"

Hata mimi naona ulakini katika hapo, mahakama ilipotumia statement kuamua rufanu ile imekuwa kama wametunga sheria mpya.

Hujamalizia hiyo statement, angalia hapa chini
So a voter has no right to petition and challenge the election results where his rights were not infringed.
 
Kupinga au kuunga mkono kwenye masuala ya kisheria ni jambo la kawaida ndiyo maana kukawa na upenyo wa kukata rufaa. Kimsingi masuala ya kisheria siyo sawa na hesabu ambapo moja na moja ni mbili. Kwenye sheria hakuna kukosea au kupatia hadi hukumu ya mwisho kwenye ngazi ya mwisho. Hivyo Shivji hajakosea sawa na akina Lissu wanaopingana na hoja ya Shivji.

Mkuu, naomba niungane nawe katika hili kwamba kila upande unajiona kwamba uko sahihi. Tatizo la sheria ni kukariri rejea za maamuzi yaliyopita. Ati, mbona tangu miaka hiyo hilo halijawahi kutenguliwa? Yaani hata kama lilikuwa na makosa?

Kwa nini basi maamuzi haya mapya yasiwe ndiyo mwanzo wa rejea mpya yenye busara ndani yake ili kuzuia ufunguaji holela wa kesi za kupinga matokeo ya chaguzi za ubunge unaoendelea kufanyika?

Yaani watu wanafungua kesi kiushabiki na kujipendekeza. Ati katukanwa mwingine, wewe wa pembeni ndiye unayeusikia uchungu kuliko yeye mwenyewe aliyetukanwa ambaye hata kuja mahakamani kutoa ushahidi amekataa?

Hakika TZ ina safari ndefu hadi kufikia nchi ya ahadi. Binafsi nawapongeza hawa majaji wa mahakama ya rufaa walioonesha njia ili watakaofuata waifuate, na nimesikitishwa na hao wengine pamoja na Prof. Shivji, msomi mzuri asiyependa mabadiliko.
 
kesi ya ched mgonja ...next time tutasikia wana-refer hukumu ya kesi ya Dowans miaka hiyo..nchi ikiwa ukiwa ....Nauguza jeraha la risasi.


Hapana! Pamoja na kwamba sikubaliani na argument ya Prof. Shivji sidhani kama amewatusi majaji waliotoa hukumu.

It is normal in the legal field to criticise court judgements. Ndiyo maana kwenye nchi za watu controversial decision kama hii inazalisha articles hata 500 within the first few months, some applauding, others, criticising, the decision.

It is normal kabisa na kufanya hivyo haina maana kuwa mtu ana-question intergrity ya jaji aliyetoa hukumu.

Tumefundishwa kukubaliana kutokubaliana. Kwa vile sijakubaliana na wewe haina maana kuwa nimekudharau au nimekutusi.

You will still be my learned brother/sister. lol.
 
Niseme tu machache...
  • Academicians are good at critics but when we welcome them on board they do the same 'mistakes' they used to criticize. Hapa nampongeza Mhe. Benjamin Mkapa aliyefika hatua ya kuwaita baadhi ya maprofessor kuwa uchwala maana waliishia critics bila kumshauri. Kwa hili niishie hapa nisiende nje ya mada.
  • Kuhusu hili la Rufaa ya Lema, mimi nasema hukumu ni sawa kwa busara za jopo la majaji na ninaomba ninikuu msingi wa Rufaa kama ulivyo kwenye hukumu.

...'So a vote has no right to petition and challenge the election results where his rights were not infringed'.


  • Sasa sio kwamba mahakama imeondoa haki ya mpiga kura kupeleka shitaka mahakamani, hapana, bali mpiga kura hana haki kupinga matokeo pale ambapo haki yake haijaathirika. Sasa suala hapa sio mbona hukumu ya Mgonja...tuambiwe ni lini mahakama imetengua...Common, there is always first time experience; and this is it! Mimi naona premises za judgement ziko very clear kwa mtu ambaye ana nia ya kuelewa na si kubisha (critical in everything).
  • Hivi mahakama si zina friends of court na hawa wasomi ni washauri mbona nao wanakuwa wanasiasa sasa?
  • Nimalizie kwa kusema kwamba moja ya taaluma inayorudisha nchi yetu nyuma ni Wanasheria..Samahani kwa kusema hili. Kwanza wamekuwa wanasiasa zaidi na pia mapenzi kwa pesa yamekuwa makubwa. Hona wezi wa nchi hii kesi zao zinavyopigwa dana dana. Hivi jamani legal ethics huwa zinasemaje? Is it moral and ethical to look for loopholes to defend someone whom you know for sure is guilty? Najua kuna wanasheria wachache wazuri lakini wengi ni pesa mbele. Mbaya mahakimu na majaji nao wameingia kwenye mchezo huu mchafu.
  • Mimi sio mwanasheria lakini nimpenzi wa kujifunza sheria na nina marafiki wengi wa sheria. Majaji ambao Tanzania wanaaminika ni majaji wa mahakama ya Rufaa, kwanza wanalipwa vizuri, wameridhika na pia wanaudhoefu.
  • Prof, Shivj is one of good and respected opinion maker inabidi awe mwangalifu katika kutoa comments zake vinginevyo heshima yake itashuka maana kizazi hiki hakiangalii wewe ni nani bali unasema nini. Akawaulize maprof. wenzake wa sheria waliofungua practice mjini huku wakishuhudia anguko la wateja wao wakiwagalagaza na kupewa changamoto kali na waliokuwa wanafunzi wao mahakamani.
 
Hii thread ni muhimu sana kwa kujifunza.

Sisi ambao hatujui sheria nashauri tukae pembeni na kuwaacha wenye ujuzi watuelemishe.

Hili suala halina siasa ndani yake wala halina uhusiano na Lema kurudishiwa ubunge au kutokurudishiwa. Hii ni tafsiri kubwa zaidi ya siasa za CCM na CHADEMA.

Tusiivuruge kwa mapenzi ya vyama vya siasa na badala yake tuwaachie wanaojua kuliko sisi watuelemishe.

naomba nikupe tano mkuu...
 
Kitu ambacho ni interesting zaidi katika hii kesi ni kwamba jambo la msingi la matumizi ya matusi na lugha za kibaguzi halijapewa kabisa nafasi na mahakama, badala yake technicalities ndio zilizoamua final verdict.
Wakati mwingine ndio maana naona hizi kazi ambazo maamuzi yake hayana standard measures ni za headache sana...
 
Shivja anaijadili sheria ilivyo lakini hakuangalia sheria hiyo katika uchaguzi huo wanaopinga matokea waliathiriwaje na madai yao kitu ambacho mahakama imeegemea kutoa hukumu yake. Hao wapiga kura hawakutukanwa na Lema sasa wanasimamaje kudai haki mahakamani wakati aliyetukanwa hakulalamika wala kuwa mmoja wapo wa mashahidi. Pamoja na ugwiji wa sheria katika hali kachemka sana.

Shivji kalelewa katika mazingira ya kuamini aliyepo madarakani anaweza kufanya chochote akitakacho ikiwemo kula hata watu wake na hata wakilalamika hawapaswi kusikilizwa mpaka huyu mtu atakapoondoka madarakani. Yawezekana anaongea kwa kutaka aonewe huruma katika kuganga njaa. Anasema hivyo kwa kuwa walioshindwa katika kesi ni Nape's Group, wangekuwa wengine wala asingeongea huyu jamaa. Nilikuwa nam'salute' sana lakini from now onward nimegeukia kwingine. Huyu hawezi kutusaidia kutatua matatizo ya wananchi wa nchi hii au kwa vile anafanana na wezi nini?
 
shivji anachemka katika hili

Kwa lipi na kivipi kachemka? Haya ndo aina ya majibu ya ujumlajumla aliyotegemea Kiranga kutolewa. Kama hatuna uzoefu au ideal tu na maswala haya ya kisheria bora tuwe wasomaji tu wa comments za wanaofahamu, mwisho wa siku tutaongeza kitu kichwani.
 
Last edited by a moderator:
Unaanza kwa kusema hukushiriki vilivyo katika mjadala, maana yake hujui nini kilisemwa na kusemwuka.

Halafu una offer vi opinion and whimsical witticism, bila kujua unaongelea nini.

Exactly my sentiments.

Your post is a disgrace, from head to toe. Now don't make me dissect it.
...kindly dissect it kwa faida ya jukwaa...
 
Hivi kesi ya mtu kutukanwa inaweza kurithishwa kwa mtu mwingine? Ok kama ni hivyo basi ilirithishwaje wakati Dr Batilda bado yuko hai? Mahakama haina umbali, Dr Batilda leo ni balozi wa Tanzania nchini Kenya sio lazima aje kwa ndege hata kwa commuter bus anafika MAPEMA TU. Nini kilishindikana kwa yeye kufungua kesi, kuja,nk.


Shivja anaijadili sheria ilivyo lakini hakuangalia sheria hiyo katika uchaguzi huo wanaopinga matokea waliathiriwaje na madai yao kitu ambacho mahakama imeegemea kutoa hukumu yake. Hao wapiga kura hawakutukanwa na Lema sasa wanasimamaje kudai haki mahakamani wakati aliyetukanwa hakulalamika wala kuwa mmoja wapo wa mashahidi. Pamoja na ugwiji wa sheria katika hali kachemka sana.
 
Hata kama Shivji yuko sahihi kuhusu haki ya mpiga kura, bado kesi husika ilikuwa ya kutunga na hawakuweza kuthibitisha madai yao! Pure CCM political games! Ni kupoteza wakati kujadili case zinazotungwa LUMUMBA!

This is what I was talking about.

What Shivji is talking about is larger than Lema and has no bearing on reinstating Lema.

Shivji is talking about larger issues regarding voters rights. I hope you understand the bounds and that one could be advocating for voter rights without threatening the reinstating of a two bit MP.
 
sheria za vioja hatutaki.mfano.mie naishi Tabora kata ya kanyenye na nimejiandikisha kanyenye.niende nikapinge matokeo ya musoma mjini kwa kuwa tu mie ni mpiga kura Tabora.
 
Haya ni maoni yake ,sheria nyingi hapa tanzania zina jikanyaga zenyewe ,tumeona uteuzi wa majaji ,na sheria nyingine nyingi hapa tumeona moja tu haki ya mpiga kura na maslahi yake kwenye chaguzi tujadili katiba ijayo iliwekeje hili kwa sababu watu wamekuwa wanatumika vibaya mtu mwenye maslahi na kesi haonekani huku wapiga kura wao ndio wanaonekana mahakamani ,kimsingi kama mwenye maslahi haoni sababu ya kuja mahakamani kuna sababu gani ya kuwa na kesi ,hapa tuache hili liwe fundisho kwa wapiga kura wanasimama mahakamani ,kwa niaba ya mwenye kesi ,inakuwaje mimi nimebaka siji mahakamani natuma wapambe wenye uchungu na mimi na wanaofurahia kubaka waje kwenye shauri . wakati huo naendeleza mikakati ya kubaka sehemu nyingine .
 
Kwa hiyo mpigakura aliejiandikisha Chakechake ana HAKI ya kupinga matokeo ya udiwani Ngara? Kumbuka kuwa mpigakura aliejiandikisha Chakechake hawezi kupiga kura ya ubunge au udiwani Ngara!

Unalinganisha udiwani na ubunge?
 
sheria za vioja hatutaki.mfano.mie naishi Tabora kata ya kanyenye na nimejiandikisha kanyenye.niende nikapinge matokeo ya musoma mjini kwa kuwa tu mie ni mpiga kura Tabora.

Kwanza inabidi ieleweke unaenda kupinga uchaguzi wa aina gani.

Na pili, kama una compelling evidence kwa nini usiweze?
 
Back
Top Bottom