Prof. Shivji apuuzwe, ni kigeugeu. Alisaliti machapisho yake ya serikali tatu wakati wa bunge la katiba

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Prof. Shivji haaminiki tena huwa anatumika na ni kigeugeu hivyo apuuzwe ktk hoja zake anatoa kupinga ubia wa serikali ya Tanzania na DP World kuendesha bandari..

Kama mnakumbuka prof. Shivji ameandika machapisho mengi sana kuhusiana na utata na udhaifu wa muundo wa muungano wetu wa serikali mbili. Alikuwa mkosaoji mkubwa sana wa muundo huu wa muungano.

Lakini (sina ushahidi Ila nina 80%) mwaka 2014 baada ya kupewa kitu kidogo prof. Shivji alibadilika na kuyasaliti machapisho yake yaliyokuwa yanapendekeza serikali tatu. Akaiunga mkono ccm ktk kuutetea muundo wa muungano wa serikali mbili.

Kwahiyo hata ktk suala hili la DP World ninaamini prof. Shivji anatumika.

Apuuzwe prof. huyu.
 
Ungeendelea na mjadala wa huo mkataba kupinga hoja zake ningekupa maua badala ya kutuhumu
 
Serikali ishatolea ufafanuzi kuwa itazirekebisha hizo kasoro. Ondoa hofu. Lkn prof. huyu uchwara anataka kuurejesha umaarufu aliokuwa nao hapo awali kwa kutumia suala DP World
 
Inaonekana hata unachoandika hakitoki Moyoni mwako....mna agenda ya kumuangusha mama.Ukiona watu wengi wanacomment kuchambua mapungufu ya wazi kwenye makubaliano maana yake wanasupport juhudi anazofanya.Mmeamua kuitundika serikali msalabani halafu mnajifanya mnaitetea.
 
Sababu ni hiyo tu au kuna nyingine?
 
Bado naona watu wanajichanganya kwenye swala la DP world, ukiwaambia waoneshe uhalisia kwa kuandamana, hawatokei.

Mitandaoni kelele nyingi
Inatakiwa waliouza bandari ndio wakae mbele kuwazuia waandamanaji. Kinachotokea watu wakiandamana wanakutana na vyombo vya dola, kwani hivyo vyombo vya dola ndio wameuza bandari? Mbona walioandamana kuunga mkono hatukuona wakivamiwa na vyombo vya dola ili tuone ushujaa wao?
 
Serikali ishatolea ufafanuzi kuwa itazirekebisha hizo kasoro. Ondoa hofu. Lkn prof. huyu uchwara anataka kuurejesha umaarufu aliokuwa nao hapo awali kwa kutumia suala DP World
Wewe Prof. unamwona ni uchwara? Sasa wewe utakuwa nani?
 
mama.Ukiona watu wengi wanacomment kuchambua mapungufu ya wazi kwenye makubaliano maana yake wanasupport juhudi
Waongee watu wengine lkn siyo huyu prof ambaye alionesha mapungufu ya muundo wa muungano wetu kwa miaka kibao mpk akayatumia kufundishia wanafunzi lkn akayasaliti. Tutamuamini vipi ktk suala hili?
 
Nenda kaandamane acha visingizio
 
Serikali ishatolea ufafanuzi kuwa itazirekebisha hizo kasoro. Ondoa hofu. Lkn prof. huyu uchwara anataka kuurejesha umaarufu aliokuwa nao hapo awali kwa kutumia suala DP World
Uhuru wako wa kubwabwaja humu unampa Shivji the same right. Wewe huna haki zaidi ya wengine kutoa maoni yao. Ukiroboto wenu hauwafanyi muwe na haki zaidi kutetea rasilimali hasa za Tanganyika
 
Wewe Prof. unamwona ni uchwara? Sasa wewe utakuwa nani?
Kwa heshima alivyokuwa amejijengea hapo awali kwa machapisho na mafundisho yake halafu akaja kuyasaliti. Anastahili kuitwa uchwara. Au hujui maana ya uchwara??
 
Yaani tuache kuwasikiliza watu wa maana tuwasikilize watu ovyo kama nyie?
 
Uhuru wako wa kubwabwaja humu unampa Shivji the same right. Wewe huna haki zaidi ya wengine kutoa maoni yao. Ukiroboto wenu hauwafanyi muwe na haki zaidi kutetea rasilimali hasa za Tanganyika
Hofu yangu ni kwamba anaweza kuwa ametumika kama alivyotumika ktk bunge la katiba mpk akasaliti machapisho ya taaluma yake
 
Yaani tuache kuwasikiliza watu wa maana tuwasikilize watu ovyo kama nyie?
Prof. Shivji ni mtu wa hovyo sana. Imagine amewafumdiaha wanafunzi kibao wa sheria kwamba hakunaga muungano wa serikali mbili lkn alipopewa kitu kidogo akayakana hadharani machapisho yake. Prof uchwara huyu
 
Kwahili la unafiki wa huyo mzee uko sahihi, ila kwa lile la bandari jana, Shivji yuko sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…